Kama umeshawahi kutamani kuwa na mikono zaidi ya miwili, basi kifaa hiki ni kwa ajili yako.
The Luna TFT panel, kifaa kingine kutoka kwa watengenezaji wa TIS Smart Home, kina sifa kadhaa zinazoifanya kuwa ni suluhisho la kipekee, na bora. Kuna mionekano tofauti ya kuchagua kwa kifaa hiki, ambacho kinauwezo wa kuondoa uhitaji wa swichi zote za taa, thermostats za ukutani, vyombo vya sauti, na kuongeza na kupunguza sauti, swichi za mapazia, vifaa vya ulinzi, na sifa zingine nyingi na kukupatia zote katika panel moja nzuri.
Panel hii inapatikana katika rangi nyeusi au nyeupe; lakini hata hivyo, skrini yake ya LED inaweza kubadilishwa kadri upendavyo ili kuendana na muonekano wa ndani kwako.
Tuchunguze sifa zake sasa ili uweze kujionea uwezo wake mwenyewe.
Luna TFT panel ina kurasa 3, kila moja inakuwa na amri 6 (swichi 18 kwa ujumla), kwa ajili ya kuendesha taa zako bila kikomo. Agana na swichi zako za kizamani za taa na uendane na dunia ya sasa ya kiteknolojia inayokimbia kwa kati huku ukiokoa umeme zaidi ya siku za nyuma.
Zaidi ya hayo, Luna TFT panel ina uwezo wa kusimamia taa za RGB na kutoa rangi 256. Unaweza kuchagua rangi unayopendelea, ukaiweka kuendana na fanisi ulizonazo ndani, ukafungua au kufunga mapazia katika chumba ili kutengeneza mazingira unayoyapendelea wewe.
Moja ya sifa za kipekee za kifaa hiki ni kwamba lugha na picha zinaweza kubadilishwa. Piga picha za taa zako, milango, madirisha au vifaa vya umeme, kisha pakia picha hizo, na ujisikie huru kuchagua jina kwa ajili yake, baada ya hapo nyumba yako itakuwa ni Rafiki yako. Hautasahau kamwe kufunga dirisha au mlango, kwa sababu kifaa cha Luna kitakukumbusha mara zote.
Mipangilio ya Luna ya kupooza na kuleta joto na katika venti inaweza kubadilishwa kulinganisha na thermostat ya kidigitali, ambayo inamaanisha kwamba inaweza kugundua joto moja kwa moja la nje na la ndani na kisha kuwekewa programu ili kuwasha/kuzima kifaa. Hebu fikiria unarudi nyumbani katika siku yenye joto kali. Unaweza kuwasha kiyoyozi ili kupooza nyumba yako kabla ya kufika kwa kutumia saa iliyo ndani ya Luna. Weka muda na utakuwa na uhakika wa kuikuta nyumba yako ikiwa katika hali ya joto safi.
Kileosura(interface) murua cha Luna kinaweza kuendesha sauti kwa kupitia matundu ya AUX, USB, redio na ya kadi ya SD. Ni jambo gani linalopendeza zaidi ya kumuona mtoto wako akiwa amelala huku akisikiliza muziki wa taratibu wenye sauti nzuri?
Pia, unaweza kuweka ufafanuzi wa hali 12 zenye hisia tofauti za joto, sauti na mwanga. Kama unataka kufanya sherehe ya jioni, au kama unataka kuwa na chakula cha jioni na mchumba wako, unaweza tu kuweka mpangilio unaopendeza kwa kutumia vidole vyako tu.
Mipangilio ya ulinzi kwa kupiga kengele katika kifaa hiki pia ni imara. Mipangilio hii inahusisha kama ifuatayo: Vacation (Unapokuwa haupo nyumbani kwa muda mrefu), Away (unapokuwa haupo nyumbani kwa masaa machache), Night (Inakutaarifu kama kuna mtu yoyote anaeingia nyumbani kwako katika muda fulani), na kitufe cha Panic Button kama ikitokea kuna dharura. Jambo lingine katika usalama ni Duress password, ambapo itawasiliana na mtu wa chaguo lako ambae amewekwa kama ukibonyeza hizo namba.
Nyongeza, inakuwa inafanya kazi kama kalenda ya kisasa pia, kwa sababu inaonyesha saa na tarehe katika kila ukurasa . Itakukumbusha kumpongeza dada yako katika siku yake ya kuzaliwa kwa sababu Luna TFT panel ipo hapa kwa ajili ya kukukumbusha tarehe zako muhimu.
Sifa nyingine ya muhimu katika kifaa hiki ni mita ya umeme, ambayo inakuonyesha matumizi yako ya umeme kiujumla ya sasa na bili ya umeme.
Unaweza kutumia weather station ili kujua hali ya hewa, ikiwemo joto la nje, kiwango cha unyevu, UV index, kasi ya upepo na uelekeo wake na pia taarifa ya mvua. Vihisio (sensors) za kiafya katika panel zitakwambia kuhusu kiwango cha carbon dioxide na gesi chembechembe zingine ndani kwako ambazo ni muhimu kujua kiafya.
Kuibadilisha Luna TFT kukidhi mahitaji yako ni rahisi sana. Pale utakapotaka kubadilisha kitu, bonyeza kitufe hicho na uchague kile kinachokupendeza zaidi wewe.
Kama unavyoona, kifaa hiki cha kisasa kimetengenezwa kufanya maisha yako yawe mazuri zaidi. Ukiwa na Luna TFT panel unaweza kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja na kufanya ndoto zako kuwa kweli.
Je, Unatafuta kitu cha kubadilisha muonekano wa ndani ya nyumba yako?
The Luna 9Gni bidhaa yenye muonekano mzuri sana kutoka watengenezaji wa TIS Smart Home, imetengenezwa kuleta muonekano bora wa ndani ikiwa na umbo la kuvutia na ina uwezo wa kufanya kazi nyingi. Sifa kuu ya kifaa hiki ni kwa sababu ya coupler yake —kifaa cha kipekee cha umeme kutoka TIS—hakuna haja ya kuita fundi umeme kukufungia waya za ziada kwenda kwenye swichi zako zilizo mbali kutoka kwenye boksi la umeme; Luna 9G ina uwezo wa kuwasha na kuzima mfumo wa taa zako kutoka katika chumba chako.
Unaweza kubadilisha swichi za taa zako zote chumbani na kuwa panel moja tu na kuokoa muda na umeme kwa kufurahia teknolojia hii inayotumika kwa wingi zaidi. Ikiwa na muonekano bora wa kifahari, Luna 9G inapatikana katika rangi nyeupe au nyeusi ikiwa na vitufe 9 vizuri katika kioo cha kugusa. Skrini ya LED inaweza kubadilishwa rangi yoyote kati ya rangi 265 zilizopo ili kupata rangi yako ya kipenkee uipendayo kiurahisi kabisa, inawashwa na taa za nyuma za RGB ifikapo usiku. Pia, kila kitufe cha Luna 9G kinaweza kufanya kazi tofauti kama kikibonyezwa mara mbili, hivyo kuna mengi sana yanayoweza kufanywa na panel hii ya kisasa.
Na zaidi, Luna 9G ina uwezo wa kufanya mambo 9. Unachotakiwa kufanya ni kuiwekea programu kwenye kiyoyozi, taa, mapazia, na mfumo wa sauti katika kifaa hiki na utengeneze mazingira unayoyapendelea zaidi kwa ajili ya kuleta hisia yoyote. Kwa mfano, kama unahitaji kutumia wikiendi yako kutazama filamu na Watoto wako, wekea mpangilio katika mfumo wa muziki ucheze filamu ya Madagascar, weka taa za sebuleni tayari, na uwashangaze watoto wako na mazingira mazuri kwa ajili ya filamu za nyumbani.
Unaweza kuifunga scrini kwa urahisi kwa kutelezesha tu kidole chako. Kuifungua kunafanyika kwa namna moja hiyohiyo, na unaweza kuweka muda wa kujifunga kama itahitajika. Uwezo huu unafanya kifaa hiki kiwe kinafaa kabisa kwa matumizi ya kibiashara na matumizi ya kiwandani pia; kwa mfano, inafanya kazi vyema katika vibaraza vya kwenye mahoteli, migahawa na hospitali pia.
Na mwisho, kutokana na uwezo wa Luna 9G wa infrared, inawezekana kutuma amri hizo kutoka kwenye rimoti. Jambo hili linaongeza thamani kwa wale ambao wangependa kuendesha nyumba zao kwa kutumia vitufe na sio kioo. Jambo zuri ni kwamba kwa matumizi haya mengi, Luna 9G itakuwa inapendwa na kila mtu.
Sasa ni muda wa kuruhusu kifaa kimoja kidogo kilete mabadiliko makubwa maishani kwako.
Ni Kitandani au Kituo cha Amri?
Kampuni ya TIS Smart Home imetengeneza kifaa cha kufanya chumba chako cha kulala kuwa kama vile kituo cha kutuma amri. Kinachohitajika kutoka kwako tu ni kifaa chetu cha Luna Bedside Panel, na unaweza kusimamia chumba chako chote ukiwa umefurahia kitandani kwako. Kifaa hiki kinaweza kubadilisha hali ya joto, taa, na mifumo mingine, na kuweza kutengeneza mazingira ya kuvutia ndani ya chumba chako cha kulalia.
Ukiwa na Luna Bedside panel, ni rahisi sana kusimamia joto pamoja na spidi ya feni katika chumba chako. Je, umechoka kuamka mara kwa mara pale joto linapozidi? Achana na “Kuamka kwenda kuwasha/kuzima feni” kila mara, na ubadilishe vifaa vyako vya joto kufikia joto unalopendelea kwa kugusa na kidole tu. Ni haki yako kulala kwa amani.
Ina thermostat iliyotengenezwa vizuri, Luna Bedside Panel inakupa ufanisi katika kusimamia vifaa vyako vya kupoozea. Pia, kifaa cha kuleta joto sakafuni (floor heating) inaweza kuwa ni jambo zuri kufikiria kuweka pia kwa siku zile za mvua zenye baridi.
Kifaa hichi kinaweza kusimamia taa, haijalishi kama unataka kuzima taa zote kwenye chumba au unataka kuzima taa moja tu ya kusomea pembeni ya kitanda chako, unaweza kuzima taa yoyote ile kutoka kwenye Luna Bedside Panel.
Unaweza kuweka mipangilio Nane ukiwa na Luna Bedside Panel. Hebu fikiria muda wako wa kulala. Ni nini kitapendeza zaidi ya upepo mzuri wa kutoka kwenye kiyoyozi, mwanga mdogo huku wimbo mzuri ukicheza taratibu? Au, kama wewe ni mmoja wa wale watu ambao wanahitaji kusukumwa kidogo inapofika asubuhi ili kuweza kuanza siku yao, basi Luna Bedside Panel inaweza kuwa msaada wako bora. Madirisha yatafunguliwa, jagi la kahawa litawashwa, na sauti ya nyimbo yako uipendayo itasikika na kukusaidia kuamka na kuanza siku yako kwa furaha.
Luna Bedside Panel pia ni suluhisho la kisasa kwa vyumba vya kulala hotelini, kwa sababu inatoa wigo mpana wa kubadilisha mwanga wa taa inayoweza kumsaidia mteja kuweka kila anachokipenda na kumfanya ajisikie kukaribishwa na kufurahia muda wake katika hoteli yako.
Luna Bedside Panel ina muonekano mzuri mweusi wa kisasa pamoja na vitufe 12 kwenye skrini ya kugusa itakayoendana na muonekano wa chumba chochote cha kulalia. Kila kitufe kinavutia na kina picha ndogo rahisi kimuonekano na kutumia. Pia, vitufe vinaweza kubadilishwa rangi yake na kuchagua yoyote kati ya rangi 265 unazoweza kuchagua. Fanya jambo lolote unalotaka kufanya kwenye Luna Bedside Panel; kila kitufe kinaweza kufanya jozi mbili za sheria pale kitakapobonyezwa mara mbili.
Pale utakapotumia msaidizi wako Luna Bedside Panel ndipo utakapojua kwamba hakika inakupa zaidi ya thamani yake. Jionee mwenyewe.
Kizazi Kipya cha Swichi za Kijanja Zenye Muonekano Unaopendwa na Mtumiaji
Haijalishi unatafuta vifaa hivi vya kiteknolojia kiasi gani, baadhi tu ndivyo chaguo sahihi. Mfululizo wa paneli za TIS Titan & Titania ni mfano moja wapo wa bidhaa za kijanja ambazo zinakupa muonekano mzuri na utendaji kazi fanisi.
Swichi hizi zina sehemu ya kugusa (touch interfaces) zenye vipimo vya joto, hali ya hewa na matumizi ya umeme kwa ajili ya usimamizi wa mwanga, hali joto, mwanga unaoingia ndani, mandhari, ulinzi na muziki. Sasa zinapatikana sokoni Mfululizo huu wa kijanja unakuja katika ukubwa wa boksi la ukutani (junction box) wa aina mbili: Paneli za Titania kwa ajili ya Marekani na paneli za Titan kwa Uingereza.
Mfululizo wa TIS Titan & Titania unabeba swichi zifuatazo:
TITANIA & Titania TFT, hii ni paneli ya kugusa ya ukubwa wa inchi 3 yenye picha za LED unazoweza kuzibadilisha unavyotaka kwa ajili ya kusimamia taa zako, hali ya hewa ya ndani, mandhari, mapazia na zaidi..
TITANIA & Titan 4G ni paneli ya 4-gang ya kugusa yenye uwezo wa kusimamia taa, mandhari, mapazia na zaidi. Unaweza pia kuongeza maandishi yako na picha binafsi. Kumbuka, unaweza kufurahia paneli hizi mpya za ukutani kama wewe ni mkazi wa Italia pia. Kama zikifungwa kwa kulala (horizontally), swichi za Titania 4G zinatosha katika boksi la umeme la kawaida linalotumika Italia.
TITANIA & Titan 3G imebeba paneli ya kugusa ya 3-gang kwa ajili ya kusimamia taa, mandhari, mapazia na zaidi. Mwisho, tunakuletea paneli ya Nesi au Kuita Mhudumu Hotelini (Nurse or Hotel Call Panel). Hii imetengezwa maalumu kwa ajili ya uangalizi; Paneli yetu ya Nesi inarahisisha zaidi mahusiano kati ya mgonjwa na nesi katika vituo vya afya. Mgonjwa anatumia kifaa hiki kuita nesi wake anapokuwa akihitaji msaada. Upande mwingine, kama unamiliki hoteli, tumia paneli yenye MUR/DND kwa ajili ya kuboresha hoteli yako. Swichi hizi mbili zinakaa kwa mlalo (horizontally) katika ukuta na zinang’aa vizuri pembeni ya vifaa vingine ndani ya chumba.
Mkusanyiko huu ni rafiki na rahisi kutumia. Unaweza kutumia vidole katika kioo chake au kama ukitaka ukatumia simu yako ya mkononi kuwezesha mandhari mazuri kwa ajili ya kufanya Yoga jioni, vyote vinaweza kufanyika ndani ya sekunde tu. Maandishi na picha zote ndani yake zinaweza kubadilishwa kuwa vile unavyotaka. Inashangaza si ndiyo?
Paneli hizi zinakuja katika rangi kadhaa na kufunikwa na aina tofauti ya mifuniko itakayoendana na muonekano wa nyumba yako. Tunajali sana juu ya kile unachopendelea na tunakupa mifunoko ya plastiki, chuma, kioo na mingine mingi kwa vile utakavyopendelea.
Mfululizo wa Titan & Titania hauna kikomo kwa sababu tunataka uishi maisha ya kisasa kijanja na bila kuwa na kikomo. Ili kuona namna inavyokuwa ukiishi ndani ya nyumba inayojiendesha, unachotakiwa kufanya ni kufunga Titan au Titania tu.
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Zimetengenezwa Kufaa Muonekano Wako
Kampuni ya TIS Smart Home inakuletea Terre. Kutoka kwenye neno la Kilatini linalomaanisha Dunia, tunayo furaha kukuletea mlolongo wa panel zinazofanya kazi kukurahisishia kila kona ya nyumba yako. Kutokana na jina lake na maana yake, mlolongo huu unapatikana katika ukiwa na muundo wa juu wa kioo, plastiki, mbao, ngozi, jiwe na chuma na unavutia kuangaliwa kutokana na mikunjo na kona zake za kuvutia.
Mlolongo huu wa vifaa vyenye muonekano wa kuvutia unahusisha vifaa 4:
Terre 4Gang Touch Panel: Kileosura(interface) rahisi tu chenye vitufe 4 vya kugusa kwa ajili ya kusimamia taa, mapazia na mazingira. : A simple 4-touch button interface to control lights, curtains, and moods.
Terre AC Control Panel: Kileosura (interface) rahisi tu chenye vitufe 4 kwa ajili ya kubadilisha joto, kasi ya feni, joto katika sakafu au vifaa vingine vya kuleta joto au kupoozea. Taarifa na kumbukumbu zinaonyeshwa katika sktini ya OLED ya inchi 1.
Terre Music Control Panel: Kifaa cha kuchezea muziki cha kugusa na kidole kinachoweza kutumika na TIS Audio Player na kukuonyesha miziki, kumbukumbu na taarifa katika skrini ya inchi 1 ya OLED.
Terre Hotel Panel: Kileosura (interface) rahisi kinachopendwa na wengi na pia kinachoingiliana na soketi za Terre pamoja na swichi zake. Panel hii inaweza kuunganishwa na 4 gang yoyote ili kukaa vyema na muonekano wa chumba cha hoteli yako. Pia wageni wako wanaweza kuomba huduma tofauti, kama vile kufua nguo, baa n.k. kwa kugusa tu picha inayohusika.
Panel hizi za ukutani zinakaa katika boksi za umeme za saizi zote za viwango vya Ulaya/Uingereza na pia zinaweza kuunganishwa kwa pamoja na Panel ya kiyoyozi, au Panel ya muziki kwa kutumia soketi ya USB. Jambo la muhimu ni kwamba hata pale unapozifunga kama panel moja, vifaa hivi ni rafiki na rahisi kutumia, kwa sababu kila kipande kina kazi zake zinazojitegemea.
Chagua tu panel ambayo inakufaa wewe zaidi na kukidhi mahitaji yako. Muda wa kutumia teknolojia nzuri na ya kukunufaisha kwa kutumia mlolongo wa Terre series kutoka TIS.
Coming soon...
Coming soon...
Umaridadi Unapokutana na Teknolojia.
Watu wengi wanatafuta vifaa vya umeme vya kisasa ili kuweza kuangalia nyumba zao vizuri zaidi; hata hivyo, wanakuwa na wakati mgumu kupata kifaa suluhisho ambacho kimetengenezwa kwa ubora na pia kina muonekano mzuri unaoendana na fasheni. Hivyo basi, TIS inakuletea Mars Series ili kukuonyesha namna teknolojia inavyoweza kuwa maridadi.
Mlolongo wetu wa Mars Series Panels una bidhaa za aina 3: Mars 10Gang+ AC, Mars 8Gang, and Mars 4Gang. Panel hizi zenye mkunjo zinaweza kuwekewa programu na kutengeneza mazingira tofauti, kuendesha motors, hali ya hewa na taa na inaweza kufungwa kwenye boksi la umeme (junction box) lolote. Mlolongo huu umetengenezwa katika rangi 7 ili kuweza kukaa vyema katika muonekano wowote wa ndani.
Mars 10Gang+ AC, ni panel yenye vitufe 10 ikiwa na skrini nzuri ya OLED, ukubwa wa inchi 1 na vitufe vya kuvutia. Kifaa hiki kinakuja na thermostat ndani yake; kinaweza kusoma joto la chumba ili uweze kuendesha mfumo wako wa kupooza au kuongeza joto kwa ufasaha zaidi.
Sifa nyingine muhimu katika kifaa hiki ni kioo cha OLED kina uwezo wa kuonyesha ujumbe mfupi uliowekwa kabla. Kwa mfano, kama una kazi nyingi sana na ukasahau kufunga mlango wa kwenye veranda kwa muda, Mars 10Gang+ AC itakujulisha kwa kutumia ujumbe mfupi kwenye kioo chake cha OLED. Pia, kama kuna sehemu maji yanavuja ndani ya nyumba, kifaa hiki kitakuwa ni cha kwanza kujua, na utajulishwa mara moja.
Panel za 8Gang and 4Gang Panels ni vileosura(interfaces) rahisi kutoka katika mlolongo wa Mars Series; zote zimetengenzwa na uwezo wa kupokea IR hivyo zinaweza kuendeshwa kwa kutumia rimoti. Sifa hii ni muhimu sana kwa watu wazee kwa sababu wanaweza kufurahia muunganiko wa teknolojia mpya na ya zamani.
Wazee wetu wanastaili kufurahia muda wao wa kustaafu bila kuwa na mawazo. The Mars 8Gang or 4Gang + rimoti inaweza kuwa ni zawadi ya kipekee kwa wazee wako. Ni rahisi sana kutumia, na utakuwa umerahisisha sana maisha yao.
Kuona tabasamu katika uso wa wazee wako hakika ni stahiki.
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Swichi Mpya kama Dhahabu
Linapokuja suala la kujiendesha kwa nyumba, swichi zenye uwezo wa kufanya kazi mbalimbali zinatakiwa kuwa juu katika orodha ya vitu muhimu, kwa sababu sio tu zinakurahisishia kazi lakini pia zinafanya nyumba yako kuwa salama zaidi. TIS Automation Group imeanzisha toleo jipya la swichi za ukutani zenye uwezo wa kusimamia taa, joto, mandhari, n.k. Moja kati yake ni mfululizo wa swichi za kufungwa ukutani wa IO Series, ambazo zinafaa kufungwa majumbani na katika vyumba vya hotelini.
Mfululizo huu ambao una vitufe vya kubonyeza unakuwezesha kuendesha nyumba yako nzima kirahisi, bila kujalisha upo ofisini, likizo, au kitandani usiku. Tunapendekeza TIS IO series kwa sababu zina muundo mzuri na ni rahisi kutumia na zinaingiliana na taa aina yoyote. Paneli hii inakuwezesha kubadilisha chumba chako kuwa cha kijanja huku pia ikikupa uhuru wa kuwasha kwa njia ya zamani pia kama ukitaka.
Kwa ufupi, kama unatafuta nyumba ambayo mapazia yanajifunga pale mwanga wa jua unapokuwa mkali zaidi, taa zinajizima unapotoka chumbani, na Kiyoyozi kinasafisha hewa hali inapokuwa sio nzuri nje, unatakiwa kuchagua swichi za TIS IO.
Sasa tuangalie ni nini kinachokuja pamoja na kifurushi hiki janja:
IO Thermostat with 4 Gang: Hii ni thermostat ya ukutani yenye skrini ya OLED na kitufe cha kuzungusha kwa ajili ya kubadilisha joto la chuba, spidi ya feni, na kuongeza joto katika sakafu. Inakuwezesha kusimamia taa, mandhari, na vifunika madirisha kwa kupitia vitufe vya kubonyeza vinne.
IO 8G: Kifaa hiki kinaweza kufungwa kwa mlalo au wima katika hoteli au mradi wowote wa makazi kwa ajili ya kutoa usimamizi kamili juu ya taa, mandhari, hali ya hewa n.k.
IO Outdoor Hotel Panel: Unaweza kuongeza ubora katika vyumba vya hoteli yako kwa kutumia kifaa hiki suluhishi, kilicho na vitufe vya kuita usafi wa chumba au kutokusumbuliwa (WUR/DND) na kioo kinachoonyesha namba ya chumba. Kama ukiiwekea programu husika, wateja wanaweza kutumia RF readers na access control functions, pia.
IO Card switch: Kama unataka kuwafurahisha wageni wako, wawekee wafurahie paneli inayovutia na rafiki kutumia. Swichi hii ya hotelini iliyowezeshwa kutumia kadi za RF inakuja na vitufe vitatu kwa ajili ya Kutosumbuliwa, Kuita usafi wa chumba na kuita huduma za ufuaji (DND/MUR/Laudry services) na inahifadhi ya kumbukumbu kwa ajili ya kutunza kumbukumbu za mtu/chumba (user/room service logs). Hivyo, inaboresha usimamizi wa hoteli bila kumsumbua mteja. Kwa ubunifu wa TIS, kila mtu anapata anachokihitaji ndani ya muda mfupi.
Manufaa yanayopatikana katika vifaa vyote katika mfululizo wa IO series ni pamoja na kuongezeka kwa usalama na kuboreshwa kwa BMS. Pia bidhaa hizi zinakuokolea pesa, na sio hayo tu. Zimetengenezwa pia ili kukuwezesha kupata muonekano bora kabisa ndani kwako. Zina mikunjo ya kupendeza na kuvutia, mfululizo huu wa paneli za ukutani una muonekano wa kipekee. Unaweza kuchagua kadri unavyopendelea.
Tunafurahia kukusaidia kupata kile unachokitaka.
Wateja Ambao Huwa Hawaondoki
Uadilifu unahitaji kuwa mkweli katika kutoa huduma bora kwa wateja. Wafanye wateja wako wajisikie nyumbani pale wanapokuwa hotelini kwako. TIS inakuletea Luna Hotel Panels, iliyotengenezwa kwa muonekano unaoendana na fasheni na kukuletea ubora katika vyumba vya wageni katika hoteli yako.
Mlolongo huu wa panel (panel series), ukiwa na vileosura (interfaces) bora, una vifaa vikuu 3:
Hotel Outdoor Bell: Toleo la kwanza la panel hii lina kitufe cha kengele pamoja na viashiria(indicators) 3 vya huduma (Kufua, Kusafisha Chumba, na Mpangilio wa Usisumbue Muda huu) au (Laundry, Make Up Room, and Do Not Disturb (DND) mode) na kiashiria cha namba ya chumba. Kama nyongeza kwenye kitufe chake cha kengele na viashiria 3, toleo la pili la panel hii lina RF, ambayo inakuwa inakupa uwezo wa kuiendesha. Inafungua na kufunga milango kwa kutumia kadi za wageni na inakuondolea hofu ya kubadilisha betri kila mala milangoni kwako.
Una uwezo wa kuchagua vitu tofauti katika kifaa kimoja.
Wageni wanaweza kupiga kengele za chumbani kwa kugusa tu katika picha ya kengele kwenye panel yao. Lakini, kama mteja amepumzika na mpangilio wa “Do Not Distrub” upo umewashwa, ujumbe mfupi utaonyeshwa katika panel, na kengele itazuiwa, na usumbufu wowote utazuiwa. Je, unafikiri wageni wako watapendelea uwezo huu kwa kutumia vifaa vya kisasa?
Hotel Card/Services Panel: Swichi hii ya kadi katika panel ina sehemu ya kubebea kadi na vitufe vitatu vya Laundry, Make Up Room, na DND. Panel hii ni ya kipekee kwa sababu ya uwezo wake wa kufanya kazi na kadi ya Mifare; pale kadi inapowekwa katika kibebea kadi chake, umeme katika chumba unawezeshwa (kasoro katika friji, ambapo umeme unakuwepo muda wote). Pia, inaweza kuwekewa programu ili kuwa na taa nyingi kadri utakavyohitaji kuziwasha. Sifa hii inakusaidia kuokoa kiasi kikubwa cha umeme kwa sababu hakuna kifaa kilichosahaulika kuzimwa kitabaki kinawaka wakati mteja akishaondoka chumbani. Sababu ni kwamba, pale kadi itakapochukuliwa vifaa vilivyowekewa programu vitajizima moja kwa moja.
Hata hivyo, unaweza kuwekea programu kifaa hiki kufanya kazi na kiyoyozi kulingana na hali ya hewa ya eneo hilo. Kwa mfano, kama hoteli ipo maeneo ya joto, unaweza kuielekeza panel iwashe kiyoyozi na kukiweka katika hali fulani ya joto na kubadilisha tu mipangilio ya taa.
(Kwa ambae atahitaji kujua: Kadi za Mifare zinaweza kubadilishwa na kwa namna unayopendelea; kama wageni wako ni wapenzi ambao wanakaa kila mmoja peke yake, unaweza kuwapa kadi mbili. Hizi kadi zinaweza kutumika kila moja badala ya nyingine. Pia, kwa sababu zinaweza kubadilishwa kwa namna yoyote ile kulingana na kazi ya wafanyakazi wa hotelini, zinakuwa na ulinzi mkubwa. Kwa mfano, kama mfanyakazi wa kusafisha anafanya kazi katika siku fulani za wiki, kadi yake inaweza kuwekwa isifanye kazi katika siku zingine asizokuwepo n.k
Hii ina thamani kubwa sana kwa kila serikali ambayo ina ndoto ya kuwa na uchumi unaokuwa kwa kuwa na matumizi mazuri ya umeme. Kuwa sehemu ya ndoto hii!
Kengele zetu za hotelini za ukutani na Panel za Kadi za Hotelini zinafungwa ndani nan je ya kila chumba. Zaidi ya hayo, zinaweza kuunganishwa na menejimenti ya hoteli na kuonyesha maombi ya wageni kwenda kwenye hoteli, hivyo kufanya wageni kukaa kwa amani na kwa faragha na pia maisha ya waangalizi wa hoteli yanakuwa nirahisi zaidi.
Ukiwa na Luna Hotel Panel wageni wako wanaweza kufurahia kukaa kwao katika hoteli yako yenye teknolojia kubwa. Fanya hoteli yako ing’ae na kupendeza kama mwanga wa mwezi.
Zimetengenezwa Kufaa Muonekano Wako
Kampuni ya TIS Smart Home inakuletea Terre. Kutoka kwenye neno la Kilatini linalomaanisha Dunia, tunayo furaha kukuletea mlolongo wa panel zinazofanya kazi kukurahisishia kila kona ya nyumba yako. Kutokana na jina lake na maana yake, mlolongo huu unapatikana katika ukiwa na muundo wa juu wa kioo, plastiki, mbao, ngozi, jiwe na chuma na unavutia kuangaliwa kutokana na mikunjo na kona zake za kuvutia.
Mlolongo huu wa vifaa vyenye muonekano wa kuvutia unahusisha vifaa 4:
Terre 4Gang Touch Panel: Kileosura(interface) rahisi tu chenye vitufe 4 vya kugusa kwa ajili ya kusimamia taa, mapazia na mazingira. : A simple 4-touch button interface to control lights, curtains, and moods.
Terre AC Control Panel: Kileosura (interface) rahisi tu chenye vitufe 4 kwa ajili ya kubadilisha joto, kasi ya feni, joto katika sakafu au vifaa vingine vya kuleta joto au kupoozea. Taarifa na kumbukumbu zinaonyeshwa katika sktini ya OLED ya inchi 1.
Terre Music Control Panel: Kifaa cha kuchezea muziki cha kugusa na kidole kinachoweza kutumika na TIS Audio Player na kukuonyesha miziki, kumbukumbu na taarifa katika skrini ya inchi 1 ya OLED.
Terre Hotel Panel: Kileosura (interface) rahisi kinachopendwa na wengi na pia kinachoingiliana na soketi za Terre pamoja na swichi zake. Panel hii inaweza kuunganishwa na 4 gang yoyote ili kukaa vyema na muonekano wa chumba cha hoteli yako. Pia wageni wako wanaweza kuomba huduma tofauti, kama vile kufua nguo, baa n.k. kwa kugusa tu picha inayohusika.
Panel hizi za ukutani zinakaa katika boksi za umeme za saizi zote za viwango vya Ulaya/Uingereza na pia zinaweza kuunganishwa kwa pamoja na Panel ya kiyoyozi, au Panel ya muziki kwa kutumia soketi ya USB. Jambo la muhimu ni kwamba hata pale unapozifunga kama panel moja, vifaa hivi ni rafiki na rahisi kutumia, kwa sababu kila kipande kina kazi zake zinazojitegemea.
Chagua tu panel ambayo inakufaa wewe zaidi na kukidhi mahitaji yako. Muda wa kutumia teknolojia nzuri na ya kukunufaisha kwa kutumia mlolongo wa Terre series kutoka TIS.
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Coming soon...
Inakuja hivi karibuni…
Hebu Tung’arishe Maisha Yetu.
Mwanga una nafasi ya muhimu sana katika kumbukumbu zetu. Unaweza kubadilisha hisia zetu ndani ya sekunde. Mwanga pia ni wa muhimu katika muonekano wa ndani ya nyumba yako. Na hiyo ndio sababu aina tofauti za taa zimekuwa zikitengenezwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Katika soko lenye ushindani mkubwa la vifaa vya uangalizi wa ndani, kampuni ya TIS inayofuraha kukuletea bidhaa zetu bora za Leading Edge Dimmer modules, ambazo zinakusaidia kwa urahisi kutengeneza mazingira mazuri katika hali yoyote na kuwa na kiwango cha mwanga unachokitaka.
Tumia taa za kuwaka zenyewe ndani ya nyumba yako kwa kutumia LE Dimmers: 2DG(channel)/6A module, 4CH/3A module, na 6CH/2A module. Vifaa hivi vya kupunguzia mwanga vinafanya kazi pamoja na teknolojia ya TRIAC na vinaweza kutumika kupunguza mwanga wa taa za balbu pamoja na taa za halogeni.
Kutengeneza mazingira ni rahisi sana kwa kutumia LE Dimmers. Hebu fikiria taa za kwenye ukumbi wa harusi zikipunguzwa mwanga wakati wadada wanaomsindikiza bibi harusi wanapokuwa wakiingia na muziki wa kipekee na kuandaa bibi harusi kuingia. LE Dimmers zinaweza kufanya muda usiwe wa kusahaulika.
Kama ikiunganishwa pamoja na kihisio mwendo cha TIS (TIS Motion Detector Sensor) LE Dimmers zinaweza kupunguza mwanga zenyewe au kuongeza mwanga zenyewe tu kwa kuangalia kama kuna mtu ndani ya chumba. Hii inaepusha upotevu wa umeme. Pia, matumizi ya LE Dimmeri hayaishii kwenye taa tu pekee; kwa sababu bidhaa hii suluhisho inafanya kazi katika mfumo ywa TIS-BUS, inaweza pia kuungwa na module nyingine ili kupunguza mwanga wat aa nyingi zaidi kadri unavyotaka kwa pamoja.
Na zaidi, uwezo wa bidhaa hii hauishii hapo tu kwenye taa. Feni ya juu pia inaweza kuendeshwa na LE Dimmers. Na kwa sababu ina ulinzi wa fuse bora ndani yake, vifaa vyako vya umeme vitabaki kuwa salama kabisa inapotokea umeme kuzidi/shoti ya aina yoyote.
Kifurushi hiki pia kinakuwa kimewekewa kitufe cha pembeni ili kukupa uwezo wa kuendesha mwenyewe kifaa chako inapotokea kuna hali ya dharura.
LE Dimmer zipo hapa kukusaidia kutengeneza mazingira yatakayokumbukwa, furaha katika sherehe, au hali yoyote katika maisha ambapo mwanga unaweza kubadilisha namna unavyojisikia.
Mahitaji Huchochea Ugunduzi
Teknolojia inaendelea kwa kasi sana, kama vile dunia inavyokimbia. Mahitaji mapya yanazaliwa na majibu mapya yanahitajika. Hili ni la ukweli pia inapokuja suala la taa; aina za taa zimebadilika kwa kati, na zinahitaji suluhisho la kisasa kuendelea kuziendesha. Teknolojia ya zamani ya TRIAC sasa imepitwa na wakati, kwa sababu haiwezi kutumika na LED, CFL na taa zingine za kuokoa umeme. Tukiwa na malengo ya kutatua tatizo hili, Kampuni ya TIS Smart Home inakuletea Trailing Edge (TE) Dimmer—suluhisho la kisasa la kupunguza mwanga wat aa za aina zote.
Swichi hii ya kupunguzia mwanga, inayopatikana katika model mbili, inaweza pia kufanya kazi na taa za umeme mkubwa (110/230A). TE Dimmers za 2ch/3A na 4ch/1.5A ni suluhisho bora katika mradi wako wa nyumbani/wa kibiashara.
Kidaa hiki kimetengenezwa kwa namna kinabakia kikiwa imara hata wakati shoti inapotokea. Muundo wake wa ulinzi unakizima pale kunapokuwa na umeme mkubwa kupita kiasi.
Sifa nyingine muhimu ya hii TE Dimmer ni vitufe vya pande mbili vilivyopo katika module. Vitufe hivi vinaweza kutumika kujaribisha pamoja na KUWASHA/KUZIMA pale kunapokuwa na hali ya dharura.
Agana na hali ya taa kuwa inawaka na kuzima zim; TE Dimmers zinapunguza mwanga kiulaini na safi kabisa. Pale zitakapofungwa, unaweza kuziunga na mfumo wa TIS-BUS na ukafurahia utendaji kazi wake na vifaa vingine bila kuhitaji uangalizi. Je, unamiliki mgahawa? Tengeneza idadi ya mazingira uyapendayo kwa kugusa tu. Ongeza mazingira ya kifahari katika mgahawa wako, huku ukiwapa wateja wako chakula watakachokikumbuka.
Wataalamu wa TIS wanatumia ujuzi wao na uadilifu wao kutengeneza suluhisho la kisasa leo ili kukidhi mahitaji yote duniani kote. TE Dimmers zipo hapa kukusaidia kutengeneza mazingira mazuri katika maeneo ya biashara nay a makazi pia.
TIS Technology ni Ramani Yako Katika Wimbi la Taa Zilizopo.
TIS imetengeneza vifaa suluhishi vingi ili kurahisisha maisha ya wateja wao. Baadhi ya vifaa hivi ni vizuri kwa ajili ya kufanya nyumba yako kuwa ya kisasa, na vingine, vikiwa na uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja, vina uwezo wa kujisimamia (automate) katika mradi wa aina yoyote. TIS 6-Channel Ballast Controller ni moja ya suluhisho ambalo lina manufaa katika mazingira ya makazi na ya kibiashara pia.
Bidhaa yetu hii ya 6CH Ballast Driver inakusaidia kusimamia taa zote zinazotumia umeme kati ya 0-10V. Kwa kutumia bidhaa hii, unaweza kwa urahisi kupunguza mwanga wa taa dukani kwako na kutengeneza mandhari mazuri ya kuvutia wateja. Ifunge tu na upunguze na kuongeza mwanga katika duka lako kadri utakavyopenda.
Fikiria namna fremu za picha katika kuta za nyumba yako zitakavyopendeza zikifungwa na taa za LED zinazong’aa. Ukuta unaong’aa wenye picha za wapendwa wako zilizozungukwa na taa za kupendeza zinazoweza kupunguzwa mwanga zitakufanya usogee karibu kuzitazama kila siku, hata unapokuwa mbali. Hiyo ndiyo kazi ya kifaa hiki cha ballast driver.
Tupo hapa kwa ajili ya kukusaidia kusimamia taa zako kwa kutumia app moja tu ndani ya simu yako bila kirahisi na bila usumbufu. Turuhusu tukupeleke katika hatua ya mbele katika ulimwengu wa taa za kijanja kwa kutumia 6-Ch Ballast controller yetu.
Furahia Teknolojia Bora ya Kuwashia Taa
Sote tunafurahia teknolojia, lakini mara nyingine inakuwa ni vigumu kufunga na pia kuvitumia baadhi ya vifaa vya kidigitali. Ndiyo maana ni muhimu sana kutafuta kifaa ambacho sio tu kinafanya kazi, lakini pia ni rafiki rahisi kutumia pia. Watengenezaji wa TIS wanatengeneza bidhaa ambazo ni suluhisho la kisasa n ani rahisi sana kutumia. Itifaki yetu ya DALI Protocol ni moja ya vitu tulivyotengeneza.
Digital Addressable Lighting Interface ni mfumo unaoruhusu kuwasha na kuzima taa tofauti.
Unaongoza katika mifumo ya kujisimamia yenyewe pamoja na mifumo ya mitandao, ni rafiki na rahisi kutumia, DALI 64 inawezesha kuangalia ta azote (ikiwemo za florescent, LED na zaidi), ballasts, na drivers. Kileosura (interface) hiki inauwezo wa kubeba channel 64, na kama zikiungwa kwa pamoja katika duara kwa kutumia mfumo wa TIS BUS, kundi la channel za DALI 64 unaweza kuwasha uwanja wa mpira.
TIS DALI protocol ni muhimu katika hali ambayo usimamizi wa taa pamoja na ulinzi ni vitu vya kutazama kwa umakini. Sehemu kama maeneo ya umma, ya biashara na/au sehemu za makutano, kama vile malls na makumbusho. Kama kukitokea nyaya zikakatika, umeme umekatika au taa zikikosa umeme kwa sababu yoyote ile, itifaki hii inauwezo wa kuziwasha kwa dharura. Hii inakupa muda wa kupiga simu na kuita fundi. Pia, kama kukitokea umeme umekatika, itifaki hii ya kisasa itarudisha mipangilio iliyopita.
Mfumo wa DALI pia unapunguza idadi ya nyaya zinazotumika kwa kiwango cha mpaka 80%. Kama ukifungwa pembeni ya taa, hakuna haja ya kufunga nyaya tofauti kwa ta azote kwenda kwenye chumba cha usimamizi kwa sababu mfumo huu unatumia mbinu ya kuzunguka (looping method). Na hivyo ndivyo DALI inavyoweza kufanya yasiyowezekana yawezekane.
Itifaki ya DALI pia inawezesha makampuni yaliyoshirikishwa (incorporated group) na vyumba vya kurusha matangazo. Kwa mfano katika sinema ambapo kuna makundi tofauti ya taa (nyekundu na nyeupe kwa mfano) katika maeneo tofauti (mbele, nyuma na pembeni). Mifumo ya zamani ya kuwashia taa haifai katika jengo kama hili kwa sababu nyaya pamoja na swichi zinazohitajika kufungo mifumo hii inaweza kuwa hatari! Ukitumia DALI, unaweza kuingiza mipangilio ambayo itafanya kundi fulani la taa ziweze kuendeshwa kwa muda mmoja bila kuwa na uhitaji wa kuwa umefunga nyaya na swichi nyingi.
Mfumo wa DALI kutoka TIS ni msimamizi wat aa (light controller) unaofanya kazi na unafanya usimamizi wa taa katika majengo na maeneo makubwa kuwa rahisi sana. Itifaki hii ni msaidizi mzuri sana katika kupangilia muonekano wa ndani kwako, kutazama na pia kusimamia mfumo wako wa ulinzi, na kukuepusha na ufungaji wa nyaya nyingi sana.
“Wacha Mwanga Ubadilishe Ulimwengu Yako”
Je, wewe ni mdau wa sherehe? Je, unafurahia taa za kwenye kumbi za kuchezea? Je, unataka kubadilisha nyumba yako na kuwa kama ukumbi wa kuchezea muziki? Basi, tunacho kile unachokitafuta. TIS DMX controller itaongeza uzuri wa sherehe yako zaidi ya hata utakavyoweza kufikiria.
Controller hii sio tu kwamba inaweza kupunguza ukali wa mwanga pamoja na kuzima na kuwasha taa; inaweza pia kutengeneza mwanga wa rangi mbalimbali pamoja na mbwembwe. Nyongeza, inaweza pia kuendesha vifaa vyote ambavyo vinatumia itifaki ya DMX512 (DMX512 protocol). Baada ya kuifunga na kuiunganisha na mfumo wa TIS-BUS System, nyumba yako haitakuwa na tofauti na steji kubwa. Utaweza kuendesha taa zote kwa namna unavyoona inapendeza katika sherehe iliyopo. Je, ni kumbukumbu ya tukio? Basi fanya sherehe ndogo itakayokumbukwa na kila mtu yenye vitu vidogo vya tofauti. Ifanye controller itengeneze mwanga mwekundu huku nyimbo ya mapenzi ikicheza, au mkaribishe mpenzi wako kucheza kati na wewe.
Habari nzuri ni kwamba TIS DMX Controller inaweza kutumiwa pamoja na aina nyingi za taa za WRGB. Haijalishi kama unasherekea kabla ya kufunga ndoa, unataka kubadilisha rangi ya mwanga wa ndai kwako katika muda Fulani, au mtoto wake wa kiume anataka tu kucheza nyumbani na marafiki zake, mambo unayoweza kuyafanya ni mengi bila kikomo. Unaweza kuwa DJ wako mwenyewe; weka hisia unazotaka, mbwembwe, na mwanga wa laser kwa kutumia DMX Controller.
Kutumia kifaa hiki ni rahisi sana. Simu yako ya mkononi ni keyboard yako. Unaweza kuendesha/kupunguza mwanga wat aa zote kwa kutumia vidole vyako tu. TIS DMX Controller inaweza kutumika badala ya DJ DMX Console kiurahisi kabisa. Urahisi kutumia ndiyo jambo linaloletwa nah ii controller.
DMX48 ni model ya controller inayobeba channel 48, kwa sababu kifaa hichi kinafanya kazi katika mfumo wa TIS-BUS kinafaa katika matamasha makubwa, kumbi za kuonyeshea mitindo, migahawa mikubwa na zaidi.
Ukiwa na DMX Controller unaweza kushirikisha hisia zako na nyumba yako.
Ifunge, kisha uruhusu mwanga uwake.
Mwanga Ambao Kamwe Hauzimiki.
Kusimamia taa zilizopo katika miradi mikubwa na majengo makubwa sio jambo rahisi. Kutokana na uwepo wa taa zinazotumia umeme wa viwango tofauti, ni muhimu kuwa na teknolojia ya kuaminika. Kifaa kipya maalumu kwa kazi hii Industrial Dimmer kutoka TIS kitakusaidia kusimamia taa za kawaida na za LED.
Swichi hii ya kupunguza na kuongeza mwanga inamuwezesha mtumiaji kuweka kiasi cha mwanga katika taa anachokitaka kwa matumizi fanisi ya umeme. Haijalishi una chaneli ngapi za taa katika mradi wako, tunaweza kukusaidia kusimamia na kuweka kiwango cha mwanga unaoutaka katika chumba chochote.
Industrial Dimmer zetu zinakupa uwezo mkubwa wa kuongeza na kupunguza mwanga kwa kiwango unachokitaka katika eneo lako. Kama unamiliki casino, basi unafahamu umuhimu wa kutengeneza mazingira na muonekano sahihi ili kupata mafanikio katika biashara. Unaweza hata kuwa na taa zinazowaka na kuzima zikiendana na muziki ili kufanya wateja wako wajisikie vizuri kila wakati. Ukiwa na TIS, ni rahisi kufanya casino yako ing’are.
Moduli hii inafanya kazi na taa za balbu pamoja na zile za LED na inakuwezesha kubadilisha kiwango cha mwanga katika taa zaidi ya moja moja kwa moja kutoka katika simu yako ya mkononi au kompyuta. Wamiliki wa hoteli wanaweza kufaidi urahisi na ufanisi wa kifaa hiki, kinachofanya usimamizi wa hoteli kuwa rahisi na rafiki kwa mazingira. Haijalishi kama unataka kusimamia taa zako ukiwa katika chumba kingine au ukiwa upande mwingine wa sayari, tunapendekeza utumie kifaa cha TIS Industrial Dimmer.
Ukiwa na moduli yetu ya kupunguza na kuongeza mwanga, unakuwa na uhakika kwamba una bidhaa ambayo imethibitishwa, rahisi kutumia, na ya kudumu. Hautapoteza muda wako kutafuta swichi za taa ili uweze kutengeneza mandhari mazuri ndani ya mgahawa wako. Ndiyo, ni sahihi; dimmer hii inaweza kutumika katika migahawa pia. Teknolojia nyuma ya bidhaa hii inaiwezesha kukaa vizuri katika eneo lolote la kibiashara.
Tunapenda teknolojia hii, na tunaamini utaipenda pia.
Fanya Nyumba Yako Kuwa ya Kuaminika.
Ni muhimu kupata kitu bora kwa hela utakayotoa, haswa inapokuja katika vifaa vya umeme ambavyo vinaweza kuathiri maisha yako kwa kiasi kikubwa pale vinaposhindwa kufanya kazi yake vizuri. Uvumbuzi mpya wa TIS unalenga kutatua tatizo hili moja kwa moja kwa kutumia vifaa vyake vilivyotengenezwa kiutaalamu vitakavyokidhi mahitaji ya nyumbani kwako yote. Mlolongo wetu wa Relay Series unakupatia kila kitu utakachokihitaji ili kukamilisha nyumba yako janja. Simamia thermostat, taa, FCU na zaidi kwa namna ambayo itakuwa ikipendeza ndani.
Mlolongo wetu wa Relay Series, ambao unategemea na idadi ya channel na unapatikana katika aina nne tofauti (channel relays 4, 6, 8 na 12), ni sehemu ya mfumo wowote wa kujisimamia na inatumika KUWASHA/KUZIMA au KUFUNGUA/KUZIMA sehemu mbali mbali za nyumbani kwako. Kwa mfano, kutegemea na mahitaji yako, mlolongo huu unaweza kusimamia taa zako, vimwagilia maji, motor za geti, mapazia, shutters, kasi ya feni, vifaa vya kuweka joto kwenye sakafu, valvu za maji/gesi, ving’ora, flashers na zaidi.
Japokuwa vifaa janja vingi vimetengenezwa maalumu kwa ajili ya kufanya kazi moja tu, kuna vichache ambavyo vina uwezo wa kufanya kazi nyingi. TIS Relay Series ni moja kati ya hivyo vichache, inakupa huduma bora ya hali ya juu bila uhitaji wa kuunganisha na kifaa kingine chochote. Hata hivyo, kama ukipendelea kuunganisha module kadhaa kwa pamoja, hiyo ni rahisi kufanya pia, kwa sababu kila relay ina kiunganishi pembeni cha BUS, na hivyo kuondoa uhitaji wa nyaya za ziada.
Mlolongo huu umetengenezwa kufanya kazi kwa mpangilio wa voltage huru, kinachomaanisha ya kwamba, kwa mfano, haijalishi kiasi chochote cha voltage kinachohitajika kuwasha kiyoyozi, relay itawasha injini.
Kama ikiungwa na mfumo wa TIS-BUS, kasi ya relay kufanya inaongezeka. Hii inakuhakikishia ya kwamba amri nyingi zinaweza kufanyiwa kazi kwa kila sekundi. Kwa mfano, fikiria kama unataka kuzima kifaa cha kuchezea muziki, kuwasha TV na pia kuwasha jagi la kutengenezea kahawa pia kuongeza joto la chumbani ukiwa unajiandaa kutazama filamu yako unayoipedelea. Mfumo wetu unaweza kufanyia kazi amri zote hizi kwa wakati mmoja.
Vifaa hivi pia vina saa nani yake hivyo vinakuwezesha kuwa huru kuweka vitendo fulani vifanyike katika muda fulani. Je, unahitaji maji yamwagiliwe nje kwenye majani unapokuwa ukirudi jioni? Weka maelezo hayo. Fanya bustani yako ipendeze zaidi hata pale unapokuwa haupo.
Mita ya umeme iliyotengenezewa ndani ya kifaa hiki ni sifa nyingine pia. Inarekodi na kuripoti matumizi yako ya umeme ya kila siku, mwezi na mwaka, na kukusaidia kutotumia zaidi ya unavohitaji.
Pale utakapomaliza kuweka maelezo kwenye relays kutumika na vifaa vya umeme vya ndani, unaweza kuviendesha muda wowote na kutoka mahali popote. Ili kuweza kuwapa wateja wetu urahisi mkubwa, tumeamua kutengeneza programu ya simu ambayo unaweza kuitumia kusimamia nyumba yako bila ya wewe kuwepo. Kwa mfano, unaweza kutumia simu yako ya mkononi kufungua geti la mbele pale unapokaribia kuingia ndani au kufunga mapazia pale upepo unapokuwa mkali.
Haya sio yote. Relays zinauwezo wa kukuruhusu kuweka maelekezo na kuzitumia wewe moja kwa moja. Kuna vitufe vya kubonyeza inapotokea kuna hali ya dharura na unahitaji kuwasha taa, hivyo nyumba yako haitabaki kweny giza.
Nyumba yako sasa sio tu kitu rahisi, jengo tu kubwa linalotuhifadhi. Ukiwa na bidhaa za TIS smart solutions, nyumba yako sasa inakuwa na uhai, kama tulivyo sisi.
Teknolojia ya Kisasa Kwa Starehe ya Juu
Kampuni ya TIS inamalengo ya kutengeneza bidhaa ambazo ni suluhisho na zitatatua mahitaji ya mteja zaidi ya alivyotegemea. HVAC Module ni moja kati ya bidhaa hizo, inafanya kazi nyingi sana kwa ubora wa hali ya juu kukupatia starehe mahali popote ulipo. Ni suluhisho la kisasa la kuendeshea mfumo wa duct split system wa HVAC, VAV 0-10V dampers, pamoja na air handling units (AHU).
Module hii ina relay 6 kwa ajili ya kuangalia spidi tofauti za feni (ndogo, kati, kubwa), kupooza, kuongeza joto na pia auxiliary contact. Kumbuka ya kwamba auxiliary contact zinaweza kuunganishwa na dehumidifier pamoja na/au pampu za kupooza/kuongeza joto. Hivi vifaa vya ngazi ya juu ya kuwasha vinaweza kufanya hatua ya pili ya kupooza/kuongeza joto. Kwa mfano, kiyoyozi cha hatua mbili kinatoa ngazi mbili: ya juu na ya chini. Inawaka kwa nguvu zote pale utakapohitaji ifanye hivyo na kwa kiwango cha chini kabisa pale unapokuwa hautaki. (module ya HVAC inafanya kiyoyozi kifanye kazi kwa uwezo wa juu kabisa wakati wa kipindi cha kiangazi na spidi za chini katika siku za baridi).
Module ya HVAC imefungwa na kihisio cha joto kilicho nje kinachoisaidia pale inapokuwa inafanya kazi na thermostats ya ukutani kama vile Luna panel. Inaweza kufanya kazi kama vile kikotoo cha kujitegemea cha joto la chumba pia (inaonyesha wastani wa joto ambalo lipo kwenye chumba). Hii inamaanisha ya kwamba Module ya HVAC iliyofungwa katika chumba chako cha kulala inaweza kuunganishwa na Luna panel ambayo ipo katika sebule. Na matokeo yake, vyumba vyote vinapata joto katika usawa mmoja, na hakuna hata mmoja ambaye atapata joto kali kuzidi.
Sifa hii inafanya Module yay a HVAC kuwa inafaa sana kwa matumizi ya kila siku katika miradi ya kibiashara, kama vile malls na migahawa. Hakuna haya ya thermostats za ukutani kwenye maeneo haya.
Module hii janja pia inatunza kumbukumbu za matumizi yake ya umeme ambayo inakuwezesha kuona muda (kwa masaa) ya ubora wa utendaji kazi wa bidhaa.
Pia ina uwezo wa kuweka ratiba, ambayo inakuwezesha kuweka matendo maalumu yanayofanyika kwa muda Fulani. Kwa mfano, unaweza kuweka maelekezo katika module ya HVAC ili iondoe ukungu ndani ya nyumba yako pale kunapokuwa na ukungu mwingi. Kama nyongeza, kwa sababu module hii inaweza kufungwa na kufanya kazi na TIS-Bus Protocol, hakuna kikomo cha vitu unavyoweza kuviendesha. Kwa mfano, unaweza kuweka mipangilio ya kwamba mfumo wa AC kwenye chumba chako cha kifahari cha spa ifanye kazi kulingana na joto ambalo unalipendelea zaidi.
Pia unaweza kutumia vitufe vyake vya pande mbili kwa ajili ya kujaribishia na pia kuchukua uwezo wa kuiendesha wakati wa dharura.
Module yetu ya HVAC ipo hapa kwa ajili ya kukufanya ufurahie vumbuzi zetu za kisasa katika ulimwengu wa kisasa wa kidigitali.
Usikubali Tu. Tengeneza Zaidi.
Muonekano wa kisasa wa ndani ya nyumba unabadilika kadri mitindo mipya inavyozid kuibuka, na mara nyingi kuendana na kasi hii ya mabadiliko huwa ni changamoto kutokana na vikwazo vilivyopo katika vifaa vya ujenzi na mifumo ya ufungaji nyaya ya sasa. Moja ya vipaumbele vyetu ni kuwawezesha watumiaji kushinda vikwazo hivyo, na tunajaribu kutengeneza bidhaa ambazo zinaweza kuendana na mazingira mbalimbali ili kuweza kukaa katika nyumba yako janja muda wowote utakapohitaji.
TIS ADS 3 Relay Module ni kifaa kidogo kinachotoa suluhisho chenye kazi nyingi. Kinasaidia kuongeza uchaguzi zaidi wa taa zako katika nyumba yako janja, tukimaanisha kwamba kama unahitaji kuongeza mng’ao katika sebule yako au kutengeneza muonekano fulani katika taa ndogo(mini bar) mpya katika kona ya chumba, basi unahitaji suluhisho hili.
Uwashaji wa taa katika bustani, maktaba, jikoni na maeneo mengine kama hayo unafanywa kuwa wa kisasa kwa kutumia ADS 3 Relay Module yetu. Hata hivyo, suluhisho hili linaweza kufanya kazi nyingi zaidi ya hiyo tu. Kama ikifungwa pembeni ya mota ya pazia, kifaa hiki cha TIS ADS kinaweza kukupa uwezo wa kuendesha vifunika madirisha(shade, shutter) pamoja na pazia lenyewe. Unaweza kuongeza uwezo wa kufunika dirisha lako na kuepusha samani zako za ndani kuharibika.
Pia moduli hii inafanya kazi na mtandao wa BUS network. Kwa hiyo, hata kama nyumba yako ilijengwa miaka mingi nyuma, bado inawezekana kuifunga na kufurahia uwezo wake wote. Ukiwa na moduli TIS ya ADS 3 Relay Module, unaweza kubadilisha muonekano wa nyumba yako kwa namna unavyopendelea wewe bila ya kuathiri ubora na muonekano unaoutaka.
Tunakusaidia kukurahisishia mambo zaidi. Ni mawazo yetu madogo tu yanayoleta mabadiliko makubwa.
Imetengenezwa. Inafanya Kazi Nyingi. Rahisi.
Katika kusimamia miradi mikubwa—iwe ni ya kibiashara au ya kimakazi—kutengeneza na kusimamia ni muhimu sana kwa sababu tunafurahia kutengeneza vitu ambavyo vinafanana na namna tulivyo na kwa sababu kusimamia miradi mikubwa kunahitaji juhudi kubwa sana. Huku kukiwepo na vitu vingi sana vya hali ya juu pamoja na vifaa vya umeme vingi, kutengeneza mradi kama vile maduka makubwa, migahawa, mahoteli na majengo mengine makubwa ya kibiashara ni rahisi sana sasa ukilinganisha na ilivyokuwa siku za nyuma. Lakini, matatizo ya kiuchumi, ubora, uimara na dhamana ni lazima viangaliwe kwa umakini. Hivi ndivyo vitu ambavyo watengenezaji wa TIS wameviwekea umakini wanapokuwa wakivitengeneza kifaa kipya cha kidigitali. Module yatu ya Room Control Unit ni mfano mmoja wapo wa kifaa kimoja wapo kilichotengenezwa ili kukidhi mahitaji mengi.
RCU Modules zinapatikana katika model tofauti, zikiwemo RCU-20R-20Z-IP, RCU-24R-20Z na RCU8in-8out.
The RCU-20R-20Z-IP ina channel input 20 na output; hivyo, ina uwezo wa kuendesha karibia kila kitu katika mradi wa vifaa vya kujiendesha vyenyewe. Kifaa hiki kinafananishwa na vihisio vyote vya mwanga, FCU, mapazia, shutters na motors vinavyopatikana katika soko. Kifaa hiki kinaweza kusimamia eneo kubwa, kufanya kazi zote huku kikiendelea kuangalia na kupunguza matumizi ya umeme.
The RCU-20R-20Z-IP ni bora zaidi na ni suluhisho linalofaa kwa hoteli. Kifaa hiki kinaweza kuboresha hoteli yako; unganisha swichi za kawaida za ukutani na kifaa hiki na uzifanye ziwe janja.
Bidhaa hii pia imefungwa na IP port, inayowezesha sehemu tofauti za jengo kuweza kuunganishwa na kuendeshwa kwa kutumia jukwaa moja. Kwa mfano, ndani ya hoteli, vyumba vyote vya wageni vinaweza kuunganishwa na kusimamiwa kwa kutumia tu programu yetu. Uwezo huu utaboresha urahisi wa kusimamia vyumba vya wageni.
Pia, inaweza kuunganishwa na intaneti na ikaweza kufanya amri kadhaa zilizowekwa kulingana na ratiba itakayowekwa. Kwa mfano, katika ghorofa lenye nyumba nyingi za kupanga, kila chumba kinaweza kuwekwa mipangilio yake pekee. Jambo hili linawezesha kusaidia kuokoa umeme kwa kiasi kikubwa.
Model zingine mbili (RCU-24R-20Z na RCU8in-8out) zina uwezo tofauti ukilinganisha channel za input na output (24 channel output/20 channel inputs na 8 channel output/input ikiwa na output channel moja ya 0-10V) na inatakiwa kuchagua kwa kuangalia ukubwa na uhitaji wa mradi.
RCU Model zote zinaweza kuwekewa mipangilio yoyote ili kwendana na mradi wako. Kwa mfano, dimmers zinaweza kuongezwa ili kuendesha feni ya juu pamoja na taa pia katika chumba. Nyongeza, vitufe vya pande mbili vimewekwa kwenye module hizi ili kuwezesha mpangilio wa dharura pale inapotokea.
RCU inakujulisha ni kiasi gani cha umeme kinatumika kila siku, mwezi na mwaka. Zitakupa ripoti ya matumizi halisi ya umeme ambayo itakusaidia kuweka taratibu zitakazokusaidia katika usimamizi wa matumizi yako ya umeme.
Kifaa hiki ni imara na kinakusaidia katika kurahisisha mradi wako. Kutengeneza na kusimamia sasa inakuwa ni rahisi, na hoteli yako, mgahawa au maduka mengi n.k inakuwa kama vile unavyotaka: safi, yenye mpangilio na kufanya kazi vyema.
Inakuja hivi karibuni…
Tukuunge Mkono Katika Lengo Lako la Huduma ya Afya
Inafahamika vizuri kwamba virusi wengi wanasafiri kirahisi kupitia hewa hasa katika maeneo ya karibu karibu kama hospitalini. Zaidi, kwa sababu ya umuhimu wa usafi katika mazingira ya hospitali, kila jambo dogo linaweza kuwa na madhara katika afya za watu. Kwa kutumia TIS smart technology, wasimamizi wa hospitali hawahitaji kuhofia harufu ya chakula kinachopikwa jikoni, kemikali za madawa yaliyotupwa, au vitu vingine vinavyoweza kuathiri ubora wa hewa na kuathiri kupumzika kwa mgonjwa. Kihisio cha Afya (Health Sensor) kutoka kwetu kinakusaidia kuboresha ubora wa hewa kwa kurekebisha joto na kugundua gesi zenye madhara.
Suluhisho hili ni kihisio chenye muonekano mzuri wa fasheni cha juu kwenye dari chenye sifa kadhaa zinazoweza kumsaidia mtoa huduma hospitali, kliniki na taasisi zingine za afya.
Kihisio cha TIS Health Sensor kimefungwa na kihisio cha CO (carbon monoxide CO2, VOC, joto, unyevu, wingi wa mwanga na mwendo, kipaza sauti, input ya kidigitali 3, na njia 32 za logic na saa.
Fikiria hali ya hewa ya joto, ambayo, kwa mazingira yaliyofungwa kama ya hospitali, madirisha na milango inawezekana kwa kiasi kikubwa iko wazi. Kuongeza hewa safi ndani ya jingo kunaongeza pia hatari ya kupata wadudu hewani kama hewa haitachujwa vizuri. Zaidi, mfumo wa AC unaweza kuwa chanzo cha bacteria kukua kama haifanyi kazi kwa ufanisi wa kutosha. Suluhisho letu linaweza kugundua gesi hizo hatari kama vile CO, VOC na zaidi na kuboresha usafi wa hewa ya ndani.
Jambo zuri kuhusu kifaa hiki suluhishi ni kwamba kinafanya kazi vizuri katika miradi ya kibiashara na katika makazi ya watu pia. Kitakaa katika nyumba yako vizuri.
Usiwe na hofu kuhusu gesi inayoua kimya kimya, gesi ya CO; kihisio hiki kinawasha feni na kutoa tahadhari kwako pale CO itakapogundulika.
Kihisio cha TIS Health kinahifadhi joto la chumba lisibadilike na unyevu kuwa katika kiwango cha usalama ili kuepusha ukuaji wa kuvu katika ukuta. Nyongeza, kama joto la ndani likiongezeka kufikia kiwango cha hatari, kitakujulisha kwa ujumbe mfupi kupitia app ya simu ya TIS.
Katika kipindi cha majira ya baridi ambapo mabadiliko ya ghafla ya joto ni jambo la kawaida, kihisio hiki kinarekebisha hewa ili iwe salama na ya kufaa.
Ikiwa na input 3 za kidigitali na line 32 za logic, kihisio hiki pia ni cha muhimu katika nyumba za watu waliostaafu. Kivipi? Pamoja na sifa zake za kiafya, kihisio hiki kinaweza kuwekewa mipangilio ya Kupiga Simu kwa Nesi pembeni ya kitanda, kihisio cha mgandamizo kitandani (ikitokea mtu amedondoka kwa bahati mbaya kutoka kitandani), au kihisio cha kitando kilicholoa. Kujua kwamba msaada unapatikana kwa kubonyeza kitufe kimoja tu kunaleta amani moyoni, si ndiyo?
Pia, kama una mwanafamilia ambaye ni mzee anayeishi na wewe, unaweza kutumia teknolojia ya kipaza sauti iliyo ndani ya kihisio cha Health Sensonr. Hii, kama ikiwezeshwa, inaweza kuwa kama mfumo wa tahadhari kwa wazazi ambao ni wazee. Iwapo mzee akipiga simu, kihisio hiki kitatuma ujumbe mfupi wa maneno kwenye application yako ya TIS kwenye simu ya mkononi. Pia itatuma taarifa kwenye Panel ya Luna ya ukutani ya chumbani/sebuleni.
Habari njema kwa wazazi wote ni kwamba kihisio cha TIS Health Sensor kinaweza kuangalia chumba cha mtoto wako pia. Je, unataka kuhakikisha kama joto halizidi sana katika chumba cha mtoto wako? Iachie TIS Health Sensor ikusaidie kurekebisha joto likae kiwango kinachopendekezwa (68–72°F (20–22°C) na wataalamu. Sifa hii ni muhimu kwa sababu inapunguza hatari ya kifo cha ghafla kwa mtoto wako (SIDS). Pia kinaweza kuhifadhi unyevu katika chumba cha mtoto katika kiwango sahihi ili kuepuka magonjwa ya ngozi kwa mtoto mchanga. Kwa mfano, kama jua linawaka nje lakini ghafla mvua kubwa ikaanza kunyesha, kihisio chetu cha kijanja kitabadilisha joto na kiwango cha unyevu mara moja ili hewa ya ndani iendelee kubaki kuwa ya kufaa. Nyongeza, teknolojia ya kipaza sauti itakupa tahadhari mara moja kama mtoto wako akianza kulia. Na sifa nyingine ya ziada ni kwamba kihisio hiki cha kijanja kinaingiliana na kihisio cha mwendo cha TIS PIR Motion sensor, ambacho kinaweza “kuwasha taa” ikitokea mtoto wako akiamka au kuanza kulia gizani.
Pia, kwa sababu PIR sensor ina ufanisi katika kutumia umeme, kihisio chetu cha afya — punde tu baada ya kuunganishwa na kihisio cha mwendo — kinaweza kuwezesha uhifadhi wa umeme katika chumba kama kukiwa hakuna mtu.
TIS inafurahi kuwa sehemu ya waanzilishi katika kuleta kwenu bidhaa za huduma ya afya. Tunaamini kwamba unastahili kilicho bora, na tunayo bahati kukupa bidhaa janja katika maisha yako. Ili uendelee kuwa salama na afya bora duniani.
Tumia kwa Busara
Kwa sababu lengo letu kubwa ni kusimamia matumizi ya nishati pamoja na kuwasaidia wateja wetu kuokoa umeme, tunajaribu kutengeneza vifaa ambavyo vinatumia umeme mdogo kabisa na kutenda kazi kwa ufanisi mkubwa. Bus Energy Servant 10 Functions Sensor ni bidhaa nyingine kutoka TIS inayounganisha teknolojia ya kisasa na utengenezaji bora kabisa.
Energy Servant 10 Functions Sensor ni kihisio cha kwenye ceiling kilichotengenezwa kuwa na muonekano bora wa kipekee huku kikiwa na PIR motion sensor, light harvest sensor, relay outputs, digital inputs, temperature sensor, infrared emitter na 32 logic & timer lines zenye uwezo mkubwa kuhakikisha matumizi ya umeme yenye ubora mkubwa ikiwa na uwezo wa kuokoa mpaka 60%, ambayo ni karibu na $240 kila mwaka.
Unaweza kujiuliza, ni kwa jinsi gani inawezekana? Hizi ni baadhi ya njia ambazo kihisio hiki kinatumia kupunguza matumizi ya umeme. Bidhaa hii janja inazima kiyoyozi kama kutakuwa na mlango au dirisha lililoachwa wazi kwa dakika 1 au kama kutakuwa hakuna mtu ndani ya chumba kwa masaa 10. Zaidi ya hayo, kama kihisio chake cha mwanga kikigundua mwanga wa jua wa kutosha, kitazima taa moja kwa moja.
Baada ya kukifunga, utahitaji gateway ili kukiunganisha kwenye intaneti. Kisha, inaweza kuendeshwa na app za iOS au Android. Hata pale unapokuwa upo katika ufukweni mwa bahari ukifurahia muda wako, hautakuwa na mawazo kuhusu nyumba yako. Unaweza kuangalia kila kitu wakati ukiwa unafurahia kinywaji chako baridi huku ukiendelea kuota jua.
Kutokana na uwezo wake wa kutuma/kupokea IR, Energy Servant 10 Functions Sensor ina uwezo wa kufanya kazi kwa kutumia rimoti. Hivyo, unapoamua kuongeza teknolojia hii katika nyumba yako, fikiria pia kuongeza nyingine katika nyumba ya wazee wako katika familia yako pia. Zaidi ya hayo, hautapitia tabu ya kubonyeza kitufe mara kwa mara ili kuweza kufikia hali ya hewa ya ndani unayoitaka. Energy Servant 10 Functions Sensor inafanya kazi katika ufanisi mkubwa sana, na kufikia hali hiyo unayoihitaji inachukua sekunde chache tu.
Ina sifa za ulinzi pia; inaweza kugundua mwendo, kutoa taarifa kama kutakuwa na moto, au ikapiga kengele kama mlango au dirisha litafunguliwa. Vihisio hivi vya ziada vinaweza kuunganishwa na bidhaa za Bus, na kwa sababu ina 12V output, inaweza kutoa umeme pia. Hivyo, unaweza kukiunganisha na vihisio cha maji/gesi na ukapata taarifa kama kukitokea kuvuja kwa chochote kati ya hivyo.
Sifa nyingine ya Energy Servant 10 Functions Sensor ni uwezo wake kuunganishwa na huduma ya sauti ya Alexa wa Amazon. Sifa hii ni muhimu kwa watu ambao hawawezi kutembea kwa urahisi. Tunafuraha kuwezesha kila mtu kuweza kufurahia bidhaa zetu za kisasa.
Kifurushi hiki cha kisasa chenye gharama nafuu kabisa kinaweza kutumika na kuendana na aina yako ya maisha kwa urahisi. Utashangazwa na sifa nyingi ambazo zinapatikana ndani ya kifaa hiki kimoja tu.
Okoa Sayari Huku Ukifurahia Teknolojia ya Kisasa
Binadamu katika ulimwengu wa leo wanafurahia jitihada zinazofanyika katika uokoaji wa nishati kwani ni wazi kwamba teknolojia, kama haitatumika kwa usahihi, inaweza kuwa na uharibifu mkubwa. Kifaa kipya kiliyotengenezwa na TIS Smart Home Group, kinachoitwa TIS Bus PIR Motion Sensor chenye uwezo wa kupima mwendo, mwanga na muda mzuri wa kufanya kazi, kipo hapa ili kuweza kuchangia katika sayari yetu kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Tis Bus PIR ni kihisio ambacho kinafaa kutumika katika maeneo ambayo kugundua uwepo wa mwendo ni muhimu. Pia inaweza kuwekewa programu ili kumsaidia mtumiaji ili uweze kutumia kiasi kidogo kabisa cha umeme kadri inavyowezekana.
Ina lux meter ndani yake, ambayo ina uwezo wa kugundua kiwango cha mwanga na kusaidia kubadilisha mwanga wa ndani.
Kwa mfano, katika mabweni yenye mamia ya wanafunzi, kutakuwa na matumizi makubwa ya umeme kama taa zitakuwa zinawaka masaa 24 kwa siku 7 za wiki. Lakini pia kuzizima itasababisha shida. Kuwa na kihisio cha mwendo kama hiki katika chumba kitawezesha taa kuwashwa/kuzimwa yenyewe moja kwa moja pale ambapo kitagunda uwepo wa mwendo.
Kifaa kina 8 logics na timer kwa ajili ya kuweka muda ambao taa ziendeshwe. Kwa mfano unaweza kuchagua taa zizime inapopita dakika 1 hakuna mwendo au kuwasha mfumo wa kiyoyozi kwa dakika 5.
Sasa, unaweza kuwaza, “Je, ina maana taa zitajizima ninapokuwa ninasoma kitabu na nimekaa sehemu moja bila kutembea?” Jibu ni HAPANA. Bidhaa hii ni janja sana. Inaweza kuwekewa programu ili kuacha taa zibaki zikiwaka kwa muda ambao unasoma au kuziacha zikiwa zimezima muda unaokuwa umelala na ukajigeuza tu. Iwekee maelekezo hayo tu na kisha uwashe mipangilio ya “study” au “sleep”.
Lakini, unawez kuuliza, vipi kuhusu tofauti ya mwanga kulingana na majira tofauti tofauti? Basi, usijali. TIS Bus PIR Motion Sensor ina uwezo wa kugundua mwanga asili unaopatikana ndani ya chumba na kisha KUWASHA taa kama tu mwanga asili utakuwa hautoshi.
Suluhisho hili la kisasa linaweza kutumika maofisini, majikoni na katika sehemu zenye mazingira kama hayo.
Funga PIR Sensor ili uweze kusimamia matumizi yako ya umeme kwa njia yenye ufanisi mkubwa. Changia sayari ili kuifanya iwe sehemu nzuri ya kuishi kiteknolojia.
Salama Siku Zote.
Vifaa vingi vya kijanja vimetengenezwa ili kuondoa hatari zinazoweza kuharibu nyumba pamoja na kuboresha usalama. Tunajua kwamba majanga ya moto ni hatari, lakini uaribifu unaosababishwa na maji ni hatari na unatokea kwa wingi zaidi. TIS inakuletea vifaa vya kijanja ambavyo vinatoa taarifa kwa mtumiaji kunapokuwa na hatari ya uaribifu wa maji ili waweze kuchukua hatua kwa haraka.
Kihisio chetu cha Kuvuja kwa Maji kinagundua matone ya maji juu ya sakafu, bati, njia za juu(duct trays), au popote pale ambapo maji yanaweza kuvuja. TIS Water Leakage inafanya kazi kijanja na ni rahisi; unaweza kuiunga katika Wi-Fi yako, na itakutumia ujumbe mfupi moja kwa moja kukiwa na tatizo.
Baada ya siku ndefu kazini, itakuwa ni jambo la kukera kama ukirudi nyumbani na kukuta jiko limejaa maji chini. Kihisio chetu kinagundua punde tu maji yanapoanza kuvuja na kukupa taarifa kabla maji hayajafika mahali ambapo hayatakiwi kufika; bila kujali upo nyumbani, ofisini, au umeenda likizo, kitu pekee unachohitaji ili kutunza mali yako ni simu yako ya mkononi.
Tuamini, na utakuwa salama ukiondoka nyumbani kwa muda mrefu kadri unavyotaka. Kihisio cha maji kuvuja cha TIS Water Leakage kitaitunza nyumba yako.
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Furahia Maisha ya Kidigitali
Kuwa na mtandao janja wa kisasa ambao kila bidhaa, bila kujali ni kifaa kinachotumia teknolojia mpya au ya zamani, kinaweza kuwa cha kisasa na cha kujitegemea ndani ya mfumo wako wa uangalizi wa nyumbani na kukufanya kupiga hatua kubwa mbele.
TIS imeleta kwenu vifaa vingi vinavyofanya kazi nyingi ilikuweza kuboresha mfumo wa BMS. 4 Digital Inputs kutoka TIS ni moja wapo.
Module hii ndogo inatumika kuunganisha aina mbalimbali za vihisio vya kidigitali (digital sensors) ambazo huwa zinafanya kazi katika mpangilio wa NO/NC (Normally Open/Normally Close) katika mtandao wa nyumba ya kisasa. Ili kuweza kuelewa hili kwa undani zaidi, chukulia mfano wa kihisio cha moshi: Kina uwezo wa kugundua tu uwepo wa moshi lakini hakiwezi kufanya jambo lingine lolote zaidi ya hilo. Hivyo, ni lazima kuwe na kiunganishi ambacho kinaunganisha kihisio hiki na kifaa kingine ili kusudi hatua muhimu ichukuliwe.
Kwa kutumia 4 Digital Inputs kutoka TIS, utapewa taarifa pale mfumo utakapogundua uwepo wa moshi au maji kuvuja ndani ya nyumba yako, na unaweza kuchukua hatua husika. Module hii ya kisasa inahakikisha mali zako zinakuwa salama inapotokea kuna moto, au kuna tatizo katika pampu ya maji, na jambo lingine lolote la dharura.
Ukiwa na TIS’s 4DI, unaweza kuboresha swichi zako/swichi za kupunguzia mwanga za zamani bila kuhitaji nyaya za ziada. Hakuna haja ya kuziondoa swichi za zamani na kuweka mpya. Unachotakiwa tu kufanya ni kufunga 4DI module yetu na ufurahie kusimamia nyumba yako kwa furaha zaidi. Fafanua tukio fulani, kwa mfano, ta azote za jikoni ziwake kama swichi ikisukumwa chini, au isukume juu ili kuacha chandelier tu ibaki inawaka.
Pia, TIS 4DI module inaboresha mfumo wa ulinzi. Ikiunganishwa na sumaku za mlangoni kwa kupitia mtandao wa TIS-Bus, unaweza kukupa taarifa kama mlango/dirisha limeachwa wazi.
Wataalamu wa kidigitali kutoka TIS wamejaribu kutengeneza bidhaa ambazo zitakupatia huduma bora na kuwezesha BMS yako kufanya kazi katika njia fanisi kuliko zote.
Inakuja hivi karibuni…
Muda Wala Haupai.
Hakika muda ndiyo unaoamua kila kitu. Unatuambia ni lini, wapi na namna gani tufanye vitu tunavyotaka kuvifanya. Hivyo kuhakikisha una ratiba iliyosahihi ni muhimu sana.
TIS inakuletea msaidizi wako, anayetunza muda, Automation Timer, ambayo ni bidhaa janja ya kisasa ambayo inafanya kila kitu kinachohusiana na ratiba yako.
Ikiwa na 240 flags pamoja na 800 logic lines, TIS’s Automation Timer inaweza kubadilishwa mipangilio yake katika namna nyingi sana. Na kama nyongeza, module hii imefungwa na AND/OR/XOR/NAND logics (logics zingine kama vile XNOR, NOT, n.k zinaweza kuendelezwa), jambo linalokupa uwezo wa kupanga ratiba yako usio na mwisho.
Jambo zuri kuhusu saa hii ni kwamba inarudisha mipangilio yake pale umeme utakapokatika na baadae kurudi, hivyo kuweka program zake upya hakuhitajiki. Pia ina uwezo wa kufanya kazi bila internet.
Inafanya kazi kwa kuangalia eneo la kijiografia la mfumo. Pia ina uwezo wa kugundua muda jua linapochomoza/kuzama yenyewe na inaweza kuwekewa mipangilio ya kutekeleza programu flani katika muda fulani. Kwa mfano, mtu anaweza kutaka taa za nje za nyumba yake ziwake pale jua linapozama. Saa hii inayojiendesha yenyewe inaweza kushughulikia hili. Inaangalia pia tofauti ya muda kipindi cha majira tofauti, Kwa msaada wa timer, unaweza kuongeza ubora zaidi katika jengo lako.
Module hii inaweza kufanya kazi na Adhana, wito wa Waislamu kwenda kuswali. Saa hii inaokoa nishati sana. Fikiria kuweka mipangilio kiyoyozi na feni ya juu ya dari viwake dakika 30 kabla msikiti haujajaa watu, hivyo hakuna haja ya kuacha taa, kiyoyozi na mifumo ya kusafisha hewa vyote viwe vinawaka kuanzia asubuhi mpaka usiku. Pia, module hii inagundua moja kwa moja relay modes zote. Hata kama itakuwa imewekewa programu za kufanya hivyo, timer haistaweza kuwasha taa kama chandelier itakuwa imewashwa. Hii ni moja ya sera ya Msikiti wa Kijani.
Automation Timer hii pia inaweza kufanya kazi na TIS smart panels. Kwa mfano, kama ikiunganishwa na Luna panel, inaweza kugundua joto la ndani ya nyumba na, kama haitahitajika, itazima kiyoyozi.
Sifa nyingine ya bidhaa hii ni kwamba ina uwezo wa kugundua tarehe pia. Uwezo huu unawezesha kuiwekea program zinazofanya kazi kulingana na siku za wiki/wikiendi. Je, unapenda kuamka na kusikiliza sauti ya kipindi chako ukipendacho cha redioni katika siku za wiki? Automation Timer inaweza kukusaidia na hilo.
Ukiwa na Automation Timer kutoka TIS, unaweza kujihakikishia kabisa kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa.
“Kupanda kwa Walinzi”
Itakuwaje kama kila mda unapokuwa ukirudi nyumbani, ungeweza kuwa na uhakika kuwa unaweza kuwasha vifaa vyako vyote vya kuhisi (sensors) nyumbani kwako kwa kugusa na kidole chako tu? Ni kweli. Kampuni ya TIS Smart Home imetengeneza Security Module, bidhaa hii ya BUS inayoweza kutumika na vihisio vyote vya mwendo kutoka TIS na inputs za kidigitali.
Module hii ya ulinzi ina uwezo wa kubeba zaidi ya BUS input 3000 zilizogawanyishwa katika maeneo 8. Input hizi zinaweza kuwekewa maelezo na zikawashwa katika muda fulani tu. Kwa mfano, unaweza kuhitaji kihisio cha moto kiwe kimewezeshwa masaa 24 siku 7 za wiki, na huku ukihitaji kihisio cha mlango wa nyuma kiwe kimewezeshwa muda unaokuwa haupo tu.
Unaweza kuwezesha/kuzuia mfumo wako wa ulinzi kwa mipangilio tofauti, kuna vacation, away, day au night. Ni uamuzi wako. Kifaa hiki kimefungwa na saa ndani yake, module hii inaweza kuwekewa melezo pia kama iwezeshe/kuzuia hii mipangilio yenyewe moja kwa moja. Unaweza kuweza kuipanga module ya kwenye kampuni yako isimamishwe saa 2 asubuhi kila siku asubuhi na iwezeshwe saa 1 jioni kila siku za wiki. Zaidi, mpangilio wa vacation unaweza kuwezeshwa moja kwa moja inapofika wikiendi.
Matiki (logics) za kifaa hiki ni za kitaalamu kiasi kwamba haiwezi kuzuia moja kwa moja yenyewe palu unapokuwa umeweka mpangilio wa Away/Vacation.
Kifaa hiki kitaboresha mfumo mzima wa ulinzi katika jengo lako kwa kiasi kikubwa. Kukuachia muda wa kuingia na kutoka, saa ya kengele, na neon la siri imara ni baadhi ya sifa za muhimu za kifaa hiki cha ulinzi. Kwa mfano, kama mfumo ukigundua kuna muda mrefu sana usio wa kawaida umepita kati ya kuingia ndani ya nyumba na kuzuia mfumo, inagundua kuwa ni mwizi, na kengele inapigwa.
Kwa nyongeza, module hii inaweza kuwa sehemu muhimu sana katika vifaa vyako vya kusimamia nyumba. Ili kuweza kuelewa jambo hili vizuri, fikiria hili: kama mfumo ukigundua kuna mtu ameingia bila ruhusa, ta azote zinawashwa, kengele ya mwizi inawezeshwa, na simu ya moja kwa moja inapigwa katika kituo cha karibu cha polisi. Pia, kama kihisio cha moto kikigundua kitu chochote, viyoyozi vyote na mifumo ya feni itasimamishwa mara moja ili kusudi moto usienee.
Amini Module ya Ulinzi kutoka TIS. Boresha usalama wako, na uruhusu ikuongezee ubora katika maisha yako.
Injini ya Nyumba Yako Yenye Nguvu Kuliko Zote
Utafurahia maisha ya kutumia vifaa vya uangalizi wa nyumbani kwako kama vitakuwa haviji na thamani kubwa sana. Pia, ni muhimu sana kama faragha yako pamoja na matatizo ya utunzaji wa umeme vikitatuliwa huku ukiendelea kufurahia utumiaji. Bidhaa mpya za kisasa kutoka TIS zimetengenezwa sasa ili kukidhi mahitaji haya: TIS Motors sasa zinapatikana ili kuendesha aina zote za mapazia yako ya ndani pamoja na shades.
Mapazia ni moja ya sehemu muhimu katika muonekano wa ndani, ina nafasi ya kipekee katika faradha yako pia. Mara nyingine tunapendelea mapazia yawe yamefungwa, wakati muda mwingine tunafurahia tukiamka na kuona jua likiwa linachomoza kitandani kwetu. Mapazia yana manufaa pia katika kuhifadhi nishati. Kama mapazia yatabaki yamefungwa, kwa mfano, chumba kinakuwa kinapoa kwa haraka. Mapazia katika nchi zilizopo katika mzunguko wa Aktiki au karibia na maeneo hayo yana umuhimu mkubwa sana. Katika maeneo haya, kufunga mapazia katika muda sahihi wakati wa kiangazi ni muhimu sana ili kuweza kulala vizuri na kuwa na afya kimwili na kiakili.
Kifurushi hiki kina bidhaa tatu za kisasa: TIS-M3 Curtain Motor, TM-120 Roller Motor, na TIS-PRJ-LFT Projector Lift Motor.
TIS-M3 Curtain Motor: Motor hii inatumika kuendesha mapazia ya vitambaa. Ina antena ndani yake ya RF, ambayo inamaanisha kwamba una uwezo wa kutumia rimoti kuiendesha. Hata hivyo, hii haikuzuii kufungua mwenyewe kama ukihitaji. Kuchagua maandhari ni rahisi sana ukiwa na motor hii; unaweza kufurahia zaidi kufunga mapazia ya dirisha kubwa muda wa mchana ili kuhifadhi samani zako za ndani. Pia, unaweza kuhitaji mapazia yako yote yawe yamefungwa inapofika usiku. Unawezaje kufanya hivi? Ni rahisi sana. Fafanua tu mpangilio huu, na kisha gusa kitufe kimoja muda wowote unapohitaji kuuwezesha.
TM-120 Roller Motor: Kifaa hiki kinafaa katika maofisi, migahawa mikubwa na midogo, Inawezekana kuendesha roller au Roman/woven shades. Kwa kutumia kumbukumbu iliyowekwa ndani yake, motor hii inaweza kuwekewa programu na ikaweza kufungua/kufunga shades kwa asilimia fulani kulingana na muda wa siku. Kwa mfano, vifunika mapazia vya ofisi vinaweza vikawekwa kiasi kwamba vifungue vyenyewe saa za asubuhi na kwa 50% inapofika mchana. Asilimia hii inaweza kuongezeka kwa 70% jioni ambapo hali ya hewa ni nzuri.
PRJ-LFT Projector Lift Motor: Hii ni bidhaa ya mwisho katika vifurushi vyetu vya kijanja. Kwa ujumla inatumika katika vyumba vya mikutano, sinema, vyuoni n.k. Kifaa hiki kimetengenezwa maalumu kujificha juu ya dari pale ambapo kitakuwa kimemaliza kutumika. Kwa namna hii, dari lako linaonekana vizuri, huku ukifurahia kinyanyua projector cha hali ya juu.
Vifaa vyote hivi vinaweza kuunganishwa na kufanya kazi na mtandao wa TIS BUS, na hakuna haja ya nyaya za ziada utakapotumia njia ya kuunga kwa kuzunguka (looping method). Hii inamaanisha utaokoa nyaya, nguvu kazi pamoja na gharama.
Pia unaweza kutumia rimoti kuiendesha. Kama ni mpenzi wa teknolojia ya zamani, usisite kutumia rimoti. Vinginevyo, itabidi utumie tablet au simu yako ya mkononi au uguse amri kwenye kioo.
Hakuna tena kufungamana kwa nyaya usioeleweka; TIS Motors zimekuja kukusaidia kufurahia maisha yako kwa furaha na kwa ufahari yote huku matumizi ya umeme yakipunguzwa. Funga motor katika jengo lako na uache bidhaa za TIS kushughulikia kila kitu.
Injini ya Nyumba Yako Yenye Nguvu Kuliko Zote
Utafurahia maisha ya kutumia vifaa vya uangalizi wa nyumbani kwako kama vitakuwa haviji na thamani kubwa sana. Pia, ni muhimu sana kama faragha yako pamoja na matatizo ya utunzaji wa umeme vikitatuliwa huku ukiendelea kufurahia utumiaji. Bidhaa mpya za kisasa kutoka TIS zimetengenezwa sasa ili kukidhi mahitaji haya: TIS Motors sasa zinapatikana ili kuendesha aina zote za mapazia yako ya ndani pamoja na shades.
Mapazia ni moja ya sehemu muhimu katika muonekano wa ndani, ina nafasi ya kipekee katika faradha yako pia. Mara nyingine tunapendelea mapazia yawe yamefungwa, wakati muda mwingine tunafurahia tukiamka na kuona jua likiwa linachomoza kitandani kwetu. Mapazia yana manufaa pia katika kuhifadhi nishati. Kama mapazia yatabaki yamefungwa, kwa mfano, chumba kinakuwa kinapoa kwa haraka. Mapazia katika nchi zilizopo katika mzunguko wa Aktiki au karibia na maeneo hayo yana umuhimu mkubwa sana. Katika maeneo haya, kufunga mapazia katika muda sahihi wakati wa kiangazi ni muhimu sana ili kuweza kulala vizuri na kuwa na afya kimwili na kiakili.
Kifurushi hiki kina bidhaa tatu za kisasa: TIS-M3 Curtain Motor, TM-120 Roller Motor, na TIS-PRJ-LFT Projector Lift Motor.
TIS-M3 Curtain Motor: Motor hii inatumika kuendesha mapazia ya vitambaa. Ina antena ndani yake ya RF, ambayo inamaanisha kwamba una uwezo wa kutumia rimoti kuiendesha. Hata hivyo, hii haikuzuii kufungua mwenyewe kama ukihitaji. Kuchagua maandhari ni rahisi sana ukiwa na motor hii; unaweza kufurahia zaidi kufunga mapazia ya dirisha kubwa muda wa mchana ili kuhifadhi samani zako za ndani. Pia, unaweza kuhitaji mapazia yako yote yawe yamefungwa inapofika usiku. Unawezaje kufanya hivi? Ni rahisi sana. Fafanua tu mpangilio huu, na kisha gusa kitufe kimoja muda wowote unapohitaji kuuwezesha.
TM-120 Roller Motor: Kifaa hiki kinafaa katika maofisi, migahawa mikubwa na midogo, Inawezekana kuendesha roller au Roman/woven shades. Kwa kutumia kumbukumbu iliyowekwa ndani yake, motor hii inaweza kuwekewa programu na ikaweza kufungua/kufunga shades kwa asilimia fulani kulingana na muda wa siku. Kwa mfano, vifunika mapazia vya ofisi vinaweza vikawekwa kiasi kwamba vifungue vyenyewe saa za asubuhi na kwa 50% inapofika mchana. Asilimia hii inaweza kuongezeka kwa 70% jioni ambapo hali ya hewa ni nzuri.
PRJ-LFT Projector Lift Motor: Hii ni bidhaa ya mwisho katika vifurushi vyetu vya kijanja. Kwa ujumla inatumika katika vyumba vya mikutano, sinema, vyuoni n.k. Kifaa hiki kimetengenezwa maalumu kujificha juu ya dari pale ambapo kitakuwa kimemaliza kutumika. Kwa namna hii, dari lako linaonekana vizuri, huku ukifurahia kinyanyua projector cha hali ya juu.
Vifaa vyote hivi vinaweza kuunganishwa na kufanya kazi na mtandao wa TIS BUS, na hakuna haja ya nyaya za ziada utakapotumia njia ya kuunga kwa kuzunguka (looping method). Hii inamaanisha utaokoa nyaya, nguvu kazi pamoja na gharama.
Pia unaweza kutumia rimoti kuiendesha. Kama ni mpenzi wa teknolojia ya zamani, usisite kutumia rimoti. Vinginevyo, itabidi utumie tablet au simu yako ya mkononi au uguse amri kwenye kioo.
Hakuna tena kufungamana kwa nyaya usioeleweka; TIS Motors zimekuja kukusaidia kufurahia maisha yako kwa furaha na kwa ufahari yote huku matumizi ya umeme yakipunguzwa. Funga motor katika jengo lako na uache bidhaa za TIS kushughulikia kila kitu.
Injini ya Nyumba Yako Yenye Nguvu Kuliko Zote
Utafurahia maisha ya kutumia vifaa vya uangalizi wa nyumbani kwako kama vitakuwa haviji na thamani kubwa sana. Pia, ni muhimu sana kama faragha yako pamoja na matatizo ya utunzaji wa umeme vikitatuliwa huku ukiendelea kufurahia utumiaji. Bidhaa mpya za kisasa kutoka TIS zimetengenezwa sasa ili kukidhi mahitaji haya: TIS Motors sasa zinapatikana ili kuendesha aina zote za mapazia yako ya ndani pamoja na shades.
Mapazia ni moja ya sehemu muhimu katika muonekano wa ndani, ina nafasi ya kipekee katika faradha yako pia. Mara nyingine tunapendelea mapazia yawe yamefungwa, wakati muda mwingine tunafurahia tukiamka na kuona jua likiwa linachomoza kitandani kwetu. Mapazia yana manufaa pia katika kuhifadhi nishati. Kama mapazia yatabaki yamefungwa, kwa mfano, chumba kinakuwa kinapoa kwa haraka. Mapazia katika nchi zilizopo katika mzunguko wa Aktiki au karibia na maeneo hayo yana umuhimu mkubwa sana. Katika maeneo haya, kufunga mapazia katika muda sahihi wakati wa kiangazi ni muhimu sana ili kuweza kulala vizuri na kuwa na afya kimwili na kiakili.
Kifurushi hiki kina bidhaa tatu za kisasa: TIS-M3 Curtain Motor, TM-120 Roller Motor, na TIS-PRJ-LFT Projector Lift Motor.
TIS-M3 Curtain Motor: Motor hii inatumika kuendesha mapazia ya vitambaa. Ina antena ndani yake ya RF, ambayo inamaanisha kwamba una uwezo wa kutumia rimoti kuiendesha. Hata hivyo, hii haikuzuii kufungua mwenyewe kama ukihitaji. Kuchagua maandhari ni rahisi sana ukiwa na motor hii; unaweza kufurahia zaidi kufunga mapazia ya dirisha kubwa muda wa mchana ili kuhifadhi samani zako za ndani. Pia, unaweza kuhitaji mapazia yako yote yawe yamefungwa inapofika usiku. Unawezaje kufanya hivi? Ni rahisi sana. Fafanua tu mpangilio huu, na kisha gusa kitufe kimoja muda wowote unapohitaji kuuwezesha.
TM-120 Roller Motor: Kifaa hiki kinafaa katika maofisi, migahawa mikubwa na midogo, Inawezekana kuendesha roller au Roman/woven shades. Kwa kutumia kumbukumbu iliyowekwa ndani yake, motor hii inaweza kuwekewa programu na ikaweza kufungua/kufunga shades kwa asilimia fulani kulingana na muda wa siku. Kwa mfano, vifunika mapazia vya ofisi vinaweza vikawekwa kiasi kwamba vifungue vyenyewe saa za asubuhi na kwa 50% inapofika mchana. Asilimia hii inaweza kuongezeka kwa 70% jioni ambapo hali ya hewa ni nzuri.
PRJ-LFT Projector Lift Motor: Hii ni bidhaa ya mwisho katika vifurushi vyetu vya kijanja. Kwa ujumla inatumika katika vyumba vya mikutano, sinema, vyuoni n.k. Kifaa hiki kimetengenezwa maalumu kujificha juu ya dari pale ambapo kitakuwa kimemaliza kutumika. Kwa namna hii, dari lako linaonekana vizuri, huku ukifurahia kinyanyua projector cha hali ya juu.
Vifaa vyote hivi vinaweza kuunganishwa na kufanya kazi na mtandao wa TIS BUS, na hakuna haja ya nyaya za ziada utakapotumia njia ya kuunga kwa kuzunguka (looping method). Hii inamaanisha utaokoa nyaya, nguvu kazi pamoja na gharama.
Pia unaweza kutumia rimoti kuiendesha. Kama ni mpenzi wa teknolojia ya zamani, usisite kutumia rimoti. Vinginevyo, itabidi utumie tablet au simu yako ya mkononi au uguse amri kwenye kioo.
Hakuna tena kufungamana kwa nyaya usioeleweka; TIS Motors zimekuja kukusaidia kufurahia maisha yako kwa furaha na kwa ufahari yote huku matumizi ya umeme yakipunguzwa. Funga motor katika jengo lako na uache bidhaa za TIS kushughulikia kila kitu.
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Fanya Nyumba Yako Ikuimbie Wewe
Muziki unaleta uhai ndani ya nyumba yako. Unaweka pumzi katika mazingira yako. Kumekuwa na vifaa vingi vya kuchezea muziki ndani ya miaka kadhaa iliyopita, lakini hiki kimetengenezwa kwa kuzingatia wapenda muziki wanachopendelea. TIS Audio Player ni din rail module mpya yenye sifa nyingi ambazo zitafanya nyumba yako itoe sauti kama za kwenye kumbi za tafrija na kuongeza rangi ndani ya nyumba yako.
Kifaa hiki kina kikuza sauti cha stereo kilichotengenezewa ndani yake cha kiwango cha 2x24W pamoja na uwezo wa kusoma kadi ya SD ya mp3, inauwezo pia wa kucheza redio ya FM. Ikiwa na mfumo wa kutoa sauti yenye ubora wa hali ya juu, TIS Audio Player ndiyo kifaa pekee unachokihitaji katika uwanja wako nje kwenye bustani muda unapokuwa ukiongea na marafiki kipindi cha sikukuu. Spika zilizo katika eneo lako zote zinaweza kuungwa kufanya kazi na kifaa hiki cha kuchezea sauti.
Bidhaa hii imewekewa auxiliary outputs, ambazo zinawezesha kiweze kuunganishwa kwa urahisi na kifaa cha kukuza sauti kingine kilicho nje.
Lakini pia ina auxiliary inputs ambazo zinaweza kuunganishwa na TV pia, hivyo unaweza kusikiliza kipindi chako unachokipendelea cha kwenye TV muda unapokuwa unapika. Unganisha spika zilizo jikoni na kifaa cha TIS Audio Player na ufurahie utendaji kazi wake. Hakikisha tu hausahau kuhusu chakula!
Unganisha kadi ya SD kwenye kifaa cha TIS Audio Player. Watoto wako wanaweza kusikiliza hadithi kabla ya kulala kitandani wao wenyewe. TIS Audio Player ni Rafiki sana na inaweza pia kuendeshwa na rimoti.
Inaweza kusimamiwa kwa kupitia app ya TIS. Weka app hii kwenye simu yako ya mkononi ili uweze kusikiliza mechi ya timu yako unayoipenda wakati ukiwa unaendelea kufanya kazi ndogondogo za ndani.
Bidhaa hii inaweza pia kufungwa na mfumo wa BUS na vifaa vingine vya makampuni ya nje, kama vile vihisio vya maji kuvuja (water leak sensor). Kama utakuwa umebanana ukikimbia kwenye kifaa cha mazoezi ya kukimbia na kusikiliza nyimbo ya kuhamasisha na wakati umeacha mlango wazi, TIS Audio Player itakutaarifu. Pia, itakutaarifu kama kuna sehemu maji yanavuja popote ndani ya nyumba. Sifa hii ni muhimu sana kwa ajili ya usalama na pia kuokoa matumizi ya nishati.
Weka muziki unaochezwa nyuma kwa ajili ya mambo tofauti tofauti ili kuweza kutengeneza mazingira unayostaili ukiwa na TIS Audio Player.
Tengeneza Simfoni Yako Mwenyewe
Je, unataka kufurahia maendeleo ya kisasa katika kusimamia vifaa vyako vya umeme kwa kuvifanya vifanye kazi kwa pamoja kwa kushirikiana? Hivi ndivyo vitu unavyovihitaji: Infrared Emitter, bidhaa ya TIS BUS ili kuweza kuwasha kiyoyozi, TV na vifaa vingine kwa ajili ya matumizi ya viwango bora.
Kifaa hichi inaendana na matoleo ya makampuni mengi makubwa kama vile Samsung, Sony, LG, n.k.
Kifaa hichi kina infrared emitter port na kihisio cha joto (temperature sensor). Hii inamaanisha ya kwamba unaweza kuendesha kifaa chochote cha infrared ukikitumia, na kama ukihitaji kusimamia kiyoyozi cha nyumba yako, kihisio cha joto kipo hapo kukusaidia, kuhakikisha ya kwamba hakuna umeme ambao unapotea na joto la chumba chako muda wote lipo katika hali inayopendeza kwako na inasomeka katika app yako au programu yako. Kwa mfano, katika jingo kubwa kama vile hospitali, uwepo wa idadi kadhaa ya BUS IR Emitters zinaweza kuunganishwa kwa pamoja na kusimamia mfumo mzima wa kiyoyozi na kurekebisha joto la ndani. Spidi ya feni pia inaweza kubadilishwa kirahisi kama ikitokea kuna mabadiliko ya joto. Kwa njia hii, matumizi ya umeme yanakuwa yamepunguzwa, na kufanya pia mazingira ya hospitali kuwa katika hali nzuri.
Zaidi, bidhaa hii haikuzuii kutumia rimoti ili kuweza kuiendesha. Watumiaji wana uwezo wa Infrared Emitter na uwezo wa kutumia rimotu ya kifaa chenyewe katika kusimamia majengo. Chaguo hili linawafaa wale watu wanaopendelea teknolojia za zamani au wanaotegemea zaidi kutumia rimoti.
Sifa nyingine ya bidhaa hii ya BUS ni kwamba iko wazi kuwekewa ratiba. Inakupa uwezo wa kuweka kitendo fulani kitokee katika muda fulani, na inakusaidia kusimamia staili yako ya maisha kwa njia ya kisasa. Hebu fikiria wafanyakazi wako wanafika kazini kipindi cha baridi kali na kukuta jengo lina joto zuri linalopendeza pale watakapofika? Kiyoyozi kinaweza kupangiwa kiwake chenyewe moja kwa moja dakika kumi na tano kabla kila mtu hajafika.
TIS BUS Infrared Emitter inaweza kuwa ni kiongozi wako nyumbani. Inasimamia vifaa vyako vinavyotumia infrared ili vifanye kazi katika njia safi na inayokupendeza.
Jaza Chumba na Sauti Yako Uipendayo.
Unapokuwa ukitafuta spika sahihi, ni vigumu kuamua ni sifa gani ambayo ni muhimu kwako kuiangalia. Je, ni ubora wa muziki, muonekano, au muingiliano wake na visaidizi vya sauti (voice assistants)? Basi, tumekuja kukusaidia kuchagua spika ya kijanja iliyo na sifa zote hizi. TIS technology imerahisisha zoezi la kupata usimamizi bora wa sauti: TIS Speakers sasa zinapatikana kwa miundo mbalimbali za kufunga juu kwenye dari, na za kutumika nje zikiwa na ubora na muonekano mzuri zitapeleka usikilizaji wako wa sauti katika hatua ya juu.
The TIS 6.5” Frameless Ceiling Speaker ni kihisio (sensor) kinachofungwa katika dari, kinachopatikana katika umbo la duara na mraba . Furahia sifa za spika yetu isiyo na fremu ndani ya mgahawa wako wakati wa mechi ya mpira mubashara kati ya Real Madrid na Barcelona. Bidhaa hii pia ni chaguo bora kwa sehemu ya mazoezi(gym), chumba cha semina, mgahawa n.k.
The TIS Outdoor Wall Mount Speaker ni spika ambayo haiathiriwi na hali ya hewa na inapatikana katika rangi nyeusi na nyeupe ambayo imetengenezwa kwa ajili ya kufungwa katika ukuta wa nje. Je, umechoka na unahitaji kuburudika? Ondoa uchovu kwa kusikiliza muziki wako pendwa ukiwa umekaa kibarazani kwako.
The TIS Rock Speaker ni spika bora zaidi kwa matumizi ya sehemu ya wazi kama vile varandani, katika bwawa la kuogelea, ukumbini na nyuma ya nyumba yako. Spika hii inabebeka kwa urahisi yenye besi kubwa na sauti pana kwa ajili ya kutumika popote utakapopachagua. Chukua wazo hili: Kama watoto wako wameboreka na haujui namna gani ya kuwafurahisha, unaweza kutafuta tent la kuchezea watoto, weka nyuma ya nyumba, andaa bwawa la kuogelea, na kisha weka muziki na uandae mandhari. Kama ukitaka, unaweza hata kuiweka spika ndani ya maji ya kuogelea. Spika za TIS haziingii maji wala uchafu.
Tunajali mahitaji yako. Turuhusu tufanye tofauti katika bidhaa zako za sauti.
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Kwa Sayari ya Kijani Zaidi
Ni muhimu kuwa na taadhari juu ya matumizi yetu ya umeme tukiwa tunafurahia vifaa vyetu vya teknolojia ya kisasa. Ni jambo la busara kuhakikisha watoto wetu wanapata nafasi ya kuishi maisha ya furaha zaidi.
Wataalamu wa masuala ya kidigitali wa TIS huwa wanajaribu kutengeneza vifaa ambavyo vinafanya kazi kwa ufanisi ulio bora huku vikitumia kiasi kidogo cha umeme kadri iwezekanavyo. Bidhaa nyingi za TIS zinakuja zimefungwa na Energy Meter, kifaa cha umeme ambacho kinapima na kutoa ripoti juu ya matumizi ya umeme kwa siku, mwezi na mwaka.
Ni single-phase power meter ambayo inafanya mahesabu ya kiasi gani cha KW/H kimetumika katika eneo lako. Vipimo vingine vya umeme, kama vile amps, voltage na active power pia vinapimwa. Inaonyesha pia gharama za matumizi ya umeme kwa kuangalia data hizi.
Betri ambayo imefungwa ndani yake pamoja na 4 timing segments zinaiwezesha mita kunakili jumla ya umeme uliotumika kwa kipindi cha miezi 12.
Energy Meter hii ni zaidi ya meter yoyote tu ya kawaida ya kuhifadhi taarifa; imeungwa kama sehemu ya mfumo mzima wa kusimamia nyumba na inaweza kuwekewa mipangilio ili itume taarifa kama kukitokea matumizi makubwa kupita kiasi. Kama matumizi ya mwezi kwa mfano, yakifika au kuzidi matumizi ya ya juu ya kawaida (matumizi makubwa kupita kiasi yanaonyeshwa na mhimili mwekundu), Energy Meter inakupa taarifa na kukujulisha kuwa sasa ni muda wa kuokoa umeme zaidi. Energy Meter ni kiongozi katika kuokoa umeme; kama ikiwekewa programu iwe inafanya hivyo, itazima baadhi ya taa au kiyoyozi pale ambapo matumizi yakigundulika ni makubwa kupita kiasi.
Energy Meter ina nafasi ya kipekee sana katika mji wa kisasa. Pamoja na kila nyumba, ofisi, au duka kuwa na ripoti ya matumizi yake ya umeme, kila kitengo cha Umeme cha Mji kinaweza kufungua taarifa hizi kwa kupitia programu za TIS smart city ili kuweza kumudu gharama za umeme na utawanyishaji.
Bidhaa za kisasa za TIS zimetengenezwa ili kuweza kutoa utendaji kazi wa kiwango cha juu kinachotakiwa. Tunaamini ya kwamba sote tunaweza kuelekea katika ulimwenu wa kijani zaidi.
Hii ni kwa ajili yet una kwa ajili ya watoto wote.
Kuwa wa Kwanza Kuanzisha Maongezi
Pata taarifa za sasa juu ya hali ya hewa ukiwa na mtabiri wako binafsi. Kama huwa unafurahia kuwa wa kwanza kuanzisha maongezi juu ya hali ya hewa, basi utapenda kifaa hiki kipya kutoka TIS. Weather Station ni bidhaa inayofungwa nje ambayo inakupa taarifa zote muhimu za hali ya hewa utakazokuwa ukizihitaji.
Kihisio (sensor) hiki kina kipimo cha kasi ya upepo na uelekeo wake, kiasi cha mwanga, joto, unyevunyevu, UV na mvua.
Sio tu kwamba kifaa hiki kina uwezo wa kuripoti taarifa zote za hali ya hewa kwako bila kuungwa mtandaoni, lakini pia kina uwezo wa kuchukua hatua fulani kulinganisha na hali ya hewa iliyopo chenyewe moja kwa moja. Kwa mfano, kinaweza kuwekewa kisiwashe maji ya kumwagilia bustani katika siku za mvua, hivyo kukusaidia kutokupoteza maji. Kinaweza kubadilisha joto la ndani ya nyumba kulingana na joto lililopo nje, hivyo kukusaidia kuokoa umeme. Kwa mfano, inapotokea kuna joto sana mchana au kuna baridi sana usiku, kifaa chako cha Weather Station kitabadilisha chenyewe moja kwa moja joto la ndani ya nyumba ili kuwezesha hali ibakie kuwa nzuri na kutumia kiasi kidogo cha umeme kama inavyowezekana.
Weather Station pia inalinda nyumba yako kama ikitokea kuna hali ya hewa mbaya sana. Kama kuna upepo wenye kasi sana, madirisha na milango yako itafungwa, na utapewa taarifa. Kitalinda pia afya yako kwa kukupa taarifa kama joto likipanda na kuwa kali sana au kushuka sana na kukutumia ujumbe mfupi jana kihisio cha UV kikigundua kipimo kimefikia kiwango cha hatari, ili uweze kuhakikisha unajipaka mafuta ya kuzuia mwanga huu ya kutosha. Hili pia linalinda mipira na samani zako salama na kuharibiwa taratibu kwa sababu ya ongezeko la joto pamoja na mabadiliko katika mwanga.
Moja ya sifa za muhimu za bidhaa hii ni uwezo wake wa kuzuia fangasi. Kwa sababu fangasi wanakua vizuri sehemu za ndani ya ukuta na wanakua kwa kasi kukiwa na unyevu, ni muhimu kutazama na kuzuia unyevu ubaki katika kiwango sahihi. Weather Station kina uwezo wa kugundua unyevu wan je na inaweza kuweka kiyoyozi katika mpangilio wa kukausha na kuwasha dehumidifier kama kikigundua kuwa kuna ongezeko la unyevu . Sifa hii inafanya Weather Station kuwa na faida kubwa katika sekta kama vile ya kilimo, usafiri wa ndege, na zaidi. Kwa mfano, katika eneo ambalo linazalisha Wanyama, kama kiwango cha unyevunyevu katika hewa hakitakuwa katika kiwango sawa, vitu vilivyopo ndani ya jengo vinaweza kuharibika. Mtabiri huyu wa hali ya hewa anakulinda na kukuwezesha wewe kuwa tayari na mabadiliko ya hali ya hewa. Hakuna mtu anayependa mabadiliko ya ghafla katika hali ya hewa, na hiyo ndiyo sababu kifaa hiki kinaweza kuwa msaada mkubwa katika biashara yako.
Tunaamini ya kwamba ili tuendelee kuwatii wateja wetu, ni lazima tuzalishe teknolojia ambayo inakidhi mahitaji yao vizuri zaidi. Tunajua kwamba ili kuwa salama, ni lazima mtu apate taarifa. Weather Station iko hapa kwa ajili ya kukusaidia kufurahia na kukupa usalama katika maisha yako ya kibiashara.
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Gateway ya Teknolojia
TIS inakuletea bidhaa ambazo sio tu kwamba zitazidi mahitaji yako yote, lakini pia zitasimama juu ya bidhaa zingine zote kwa sababu ya kazi nyingi ambazo vifaa vyetu vinazifanya. Kwa mfano, IP-Com_Port ni module kwa ajili ya kufanyia mawasiliano iliyotengenezwa kwa ajili ya kuunganisha mtandao wa BUS na kutengeneza ulimwengu wa kijanja unaokupa nafasi nyingi za kuchagua.
Inafaa haswa miradi mikubwa, TIS’s IP-Com_Port inaunganisha na kushirikisha vifaa vyako vyote janja na kuvifanya kuwa rahisi kuvisimamia. Mpangilio wa nyaya katika TIS-BUS unabeba hadi vifaa 64 kwa kila waya. Katika miradi ambayo ina vifaa vingi sana, port ya IP inaweza kuongezwa katika kila mtandao ili kufanya kila kitu kiweze kuwa kimeunganishwa kwa pamoja. Ukitumia module za IP na nyaya za Ethernet, kusimamia mfumo wa mwanga, hali ya hewa, na mfumo wa ulinzi katika ghorofa kubwa inakuwa ni jambo rahisi kulifanya.
Pia, module hii inaunganisha mtandao wa BUS kwenye wireless gateway, na kukuwezesha kusimamia nyumba yako hata kipindi unapokuwa mbali na nyumbani. Hakuna haja ya kuongeza dongles au adapters. Unachotakiwa tu kufanya ni kuweka app ya TIS katika simu yako janja, na kisha utazame nyumbani/kazini kwako popote utakapokuwa.
Kama unataka kuunganisha bidhaa tofauti za makampuni tofauti, IP-Com-Port ndiyo kitu unachokihitaji. Kuunganisha na vifaa vya watengenezaji wengine inawezekana pia. Unaweza kuunganisha makufuli yote ya umeme, Mifumo ya viyoyozi ya VRV, na zaidi kwenye module hii na kisha ukatengeneza muundo wako binafsi wa vifaa vilivyounganishwa kirahisi. Kwa njia hii, kama mlango ukifunguliwa sehemu Fulani, taa inakuwa inawaka ndani ya chumba kitupu, au unakuwa na kiyoyozi kikifanya kazi kwa nguvu, unachohitaji tu ni simu yako ili uweze kuendesha kila kifaa.
Mwisho, kifaa hichi kina sehemu mbili za kuunganisha: RS232 na RS485. Kimewekewa ASCII pamoja na Hexadecimal python katika baud rate yeyote. Hii inamaanisha kiasi cha data kisicho na kiwango kinaweza kutumwa na kusomwa kwa kila sekunde, hivyo unaweza kutoa amri kwa vifaa vingi kwa kadri unavyotaka, na zote zitafanyika bila muingiliano wowote.
Ifunge, na uunganishe kila kitu. Furahia ulimwengu bora wa kisasa na TIS IP-Com-Port.
Kutana na Superman wa Vifaa janja vya kisasa
Kama vifaa vyako janja vimeunganishwa na nyaya kiasi au vinafanya kazi bila kutumia waya kwa kiasi fulani, usijali kuhusu hilo. Kampuni ya TIS Smart Home ipo hapa kuhakikisha haubanwi na mifumo ya aina yoyote. Furahia uwepo wa teknolojia ya kisasa itakayokurahisishia maisha yako. AIR-BUS Converter, sasa inapatikana kwa ajili ya kutumika kwa vifaa vinavyotumia waya na visivyotumia waya, hakika itaongeza thamani katika biashara yako.
Kiunganishi hiki kitakuwa ni kama daraja kuunganisha vifaa vyako vinavyotumia waya na vile visivyotumia waya. Hii inamaanisha ya kwamba kama una panel ukutani iliyofungwa na nyaya na pia una air ceiling sensor, vinaweza kuunganishwa na kuendeshwa kwa pamoja. Unapokuwa uko njiani kuelekea nyumbani, washa AC, ongeza mwanga wa sebuleni kwako, washa microwave oven ili kupasha chakula chako. Vyote hivi vinawezekana kwa kugusa kidogo tu na vidole vyako.
Air Bus ni mini converter ambayo inaboresha nyumba yako mara moja. Unachohitaji kufanya tu ni kufunga kifaa hiki pembeni ya au nyuma ya kifaa cha waya (wired module) na kisha weka mipangilio kwa ndani yake kwa kutumia app ya simu yako.
Suluhisho hili linaweza kutumika kuunganisha vifaa vya waya kwenye WiFi au kukuwezesha kutumia rimoti ili kuendesha au kubadilisha baadhi ya bidhaa zetu (Luna, Mars, Terre series) na kuwa WiFi Air panels. Kwa mgano, kuongeza itifaki za WiFi (WiFi protocol) ndani ya panel ya Luna TFT ndani ya ofisi yako inakuwezesha kuendesha kwa kutumia rimoti, hivyo unaweza kutumia panel ya Luna kuwasha kiyoyozi kikuu kwa kutumia simu yako ya mkononi. Air Bus Converter pia inaweza kutumika kama nyongeza katika panel zote za ukutani bila kuhitaji zile za zamani.
Air Bus converter inaweza kuja pamoja au bila power supply. TIS Air-Bus haitoi umeme kwa ajili ya vifaa vyako, lakini kama ukifunga TIS Air-Bus-3W, inaweza kutoa umeme kwa ajili ya kifaa. Hii inamaanisha kwamba kifaa kilichofungwa kinachotumia nyaya, kama vile Luna 9G panel, kinaweza kufanya kazi hata bila kufungwa na nyaya.
Nyongeza, kifaa hiki kina logics zaidi ya moja kwa ajili ya kuelezea utendaji kazi wa kifaa hiki cha kisasa, na kinakifaa kinachotumika kuweka ratiba ambacho kinakuwezesha kufanya ubora wa utendaji kazi wa vifaa vyote uende sawa. Air-Bus Converter kiujumla ni kama vile mwamvuli kwa ajili ya TIS IP Port na TIS Automation Timer; japokuwa ni kifaa kidogo, kinabeba uwezo wa kufanya kazi zao zote.
Kama vile unavyoweza kuona, Air Bus Converter ni supermana wa vifaa vya kujiendesha vyenyewe kikiwa na utendaji kazi wa kiwango cha juu na kinafanya uendeshaji wa vifaa vya aina yote kuwa rahisi kama kula keki. Jaribu leo.
Ya Thamani na Kwa Kila Mtu
Idadi ya vifaa janja vya majumbani kutoka katika makampuni mbalimbali inaongezeka kila siku, lakini sio vifaa janja vya majumbani vyote vina uwezo wa kutumika kwa matumizi mbalimbali kama vinavyotakiwa. Katika kupata muonekano bora unaofaa katika miradi ya aina yote, TIS inashirikiana na itifaki (protocol) maarufu. Bidhaa ya TIS BUS-KNX Converter ni bidhaa inayounganisha mtandao wa TIS BUS na mitandao maarufu ya KNX ya Ulaya kwa ajili ya kurahisisha zaidi maisha ya mtumiaji.
Kiurahisi, hii inamaanisha kwamba hakuna jengo ambalo hauwezi kulifanya kuwa la kisasa. Haijalishi kama unataka tu taa ya balbu, kamera ya ulinzi, au thermostat, unaweza kuanza na vifaa vyetu suluhishi. Unaweza kuendesha kitu chochote kama taa na joto mpaka makufuli na ulinzi, hata kama nyumba yako inatumia itifaki ya KNX protocol.
Tunaongeza ufahamu wa nyumba yako; hata kama vifunika madirisha vyako vinaendeshwa na KNX, bado vinaweza kujifunika vyenyewe moja kwa moja mchana kwa kutumia itifaki ya TIS protocol. Sio lazima kununua bidhaa nyingi au kuingia gharama kubwa ili uweze kufanya nyumba yako kuwa ya kijanja. Ukiwa na TIS BUS_KNX, taa zote, AC, swichi za ukutani, mapazia, makufuli, mageti, mota, na zaidi vinafanya kazi kwa pamoja kukupa starehe na ulinzi.
Hata hivyo, kifaa cha TIS BUS-KNX converter sio tu kinarahisisha maisha yako. Lakini pia kinakusaidia kuokoa gharama za kuongeza joto na za umeme. Kwa hiyo, kama unataka kufanya manunuzi yako kwa ajili ya sikukuu au kununua zawadi za ndani, kumbu kwamba moduli ya TIS BUS-KNX itakuwa ni zawadi bora kwa wapendwa wako.
Ukiwa na TIS, unafika mbali zaidi ya ukomo wa kufanya nyumba yako kuwa ya kidigitali kwa unafuu.
Upo tayari? Bonyeza!
Hata kama haitakuwa rahisi zaidi ya hapa, itakuwa ni bora zaidi. Je, ulishawahi kulazimika kuamka ili kufanya jambo dogo tu, halafu mwisho ukawa umesahau kuzima taa? Vifaa vya kisasa siku hizi vinatuwezesha kufanya mambo mengi kwa urahisi. Watengenezaji kutoka TIS Smart Home wanakuletea: TIS Remote Control, bidhaa yenye muonekano wa kwenda na wakati kiteknolojia. Rimoti hii nzuri yenye mikunjo mizuri ina vitufe 34 vya kubonyeza kwa ajili ya kusimamia mwanga, mapazia, kiyoyozi, kichezea muziki, redio n.k
Vitufe maalumu 12 vimetengenezwa kwa ajili ya uangalizi (wa taa moja moja au kundi la taa). Unaweza pia kutumia vitufe 3 ili kuingiza mazingira unayoyapendelea.
Kama umerudi nyumbani kutoka kazini na umechoka sana huwezi kutembea tena, ni sawa, pumzika tu kwenye sofa; TIS Remote Control ipo nawe. Ichukue na ufanye jambo lolote unalolitaka. Vipi kuhusu kuwasha kipindi chako unachokipenda katika redio ili kusikia taarifa za matukio ya sasa? Unaweza pia kufunga mapazia ili kuwa na mazingira ya ndani ya kupendeza zaidi huku ukiweka kiyoyozi chako katika kasi ya wastani na kuzima taa mbili au tatu ili kulala kwa muda mfupi katika sofa lako.
Kifaa hiki kinakuwa na kitufe cha Kuwezesha au cha Paniki. Wakati wa hali ya dharura unaweza kutumia vitufe hivi viwili kusimamia mfumo wako wa ulinzi. Kama ukijihisi upo hatarini, unaweza kufanya vitu kadhaa kwa wakati mmoja. Usichanganyikiwe. Ukibonyeza vitufe hivi viwili, simu ya kuomba msaada itaenda katika kituo cha karibu cha polisi, na simu moja kwa ndugu yako, na jirani unayemuamini. Kengele pia itawezeshwa. Unachotakiwa kufanya ni kuweka maelekezo kwa kadri unavyoona inafaa.
Rimoti hii ya kubeba mkononi inayopatikana katika rangi nyeusi na kijivu inakuwezesha kusimamia vifaa vyako vyote ya kisasa kwa kutumia mkono mmoja tu.
Kuishi kwa urahisi na usalama ndilo jambo ambalo tunajaribu kukupatia kwa kutumia TIS Remote Control, kwa sababu tunaamini kuwa unastahili.
Je, upo tayari kwa ajili yake?
Usalama na Urahisi Kurekebishika Ndani ya Bidhaa Moja.
Ufanisi na kudumu kwa bidhaa kunategemea na ubora wa umeme unaoingia. Haswa kama ni mfumo wa kujiendesha ambao kila kifaa kinakuwa kimeungana na kingine, kifaa cha kusambazia umeme (power supply) kinakuwa na nafasi muhimu. TIS Power Supply ina uwezo wa kuvipa umeme vifaa vyote vinavyotumia 24 VDC. Moduli hii inafaa kwa matumizi yote yanayohitaji umeme usiobadilika badilika wala kuhitaji kuangaliwa kila mara. Unaweza kuiacha nyumba yako kwa muda wowote utakaotaka; moduli yetu ya kusambazia umeme ni mlinzi wa mali yako.
TIS Power Supply ipo hapa kukusaidia ufurahie ufanisi mkubwa wa mfumo wako wa kujiendesha bila usumbufu wowote wa kukatishwa.
Meneja Mjanja wa Kisasa
Kusambaza nyaya kwa umakini katika maboksi ya umeme ni mradi mkubwa na unaochosha, lakini mahali ambapo kuna idadi kubwa ya nyaya, ni muhimu kama zitakuwa zimepangwa vizuri. Cable Manager ni din rail module kutoka TIS kwa ajili ya kufungia boksi za umeme na kupangia nyaya katika mpangilio safi na rahisi.
Module hii ina terminal 7 na ya muhimu sana katika utendaji kazi wa itifaki ya BUS (BUS protocol)
Acha upangaji wa nyaya kwenye boksi la umeme ubaki kuwa juu ya Cable Manager na ufurahie ufungaji msafi kila mara.
Ufahamu Pamoja na Utendaji Kazi
Siku hizi, watengenezaji wengi wapya wa kidigitali wanazindua vifaa vya kielektroniki, na nyumba zetu zimejaa vifaa vya makampuni mengi tofauti.
Bidhaa za kampuni ya TIS Automation Company vimetengenezwa ili kuweza kutumika katika mahitaji yote ya kisasa katika nyumba. Ili kuwezesha hili kutokea, tunakuletea IR Learner—code learner yenye ufahamu inayowezesha mtandao wa TIS uweze kupokea na kuunganishwa na vifaa vya kampuni lolote.
Kama kifaa cha infrared hakitafanya kazi na bidhaa ya IR kutoka TIS, kama vile Energy Servant 10F Sensor na IR Emitter, basi ni kwa sababu code zake hazipatikani katika maktaba ya TIS. Hapa ndipo IR Learner inapokuja na kuwa mkombozi. Itajifunza code mpya na kuzitunza katika kumbukumbu yake yenye ufahamu.
Unaweza kuhamisha data mpya kwenda kwenye PC yako kwa kutumia USB port na kisha kupakia kwenye kifaa chako cha TIS chenye uwezo wa infrared. Kumbuka, kutunza code katika kompyuta yako ni jambo la muhimu kwa ajili ya miradi mingine siku za mbele.
Unaweza pia kujaribu usahihi wa code mpya kabla ya kuweka taarifa zozote katika database. Chaguo la IR transmitter katika kifaa hiki linafanya aina yoyote ya data mpya ziwezekane kujaribiwa.
Waandisi wa TIS wanayo furaha kufanikisha kuboresha maisha yako ya kisasa popote utakapokuwa bila kujali unatumia kifaa cha kampuni gani.
Inakuja hivi karibuni…
Mpangilio Bora Zaidi.
Hata katika nyumba za kijanja, nyaya na vifaa vingine huwa vinahifadhiwa chini ya kabati au katika chumba cha chini ya nyumba. Umuhimu wa maboksi ya umeme huwa unapuuziwa katika miradi ya kujiendesha, japo ni muhimu sana kwa ajili ya usalama na ufanyaji kazi mzuri wa vifaa vingine. Pamoja na kutengenza bidhaa zingine za kijanja, TIS Automation Group pia wametengeneza Distribution Box la kipekee kwa ajili ya kupangilia waya vizuri na kwa usafi zaidi.
Boksi hili lenye muonekano wa kipekee lililofunikwa ndani yake kuna circuit breakers pamoja na vifaa vingine vya umeme vinavyolinda umeme kuwa sawa ndani ya nyumba yako. Pia vinalinda nyaya zako za umeme dhidi ya shoti na umeme kuzidi ambavyo vinaweza kupelekea hitilafu za umeme.
Kuna sababu kadhaa za kukufanya uhitaji kutumia boksi janja la usambazaji wa umeme kutoka TIS katika jengo lako. Kwanza, lina mfuniko wa kioo na kasha zuri. Lina muonekano mzuri na linaweza kukaa na kirahisi kuendana na muonekano wa ndani kwako. Pili, linabebeka kirahisi, ni rahisi kufunga, na kutumia, hivyo kila mtu anaweza kutumia. TIS DB Box imebeba reli nyoofu (modula rails) na vishikizo vya sumaku (magnetic fixings) kwa ajili ya kufunga na kupangilia kwa urahisi.
Mwisho, linasaidia kupunguza hatari ya kutokea kwa hitilafu za umeme ambazo wakati mwingine ni kiashiria cha kuwepo kwa tatizo katika sehemu ya usambazaji wa umeme. Ukiwa na TIS DB box, unaweza kuepuka matatizo ya mara kwa mara ya nyaya au shida ya umeme. Hata kama matengenezo yakihitajika kufanyika, mafundi wanaweza kurekebisha tatizo kwa urahisi zaidi, kwa sababu nyaya zote zimewekewa majina ndani ya bodi ya TIS smart Distribution.
Tuko hapa kukusaidia uwe salama huku ukifurahia teknolojia za kisasa kutoka TIS.
Hatua ya Mwisho kuelekea katika Ulimwengu wa Kujiendesha
Baadhi ya swichi za ukutani za TIS, kama vile Luna, Mars na baadhi ya bidhaa katika mlolongo wa Terre (Terre series) zinahitaji kifaa cha ziada nyuma ya swichi kuwekewa mipangilio ili kuingiliana na mtandao wa AIR/BUS na kisha kuanza kufanya kazi. Panel iliyoongezwa ni module ndogo iliyotengenezwa ili kutosha nyuma ya swichi na kuziwezesha kuwasha taa, FCU, mapazia, motor, na zaidi.
Bidhaa hii janja nay a kisasa inapatikana katika models nne:
ADD-3R-3A: Module hii ina relay channels tat una inatumika kuendesha taa 3 au feni 1xFCU yenye spidi ya Low/Med/High pamoja na kupooza/Kuongeza Joto/ Feni. Inaweza pia ikawekwa kwa namna ikaweza pia kuendesha mapazia pamoja na taa, hivyo ni wewe tu kuwa mbunifu na kutengeneza namna unavyotaka wewe.
ADD-3DL-12V: Module hii inatumika katika kuangalia pamoja na kusimamia kifaa chochote cha tatu kinachofanya kazi kwa kutumia umeme wa 12VDC, kama vile PIR au kihisio cha moshi. Kwa mfano, kama ukitaka kufunga kihisio kama hiki ndani ya jiko lako, sio lazima uwe na waya nyingi kutoka jikoni kwako mpaka kwenye boksi la kusimamia (control box); kifaa hiki kina uwezo wa kutoa umeme huo unaohitajika. Relay pamoja na swichi za kizamani pia zinaweza kuendeshwa na kifaa hiki.
ADD-2DL-IRR: Module hii inakaribia kufanana na module iliyopita lakini imewekewa na kitu kimoja cha ziada: kifaa cha nje cha kupokea infrared. Nyongeza hii katika panel inasaidia katika kuendesha swichi ambazo zinakuwa mbali na wewe au ziko mbali na upeo wa macho yako. Kama utatumia ADD-2DL-IRR, hauna haja ya kuweka chochote kwani panel ya swichi zote inakuwa katika sehemu moja. Kwa mfano, unaweza kutumia rimoti ya TIS ili kuzima taa zilizopo sebuleni wakati ukiwa umekaa katika chumba cha kupumzikia
ADD-2DL-IRE: Module hii inauwezo wa kubeba maeneo(zones) mawili na vifaa vya IR. Mara nyingi inatumika kwa ajili ya kusimamia kiyoyozi cha mgawanyiko (split AC). Inaweza kujifunza mpaka aina 64 za amri za IR (64 IR codes), na kama ikifungwa pamoja na emitter probe ikawekwa juu ya sehemu ya kupokea IR kwenye kifaa, inaweza kukiendesha kwa ufanisi mkubwa.
Sifa ya kipekee kabisa ya panel hizi nyongeza ni kwamba zinapunguza uhitaji wa nyaya kwa kiwango kikubwa sana. Pia ni nzuri kiuchumi kwa sababu ni vifaa vichache sana vinavyohitajika kufungwa. Lakini pia, vinahitaji nguvu ndogo sana ya binadamu. Panel hizi nyongeza zinakuhakikishia huduma ya usimamizi wa vifaa vyako kwa kiwango cha ubora na katika bajeti ya kiasi kidogo sana.
Na pia, zinaongeza mvuto na kupendeza ndani ya nyumba yako. Swichi za ukutani zinaweza kusambazwa katika sehemu tofauti za nyumba yako nzuri ili kusudi isitokee swichi moja ya ukutani ikajazwa na panel.
Ongeza module hii ndogo, na uiache ifanye mabadiliko makubwa katika maisha yako. Kwani ni mawazo madogo madogo ambayo huwa yanafanya mabadiliko makubwa sana duniani.
Rahisi na Laini
Kama unatafuta panel iliyotengenezwa vizuri sana kwa ajili ya nyumba yako, hii hapa ndiyo unayoihitaji. Bidhaa yetu katika mlolongo wa WiFi, Venera Switch ni ya kifahari iliyotengenezwa ili kukusaidia kusimamia taa, mapazia na shutters.
Swichi ya Venera ni swichi ya ukutani ya kugusa yenye namna mbalimbali za usimamizi. Ifunge kwa hatua tatu rahisi: Ondoa swichi yako ya zamani na uweke mpya, iunganishe na intaneti, na uanze kuitumia. Bila kujalisha nyumba yako ni nyumba ya kupangisha au ni nyumba yenye uwanja mkubwa mbele, ukishabadilisha swichi za zamani, swichi ya Venera inakuwa tayari kuanza.
Jambo pekee ninalotakiwa kufanya ni kuiunganisha tu kwenye intaneti kwa kutumia simu; kisha unaweza kuisimamia nyumba yako kutoka mahali popote ulipo. Swichi ya Venera ina WiFi ndani yake nyenye uwezo wa 2.4Hz, hii inamaanisha kwamba unakuwa na uwezo wa kufikia nyumba yako. Pale unapokuwa haupo na unahitaji maua yako yapokee mwanga kidogo, jambo unalotakiwa kufanya ni kufungua tu pazia la sebuleni kwa masaa kadhaa kwa kutumia simu yako ya mkononi.
Swichi ya Venera inaweza kubadilisha mwanga katika chumba chako cha kulala au mfumo mzima wat aa katika jengo. Inaweza kufanya yote. Panel ya swichi ya Venera inaweza kuunganishwa na kifaa chochote cha TIS kwa kutumia mtandao wako. Hii inamaanisha kwamba panel moja inaweza kubadilisha panel zingine zote, na unaweza kusimamia vifaa vingine vyote vilivyoungwa na TIS ndani ya nyumba yako kwa njia rahisi tu ya kuwasiliana na panel kwa kutumia programu ya simu.
Zaidi ya hayo, Venera ina saa ya mtandaoni muhimu sana. Kwa mfano, unaweza kuweka izime taa yako ya nje pale jua linapochomoza au kufunga mapazia pale mwanga wa jua unapotishia kuathiri samani zako.
Nyongeza, kifaa hiki kina mita ya umeme inayokupatia ripoti ya matumizi yako ya umeme ya mwezi na ya mwaka. Hii inakupa picha kamili juu ya matumizi yako ya umeme na utajua namna ya kutumia vizuri.
Unaweza kutumia rimoti pia kwa wale wanaopendelea. Swichi inaweza kuwasaidia babu zako na matatizo yao mengi sana. Hawahitaji kuwaza sana juu ya taa za nje usiku. Sio lazima watembee kwenda kuzima taa; ni kuwapa rimoti tu.
Panel hii janja inapatikana katika rangi nyeusi na nyeupe, unaweza kubadilisha mipangilio ya taa za kwenye vituge vya LED. Kama una picha ya nyuma rahisi pia, unaweza kuiwekea rangi ya maua kwa juu na upendezeshe ukuta wako, au kama rangi nyeusi inaendana vizuri na kinanda kilichopo ndani kwako, basi nenda kwenye mipangilio na uchague rangi. Kuna wigo wa rangi 256 za kuchagua, na unaweza kuifanya LED iwake na mwanga nusu ili uweze kuiona usike.
Ni rafiki na rahisi kutumia, swichi ya Venera ipo hapa kukusaidia kurahisisha maisha yako. Tuandike maisha yetu ya mbele kwa pamoja.
Kama vile Kipande katika Filamu ya Kukumbukwa
Mwanga unaweza kubadilisha kabisa namna unavyojisikia unapokuwa katika eneo. Lakini pia unaathiri namna vitu vinavyofanya kazi. Kuwa na kifaa kinachoweza kusimamia aina tofauti za mwanga ndani ya chumba inakupa nafasi kubwa ya kutengeneza mazingira mbalimbali. Kampuni ya TIS Smart Home inakuletea Venera Dimmer—panel ya ubora wa juu ya kusimamia kiwango cha mwanga ndani ya nyumba yako.
Panel hii yenye muonekano wa kifahari ina vitufe vitatu vya kugusa kwa ajili ya kuongeza na kupunguza mwanga. Unaweza kuweka kiwango cha mwanga kwa asilimia kulingana na kile unachopendelea.
Unachotakiwa kufanya ni kutoa swichi yako ya zamani, kisha kuibadilisha na Venera Dimmer, iunganishe kwenye intaneti, na kisha uweze kuchukua usimamizi wa taa za nyumbani kwako.
Kila aina ya taa inawezekana kuunganishwa na Venera Dimmer. Unatakiwa tu kufunga panel hii na kuanza kuweka mipangilio unayoipendelea wewe. Tengeneza mazingira ya kuvutia kwa kupunguza tu mwanga kwa kutumia kidole chako. Ukiwa na Venera Dimmer hautakaa kuwaza tena kuhusu mishumaa kuishia.
Venera Dimmer imetengenezwa na WiFi module ya 2.4Hz, na inajiunga moja kwa moja kwenye intaneti na itakufanya uweze kuzifikia taa zako popote ulipo. Uwezo huu unakuwezesha kubadilisha mipangilio yake kwa kupitia simu ya mkononi.
Venera Dimmer saa iliyopo mtandaoni pia ina manufaa makubwa. Kwa mfano, unaweza kuiwekea ratiba ya ndani ili kuweza kukupa kiwango fulani cha mwanga katika taa ya kwenye korido kwa muda tofauti ili kusudi, kwa mfano, unapokuwa unaamka usiku ili kutumia bafu, taa ya kwenye korido isikupofushe macho. Au, unaweza kuiwekea kwamba iwashe taa ya sebuleni mpaka mwisho wakati jua likiwa limezama katika siku za baridi kali. Hata hivyo, wewe ndio unachagua namna ya kuitumia, Venera Dimmer inafanya nyumba yao iwe na joto zuri nay a kung’ara.
Nyongeza, mita ya kuokoa umeme ndani ya Venera Dimmer ni kifaa cha muhimu sana katika kuangalia matumizi ya umeme kwa kila mwezi na mwaka. Kwa namna hii utajua ni lini na kwa namna gani ufaye matumizi yako uweze kuyafanya ili kuweza kuyasimamia vizuri zaidi.
Panel hii iliyo rahisi kutumia sasa inapatikana ikiwa na rangi nyeusi na nyeupe, na rangi ya vitufe vya kubonyeza inaweza kubadilishwa na kuchagua moja ya rangi kati ya rangi 256, hivyo basi yote inategemea na upendeleo wako wa muonekano wa ndani kwako.Vunga Venera Dimmer na ufurahie namna zote za kufanya uishi milele.
Venera Iko Sahihi Muda Wote
Ni kweli. Venera Thermostat Panel, bidhaa nyingine kutoka kampuni ya TIS, inajua kila kitu kuhusu hali ya joto katika eneo lako la makazi.
Thermostat hii ya ukutani ina WiFi ndani yake na ina vitufe vinne vyenye picha pamoja na skrini ya OLED ya inchi 1 inayoonyesha joto la sasa la ndani pamoja na spidi ya geni.
Kiurahisi unatakiwa kuibadilisha swichi ya thermostat yako ya zamani na kuweka kifaa hiki kipya na kisha, kiunganishe kwenye intaneti, na usimamie joto la nyumba yako kwa ufanisi.
Kufanya kazi na thermostat hii ni rahisi sana; gusa tu kitufe cha juu/chini ili kupandisha au kushusha joto mpaka itakapofika katika kiwango unachokipendelea. Kuongeza joto katika sakafu, FCU units, split AC na VRV AC vyote vinaweza kusimamiwa na thermostat hii.
Kifaa hiki kinaweza kusimamiwa kwa kutumia simu ya mkononi janja. Kikishaunganishwa tu kwenye intaneti, unaweza kutazama na kusimamia joto ndani ya nyumba yako kwa kutumia programu ya simu kutoka TIS. Nyongeza, kwa sababu programu hii inauwezo wa kutumia GPS, unaweza kuiwekea maelezo Venera Thermostat ili yenyewe moja kwa moja ijiweke katika mipangilio ya kutunza umeme pale unapokuwa uko mbali na kuweka joto linalofaa kabla haujafika nyumbani.
Kuwa na saa ndani kunafanya kifaa hiki kuwa na faida zaidi. Unaweza kufafanua muda fulani kifaa kiwake/kizime. Fikiria kama wazazi wako wanataka kukaa nyumbani kwako katika wikiendi au kama unafanya kazi katika studio yako ya nyumbani kwa muda fulani kila siku. Venera Thermostat kwa umakini itasimamia kiyoyozi chako kulingana na ratiba yako uliyoiwekea.
Panel hii inaweza kufungwa katika maeneo mengi ya makazi, ya kibiashara na katika viwanda. Inasaidia sana katika kuokoa muda unaokuwa unapotea. Kwa mfano, fikiria sehemu kama kwenye msikiti; sehemu kama hizi zinatumia umeme mwingi sana kila siku kwa sababu ya watu wengi wanaoingia. Hata hivyo, kama kiyoyozi kingekuwa kinaweza kujiwasha chenyewe dakika 30 kabla ya kila swala na kisha kijizima chenyewe baada ya kila swala, msikiti ungeweza kuokoa karibu 70% ya umeme unaotumika kila siku.
Kama nyongeza, panel hii ina mita ya umeme itakayokuonyesha matumizi ya umeme kila siku na kwa mwaka pia.
Thermostat hii nzuri inapatikana katika rangi Nyeusi na Nyeupe, na vitufe vyake vinaweza kubadilishwa rangi na kuwa rangi yoyote kati ya 256. Kama unavyoona, panel ya Venera Thermostat inatosha kukaa katika muundo wa nyumba yako, na inaweza kufungwa na ikakaa vizuri kabisa.
Iache Nyumba yako Ikutunze Wewe
Malengo yetu siku zote ni kutimiza mahitaji ya wateja wetu zaidi ya walivyotegemea katika njia iliyo na ubora zaidi, watengenezaji wa kampuni ya TIS smart home wanakuletea WiFi ADS controllers sokoni kwa ajili ya kusimamia aina yoyote ya vifaa vya umeme vya nyumbani (kwa mfano, kuzima/kuwasha, kupunguza mwanga, sequential layouts, na kuweka rangi za RGB katika taa).
Chini ni maelezo mafupi ya bidhaa zetu 3 kuu tunazozitoa katika mrorongo huu:
ADS Relays: Kifurushi hichi kinakuwa na swichi 2/3 za channel relay na zinatumika kusimamia taa, shutters, na vifaa vingine vya umeme.
Relay hii yenye teknolojia ya juu inasaidia kupunguza idadi ya swichi za zamani, lakini pia hata kama unapendelea kuwa na teknolojia ya zamani, ADS Relays zinaweza kuunganishwa na swichi za zamani. Kwa kufanya hivi taa za chumba cha kupumzikia, kwa mfano, kazini kutakuwa na swichi za ukutani zote na unaweza kuziwasha kwa simu yako ya mkononi.
ADS Dimmer: Bidhaa hii ni suluhisho na ina uwezo wa kupunguza mwanga wa taa ya aina yoyote ile. Inafanya kazi na imetengenezwa kwa ajili ya kutumika na mtu mwenye maisha ya aina yoyote, ADS Dimmers zinakuwezesha kubadili hisia ya mazingira yako kwa kuweka kiwango cha mwanga unachokipenda.
ADS RGBW: Kuna wigo mpana wa kuchagua rangi, kifaa hichi ni uvumbuzi mkubwa na wa kisasa katika kuwasha taa. Pamoja na rangi za msingi ambazo ni nyekundu, kijani, bluu na nyeupe, ADS RGBW inaweza kutengeneza mtiririko wa rangi zenye weusi tofauti (end-end sequential color shades) ili kufikia mahitaji fulani. Je, unasherehekea siku yako ya kuzaliwa? Unaweza kuweka mpangilio wa rangi zako unazozipendelea na kuunganisha na taa pamoja na muziki wako unaopendelea.
Kwa sababu vifaa vyote vya kwenye WiFi series, vimetengenezwa kuendeshwa kwa kutumia app ya simu ya mkononi ya TIS kwa ajili ya iOS na Adroid, hivyo hakuna kikomo cha maelezo unayoweza kuyatuma kwenye kifaa. Unaweza kusimamia nyumba yako ukiwa mahali popote.
Zaidi, kinaweza kutumika na msaidizi wa Amazon Echo na Alexa, hivyo unaweza tu kuongea amri yako, na kisha ADS controllers itatekeleza.
Kila kifaa ndani yake kuna muda ambao unaweza kutumika kuweka ratiba ya mambo ya kufanywa. Kwa mfano, unaweza kuiwekea maelezo Relay ifungue maji ili kujaza bwawa la kuogelea kila inapofika sikukuu na unataka kufurahi na familia yako. Au, Unaweza kuifanya ADS Dimmer kuonyesha mwanga mdogo wa bluu kila inapofika wikiendi unapotaka kutazama tamthilia. Pia, ADS RGBW inaweza kuwekewa programu ili kubadilisha taa ya chumbi kuwa nyeupe laini kila inapofika jioni na kuna mtoto anahitaji kufanya kazi yako ya shuleni.
ADS Relays pamoja na Dimmer zimefungwa na mita ya umeme inayoweza kukupatia ripoti ya kiasi cha matumizi ya umeme kwa sasa, mwezi na mwaka na itakujulisha kipindi ambacho mfumo unatumia umeme mwingi sana kupita kiasi.
Kifurushi hichi kinatoa mchanganyiko bora wa teknolojia, ubora na kufanya dunia iwe salama, ya kijani zaidi, na yenye matumizi bora zaidi.
Badilisha Nyumba Yako
Ili kuboresha zaidi urahisi kwa wateja wetu kutumia vitu vya internet (Internet of Things ‘IoT’), TIS inakuletea bidhaa ambayo inabeba teknolojia ya hali ya juu huku ikiwa na muonekano bora: ACM Controllers zetu zinakupa uwanja mpana wa kuchagua uangalizi unaotaka wewe.
Mrorongo huu wa WiFi series una bidhaa kuu tatu ndani yake na zinaweza kutumika kusimamia taa (kuwasha/kuzima/kupunguza mwanga), shutters, mageti na kuendelea. Zina umbo dogo, na zinaweza kuwekwa mahali popote unapohitaji kuziweka bila kuvuruga muonekano wa nyumba yako unaoupenda.
Chini ni uchambuzi mfupi juu ya mambo unayoweza kuchagua:
ACM Relays: Kifurushi hichi kinabeba relays 2 na kinatumika kuendesha taa na motor. ACM relays zinakuwezesha kubadilisha nyumba yako bila kuondoa swichi za zamani. Unachotakiwa kukifanya ni kuongeza tu hizi relays kwenye swichi za zamani, hivyo kama unataka kubakisha muonekano wa ndani ya nyumba yako uliokuwepo pamoja na kufurahia teknolojia mpya, bidhaa hii ni suluhisho bora kwako. Nyongeza, kila kitu kina kasi ukitumia ACM relays; geti lako la kuingilia na gari linafunguka pale tu unapowasiri, inakupatia urahisi kwenye vidole vyako, na nyumba yako itakukaribisha kwa milango wazi pale tu utakapogusa kitufe kimoja tu.
ACM Dimmer: Kifaa hichi ni suluhisho la gharama nafuu sana kwa watu wanaotaka kubadilisha taa za kuwasha kwa kubonyeza bila ya kuondoa swichi za zamani. Unapoongeza kifaa cha ACM Dimmer, unachotakiwa kufanya ni kubonyeza na kushikilia swichi mpaka ifikie kiasi cha mwanga unachokitaka. Je, unahitaji kupunguza mwanga kidogo tu kwa ajili ya kujisomea jioni? Swichi hii ya kupunguzia mwanga itakutatulia tatizo hili.
Imetengenezwa na Muonekano Bora kwa Matumizi Muhimu
Je, unatafuta kifaa rahisi kinachoweza kufanya mambo mengi? Basi umekuja sehemu sahihi. Kampuni ya TIS Smart Home Company inatoa moja ya bidhaa rahisi na Rafiki kutumia huku ikikuwezesha kusimamia vitu vingi sana. Bidhaa yetu ya Air Socket ni moja kati ya bidhaa zetu zinazofanya kazi bora sana kutokana na urahisi wake wa kuhamishika.
Unaweza kufunga kifaa hiki sehemu yoyote utakayoihitaji bila kupata ugumu wowote. Unachotakiwa kufanya tu ni kukichomeka tu popote unapokihitaji. Mengine yanabaki katika vidole vyako.
Socket hizi, ambazo zinapatikana katika rangi nyeupe, zina muonekano mzuri na ni rahisi kukaa katika muonekano wowote wa ndani.
Kuna aina mbili za socket: Relay na Dimmer.
Aina ya kwanza ina uwezo wa KUWASHA/KUZIMA taa pamoja na vifaa vingine vya umeme. Kama wewe ni mshabiki wa mpira wa miguu ambae huwa unaishia kulala usingizi katikati ya kipindi cha pili, basi unaweza kuiwekea mpangilio TV yako iwe inajizima yenyewe unapofika muda Fulani. Kifaa hichi kidogo lakini kinachofanya kazi kubwa ni msaidizi mkubwa sana kipindi unapokuwa mambo mengi na huwezi kuyasimamia peke yako. Kama marafiki zako wamekwambia watafika muda sio mrefu, unaweza kutumia Air Relay Socket ili kuwasha heater ya umeme uweze kuweka joto la chumba sawa kabla hawajafika. Au kama ukitoka nyumbani na haukumbuki kama umezima pasi ya umeme, unaweza kuangalia kwa urahisi kwa kutumia simu yako ya mkononi, na ukaweza kuizima kwa kugusa tu na kidole. Air Sockets ni zawadi bora sana kwa marafiki ambao ni wasahaulifu.
Air Dimmer Sockets zinaweza kuunganishwa na aina yoyote ya taa, na zinatoa kiwango cha mwanga bora sehemu yoyote kadri utakavyohitaji. Kwa mfano, unaweza kupunguza mwanga wa taa yam toto wako ili asome usiku na kuwa kama mwanga wa mwezi. Pia, unaweza kuchomoa na kuihamisha socket sehemu yoyote utakayotaka. Je, ungependelea taa ya bafuni ipungue mwanga kidogo? Au taa ya kwenye ngazi na ya nje? Hakuna kikomo. Air Dimmer Sockets zinahamishika kwa urahisi na ni rahisi sana kuzitumia.
Vifaa hivi vyote vimefungwa na WiFi module ndani yake, hivyo vinaweza kuunganishwa moja kwa moja kwenye intaneti. Hii inakuwezesha wewe kuvisimamia popote ulipo. Kwa mfano, unapokuwa unarudi nyumbani baada ya siku ndefu sana kazini, hakuna kitu kizuri kama chai nzuri kabisa kwenye kochi lako. Unaweza kuwasha jagi la kuchemshia chai, na unapoingia ndani, ukaikuta iko tayari.
Sockets hizi pia zinakujulisha ni kiasi gani cha umeme umetumia kwa siku/mwezi/mwaka, data ambazo ni muhimu sana kuwa nazo kama unaijali dunia na mfuko wako pia.
Air Sockets pia zinaweza kuunganishwa na mfumo msaidizi kutoka Amazon, Alexa. Hii inakupa uwezo wa kutoa amri kwa kutumia sauti kama itahitajika. Kama ikitokea kuna mgonjwa, misuli kuuma, au hata kama utakuwa umeweka simu yako katika chumba kingine, sio lazima usimame kwenda kuwasha mashine ya kuoshea vyombo au nguo . Mwambie tu Alexa kile unachotaka kifanyike.
Kampuni ya The TIS Smart Home Company inaunganisha teknolojia ya kiwango cha juu kabisa pamoja na utendaji kazi bora ili kukupatia bidhaa bora zenye muonekano mzuri na kutoa huduma za kufaidisha katika ulimwengu wetu wa leo.
Tengeneza Simfoni Yako Mwenyewe
Je, unahitaji kufurahia maendeleo ya kisasa katika kusimamia vifaa vyako vya umeme ambavyo vinafanya kazi kwa pamoja au kwa kutojitemea katika namna inayopatana? Hiki ndicho unachokihitaji. Air Infrared Emitter, Kifaa kilicho na TIS WiFi kwa ajili ya kuendesha kiyoyozi, TV, sinema ya nyumbani, na vifaa vingine kwa ufanisi wa hali ya juu.
Controller hii inaweza kufanya kazi na vifaa vya kampuni lolote kubwa duniani ikiwemo Samsung, Sony, LG n.k na pia inapatikana katika aina mbili: AIR-1IRE-T na AIR-2IRE.
AIR-1IRE-T: Kifaa hiki cha Air kina infrared emitter port na kihisio cha joto (temperature sensor). Hii inamaanisha kwamba unaweza kuendesha kifaa chochote kinachotumia infrared na kusimamia matumizi ya kiyoyozi chako cha nyumbani kwa kutumia kihisio cha joto, ili kusudi usipoteze umeme na joto la chumba muda wote liwe kiwango kinachopendeza. Kwa mfano, fikiria kama ukiamua kufanya sherehe ndogo kwa ajili ya mwenzako. Kwa kutumia simu yako ya mkononi na kubonyeza kidogo tu ukiwa njiani, unaweza kuwasha kiyoyozi na kuweka joto linalopendeza n ahata kuwasha muziki na kucheza muziki wa “Happy Birthday” muda unapofungua mlango. Inapendeza, au sio? AIR-1IRE-T itakusaidia kutengeneza kumbukumbu za kudumu.
AIR-2IRE: Emitter hii ina infrared port 2 zilizotengana zinazotumika kuendesha vifaa viwili vya infrared vya kampuni moja kwa wakati tofauti; lakini, kifaa chake kikuu inachokitumia ni vifaa vya sinema ya nyumbani kama vile TV, DVD, SAT BOX, Apple TV box n,k. Ulishawahi kukutana na muda ule ambao rimoti inapotea haionekani na unalazimika kuzima na kuwasha kifaa kwa kutumia kitufe cha KUZIMA/KUWASHA kilichopo kwenye kifaa chenyewe? Hakuna haja tena ya kutunza rimoti 5 au 6 pembeni yako. Kuendesha vifaa vyako vya sinema ya nyumbani inakuwa ni rahisi sana pale mipangilio yako yote unapoweza kuiweka katika iPad au iPhone yako?
Panel hizi mbili zinashirikiana uwezo wa kujiunga moja kwa moja kwenye intaneti, na kwa sababu zimetengenezwa zikiwa na teknolojia ya WiFi ndani yake, inawezekana kuvisimamia bila kuhitajika kuwepo katibu. Hakikisha tu ya kwamba una app ya TIS kwenye simu yako janja ya mkononi.
Zaidi, havikuzui wewe kutumia rimoti. Unaweza kutumia vyote infrared Emitter pamoja na rimoti ya kifaa kingine ili kuweza kuziendesha. Chaguo hili linapendelewa sana na wale watu wanaopenda teknolojia ya nyuma au wanapendelea tu kutumia rimoti ya kawaida.
Sifa nyingine ya kifaa hichi cha Air product ni kwamba inawezekana kukiwekea ratiba. Kupanga tukio fulani lifanyike katika muda Fulani, na kukiachia kikusaidie. Hebu fikiria kufika dukani kwako na kukuta mazingira ya hali ya hewa ni ya hali ya joto kidogo wakati wa kipindi cha asubuhi majira ya baridi kali. Je, haitapendeza kwa wafanyakazi wenzako kama hawatalazimika kusubiri joto liongezeke kidogo dukani pale wanapofika ofisini? Kiyoyozi kinaweza kuwekewa mipangilio ya kuwaka chenyewe robo saa kabla ya kufika.
Athan logic inatatua tatizo hili, haswa kwa waislamu. Infrared emitter inaweza kuwekewa ratiba ya kuwasha/kuzima mfumo wa kiyoyozi katika muda fulani. Kuacha mfumo wa kiyoyozi UNAWAKA muda wote ndani ya msikiti unasababisha kupotea kwa umeme mkubwa sana, hivyo ni busara kuwasha tu muda ambao kuna watu ndani yake. Kwa mfano, kama adhan ani saa 06:45 mchana, viyoyozi vya msikitini vinaweza kuwekewa mpangilio wa kuanza kuwaka kwanzia saa 6:15 mchana. Kwa njia hii, hata kama kunapotokea mabadiliko ya muda wa Athana wakati wa majira tofauti, mfumo wa kiyoyozi bado unaendelea kuwaka nusu saa kabla mtu yoyote hajafika. Kufanya hivi kunahakikisha uangaliaji wa umeme ni wa kiwango cha juu.
TIS’s Infrared Emitter inaweza kuwa kiongozi wako. Inasimamia vifaa vingine vya infrared ili vifanye kazi kwa usahihi na pia muda huo huo kuzingatia uokoaji wa matumizi ya umeme.
Hifadhi Joto Ndani Hata Katika Kipindi Kirefu cha Baridi.
Joto linapotakiwa ni ndoto ya wengi. Hakuna kitu kizuri zaidi ya kuwa na chumba chenye joto katika miezi yenye baridi kali sana bila kuwa na hofu ya kuwa na bili kubwa. Lakini kurekebisha joto ndani ya chumba cha ukubwa fulani na muda fulani wa siku, kawaida, imekuwa ni changamoto. Hata hivyo, siku hizo sasa zimekwisha, kwa kuwa TIS sasa imekuja na suluhisho litakalofanya kuhifadhi joto kuwe rahisi na fanisi zaidi.
Kifaa cha TIS Thermostat Radiator Valve kitafanya joto la kila chumba kuwa sahihi. Kinatumia ufahamu wa kujiendesha (automation intelligence) kuongeza joto katika vyumba bila ya kuongeza gharama ya umeme. Kifaa hiki kisichotumia waya, kinatumia betri na kina uwezo wa kuhifadhi joto la chumba kwa usahihi.
Kifaa hiki kinarekebisha radiator kwa kufungua na kufunga chanzo, na kukuruhusu kubadilisha radiator bila kuhitajika kuwepo karibu.
Kwa kifaa hiki, unakuwa na njia nyingi za kusimamia radiator katika nyumba yako: unaweza kuzifanya zijiendeshe na kuweka ratiba ya kuwaka, unaweza kutumia app ya TIS katika simu yako kuweka kiwango cha joto kama una intaneti, na unaweza kubadilisha kwa kutumia vitufe vilivyopo juu yake pia katika kioo chake cha kugusa cha LCD.
TIS TRV inaingiliana pia na teknolojia ya eneo la kijiographia (geo-location technology). Hii inamaanisha kwamba inajua kama umeondoka au umerudi nyumbani. TRV inatumia teknolojia hii kufungua radiator muda muafaka ili kukukaribisha katika mazingira yanayopendeza unaporudi nyumbani katika kipindi cha baridi kali. Nyongeza, unaweza kupunguza bili ya umeme, kwa sababu kifaa hiki ni rafiki kwa mazingira na kinawaka kuongeza joto la chumbani pale tu inapohitajika. Pia kinarekebisha joto la chumba husika. Fikiria namna inavyopendeza kuingia ndani ya jiko lenye joto kuchukua kikombe cha kahawa asubuhi na kutokuwa na hofu ya hela kupotea kwa kuongeza joto la chumba ambacho hakitumiki.
Tunakushauri ufunge TIS TRV leo na upunguze gharama yako ya nishati huku ukifurahia mfumo unaojiendesha wa kusimamia joto.
Okoa Sayari Huku Ukifurahia Teknolojia ya Kisasa
Binadamu leo wanafurahia pale kunapokuwa na uokoaji wa nishati, kwa sababu imegundulika kwamba teknolojia inaweza kuwa na uharibifu mkubwa kama isipotumika kwa usahihi. Bidhaa mpya iliyotengenezwa na TIS Smart Home Group, inayoitwa TIS Air PIR Motion Sensor inafanya kazi kwa kuangalia mwendo, kiasi cha mwanga na muda, na ipo hapa kusaidia kuchangia katika sayari kwa kutumia teknolojia yake ya kisasa.
Tis Bus PIR ni kihisio ambacho kinafaa kutumika katika maeneo ambayo kugundua uwepo wa mwendo ni muhimu. Inaweza kuwekewa programu ambazo zitaiwezesha kutumia kiwango kidogo kabisa cha umeme kinachowezekana.
Pia ina lux meter, ambayo ina uwezo wa kugundua kiwango cha mwanga na kusaidia kubadilisha mwanga wa ndani.
Kwa mfano, katika mabweni yenye mamia ya wanafunzi, kutakuwa na matumizi makubwa ya umeme kama taa zitakuwa zinawaka masaa 24 kwa siku 7 za wiki. Lakini pia kuzizima itasababisha shida. Kuwa na kihisio cha mwendo kama hiki katika chumba kitawezesha taa kuwashwa/kuzimwa yenyewe moja kwa moja pale ambapo kitagunda uwepo wa mwendo.
Kifaa kina 8 logics & timer ambavyo unaweza kuweka muda ambao taa ziendeshwe. Kwa mfano unaweza kuchagua taa zizime inapopita dakika 1 hakuna mwendo au kuwasha mfumo wa kiyoyozi kwa dakika 5.
Hii inaleta baadhi ya maswali: Je, taa ZITAZIMA nikiwa nimekaa sehemu moja ninasoma kitabu na sitembei? Jibu ni HAPANA. Bidhaa hii ni ya kisasa. Inaweza kuwekewa programu ili kuacha taa zibaki ZINAWAKA kwa muda ambao unasoma au kuziacha ZIMEZIMA muda unaokuwa umelala au unapojigeuza. Iwekee maelekezo hayo tu na kisha uwashe mipangilio ya “study” au “sleep”.
Na vipi kuhusu tofauti ya mwanga kulingana na majira tofauti tofauti unaweza kuuliza? Basi, usijali. TIS Bus PIR Motion Sensor ina uwezo wa kugundua mwanga asili unaopatikana ndani ya chumba na kisha KUWASHA taa kama tu mwanga asili utakuwa hautoshi.
Suluhisho hili la kisasa linaweza kutumika maofisini, majikoni na katika sehemu zenye mazingira kama hayo.
Funga PIR Sensor ili uweze kusimamia matumizi yako ya umeme kwa njia yenye ufanisi mkubwa. Changia sayari ili kuifanya iwe sehemu nzuri ya kuishi kiteknolojia.
Tumia kwa Busara
Lengo letu kuu likiwa ni kusimamia matumizi na uokoaji wa umeme na nishati kwa wateja wetu, tunajitahidi kutengeneza bidhaa zinazotumia umeme wa kiwango cha chini kabisa na kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu. 10-Function AIR Energy Servant ni bidhaa nyingine ya TIS ambayo inaunganisha teknolojia ya kisasa kabisa pamoja na muonekano bora wa kifahari.
10-Function AIR Energy Servant ni kihisio cha juu kwenye dari (ceiling sensor) kilicho na muonekano mzuri na ikiwa na PIR motion sensor, light harvest sensor, relay outputs, digital input, temperature sensor, infrared emitter, 32 logic na timer lines kikiwa na uwezo mkubwa wa kuokoa matumizi ya umeme (jumla ya 60% inaokolewa, ambayo ni sawa na takribani $240 kila mwaka).
Ni kwa namna gani 10-Function AIR Energy Servant inaweza kuokoa umeme? Bidhaa hii suluhisho inazima kiyoyozi kama kuna mlango au dirisha ambalo liko wazi kwa zaidi ya dakika 1 au kama hakuna mtu ndani ya chumba kwa masaa 10. Zaidi ya hapo, kama kihisio chake cha mwanga kikigundua kuna mwanga wa jua wa kutosha, moja kwa moja yenyewe itazima taa.
Baada ya kukifunga, unaweza kukisimamia kwa kutumia app za iOS na Android. Ina WiFi module ndani yake na kufanya iwezekane kusimamia taa, mapazia na joto la chumba kutoka eneo lolote ulilopo duniani. Hata pale unapokuwa unafurahia na familia yako ufukweni, hautakuwa na mashaka kuhusu nyumba yako. Utakuwa na uwezo wa kusimamia kila kitu katika simu yako huku ukifurahia kinywaji cha baridi chini ya jua.
Pia inakupa ripoti ya siku, mwezi na kwa mwaka ya matumizi yako ya sasa ya umeme.
Kwa sababu ya uwezo wake wa kutuma/kupokea IR, 10-Function AIR Energy Servant inaweza kufanya kazi kwa rimoti au kuunganishwa na huduma ya sauti ya Alexa kutoka Amazon, ambayo ni msaada mkubwa kwa wanafamilia au marafiki ambao wanashida katika kutembea. Tunafurahi sana kila mtu anaweza kufurahia bidhaa zetu janja za kisasa.
Na nyongeza, sio lazima kupitia hatua ndefu ya kubonyeza vitufe ili uweze kuweka mipangilio ya mazingira ya nyumbani kwako unayoyapendelea. Kwa kutumia utendaji kazi bora wa 10-Function AIR Energy Servant, unaweza kuweka mazingira bora unayopendelea ndani ya sekunde chache tu. Pia inatoa ulinzi; inaweza kugundua mwendo, moto na kupiga kengere pale ambapo mlango au dirisha litafunguliwa.
Kifurushi hichi kinapatikana kwa bei ndogo kabisa na kinaweza kuendana na aina yoyote ya maisha yako. Utashangazwa na idadi ya mambo yanayoweza kufanywa na kifaa hiki kimoja tu cha kisasa.
ACM 3Z: Kifaa hichi cha kisasa kinaweza kuunganishwa na kihisio cha kuvuja kwa maji, moshi na zaidi ili uweze kupewa taarifa pale tatizo lolote linapotokea bila kujalisha upo wapi. Kwa sababu utapewa taarifa mara moja, unaweza kuchukua hatua hapo hapo. Hakuna tena kuharibika kwa sakafu yako, na utaweza kuokoa viti na meza zako.
Vifaa hivi vimetengenezwa vikiwa na WiFi ndani yake na vinaweza kuunga moja kwa moja na TIS server. Hii inamaanisha ya kwamba unaweza kuangalia nyumba yako hata muda unapokuwa haupo. Pia, unaweza kutumia saa ili kuweka mipangilio katika ACM modules ili ziweze kufanya kazi Fulani katika muda Fulani. Kwa mfano, kama unapenda kuoga maji ya moto kila siku asubuhi kabla ya kwenda kazini, unaweza kuiwekea maelezo ACM module ili iweze kuandaa maji ya moto kwa ajili yako kila inapofika saa 1 asubuhi.
Pia zinaweza kukupatia kumbukumbu zako za matumizi yako ya umeme kwa mwezi na kwa mwaka. Hii inakusaidia kuona ni kiasi gani cha umeme unachotumia ili uweze kufanya mabadiliko ya matumizi kama itahitajika.
TIS ni kampuni kwa ajili ya nyumba yako ya kisasa kwa ajili ya utendaji kazi bora wa vifaa vyako vya umeme na pia kukuletea teknolojia ya kisasa kabisa itakayoendana na muonekano wa nyumba yoyote.
Usikose Mleta-Barua
Suluhisho hili ni kwa ajili ya mtu yeyote anayetaka kuboresha ulinzi katika jengo lake na kifaa cha gharama nafuu. Aina hii ya ulinzi inakuwezesha kusimamia mlango wa kuingilia pamoja na uwezo wa kuthibitisha mgeni kwa sauti na kwa kumuangalia ni teknolojia pendwa kwa wasimamizi wa jengo.
TIS-AP-CDTO-18 ni Simu yenye Video ya Mlangoni ya IP ya kijanja yenye sifa nyingi maalumu kwa ajili ya kuboresha ulinzi wa jengo lako na kukusaidia kutazama mlango au geti la kuingilia.
Kifaa hiki janja cha mawasiliano ya video kina paneli ya aluminium na kioo cha kugusa cha IPS LCD cha ukubwa wa 7” na kinaonyesha picha halisi ya eneo lako la kuingilia ndani. Uniti hii ina kamera zenye resolution kubwa na uwezo wa kuongeza mwanga yenyewe, hivyo picha siku zote zinaonekana vizuri.
Simu hii inayokaa mlangoni ina kifaa cha kusomea kadi na kihisio cha IR (IR sensor), hii inatoa uwezo wa kuingia na kutoka katika nyumba za kupanga kirahisi na kuingia ndani kwa kutumia uso (face detection) na/au pin code zitakazotumiwa kwa kupitia WiFi.
Kifa hiki suluhishi, ambacho kina relay 3, kinaweza kufungwa kwenye ukuta, na kwa sababu hakipitishi maji/vumbi, kitakaa popote utakapokifunga.
Pia ni muhimu kuelezea kwamba kufanya kazi na panel hii ya nje ni rahisi sana; teknolojia ya kiwango kikubwa ya TIS-AP-CDTO-18 inawawezesha watumiaji kuhifadhi namba za simu za kila unit, na sehemu ya kupiga simu imewekwa ili kila mtu awe huru kufanya kazi na kifaa hiki cha mawasiliano cha mlangoni.
Mfumo wa TIS-AP-CDTO-18 pia unakupa sifa kadhaa za sauti, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kukata mwangwi, kuweza kuwasha kwa kutumia sauti, na kutengeneza sauti za kupumzisha.
Kifaa hiki cha mlangoni kina ubora wa picha mkubwa pia. Kamera zake zina ubora wa picha wa mpaka kufikia 1080p na LED kali kwa ajili ya kumulika picha nyakati za giza.
Tumia sehemu ya kupunguza au kuongeza sauti, rekebisha kipaza sauti unavyotaka pamoja na urefu wa maongezi ya simu na upokee taarifa kunapokuwa na dharura popote ulipo duniani. Tazama sehemu ya kuingilia katika eneo lako kupitia simu yako ya mkononi, na utapewa taarifa kukiwa na jaribio lolote la kuvunja.
Unaweza kutumia kifaa hiki cha mawasiliano kwa ajili ya taarifa za biashara na kutoa ujumbe wa kukaribisha wageni pia. Pia, kinaweza hata kufungwa kama simu ya mlangoni katika ofisi ili kuboresha BMS ndani ya jingo lako.
Unastahili kupumzisha akili na kurahisisha maisha yako kwa kuyafanya yaende vile unavyotaka wewe, na tunajitahidi kukusaidia ufanikiwe kwa hilo.
Kuwa Mjanja
Je, unatafuta mfumo wenye ulinzi wa kiwango cha juu utakaokuhakikishia unaangalia eneo la kuingilia ndani? TIS automation inakupa suluhisho la kijanja kwa ajili ya kuwathibitisha wageni wako kwa sauti na kwa sura; TIS-OUT1-Villa-18 ni simu ya mlangoni yenye sifa nyingi bora zinazoendana na mfumo wako wa kidigitali katika jengo la ofisini na katika nyumba za kupanga yani apartment/flat.
Kifaa hiki suluhisho kimetengenezwa kwa zinc alloy na kinaweza kufungwa katika sehemu yoyote duniani kwa sababu hakipitishi maji na vumbi. Kina kitufe kimoja cha kupiga simu na sehemu ya kusoma kadi (RF card reader) kwa ajili ya kusimamia watu wanaoingia ndani vizuri.
Funga TIS-OUT1-18 na ufurahie kiwango kikubwa cha urahisi utakaokuwa umeletwa na namna teknolojia yetu janja inavyofanya kazi; simu hii ya video ya mlangoni inaweza kufanya kazi na G-sensor na hivyo kukupa ulinzi wa juu zaidi pamoja na urahisi katika kusimamia wanaoingia ndani. Kitufe cha kutoka ni moja ya faida ya TIS-OUT1-18; inafunga mlango na hakuna mtu anayeweza kutoka nje ya jingo bila kuwa na ruhusa yako.
Kifaa hiki janja kina SIP na kinarekebisha mwanga mweupe chenyewe. Pia kina relay za output 2 ambazo zinaweza kupangiliwa na milango yoyote miwili. Kwa mfano, unaweza kutaka kufunga kifaa hiki katika geti kuu na katika mlango wa kuingia ndani ya jingo.
Kamera yake ya 3M inaweza kubadilisha mwanga yenyewe na kuhamisha picha kubwa ili uweze kufaidi picha pana la eneo la kuingilia ndani ya jingo lako. Hata hivyo, pia inaweza kukata mwangwi ndani ya TIS-OUT1-18, hivyo utaweza kufurahia simu za kibiashara kama ikitokea kuna simu zaidi ya moja.
Wezesha uwezo wa kugundua sauti na uruhusu kujiongezea mwanga wa picha moja kwa moja ili uweze kumtambua mgeni vizuri. Simu yetu ya video ya mlangoni inawasha uwezo wa kuona usiku moja kwa moja giza linapoingia ili kusudi pamoja na taa zake la LED zinazomulika mlangoni mwako paendelee kung’ara kama almasi.
Kumbuka unaweza kutumia kupitia simu yako ya mkononi kama ukiwa mbali na ukitaka kumfungulia mgeni mlango.
Matamanio ya kutengeneza vifaa suluhishi vya kijanja kwa ajili yako yanaamsha ubunifu wetu na ndiyo kitu kinachosukuma wataalamu wetu kutengeneza bidhaa bora za kiteknolojia zinazoweza kufanya kazi muhimu na kuwa na muonekano wa kuvutia.
Kamwe Sio Mbali na Wewe
Katika dunia ya kisasa, dunia ambayo maarifa ya kidigitali ni ufunguo katika kushinda mbio za teknolojia, umuhimu wa kutoa vifaa muhimu vinavyoweza kubadilika kulingana na matumizi ni mkubwa hauna kipimo.
Kifaa kilichotengenezwa upya cha TIS-AP-CDM-18 ni kifaa cha mawasiliano cha video kilichofungwa na mfumo wa SIP na kifaa cha kusomea kadi (RF card reader) kinachokupa ubora mkubwa wa sauti na video na kukuwezesha kuangalia eneo lako la kuingilia ndani mubashara.
Simu hii ya kukaa mlangoni, ambayo ina panel ya aluminum isiyopitisha maji na vitufe vya namba, inaweza kufungwa katika eneo lolote; sio hayo tu lakini pia kuna toleo lingine la kifaa hiki kisichodhuriwa na baridi kinapatikana kwa maeneo yenye baridi kali.
Lakini kazi kubwa zaidi ya kifaa hiki janja ni kumpa mtumiaji uwezo wa kusimamia watu wanaoingia ndani ya eneo kutaka kuongea au kuona wageni wao; Ni kama vile unakuwa siku zote haupo mbali na nyumbani. Tunalenga kuwapa wateja wetu ulinzi ulioboreshwa na amani. Haijalishi upo wapi, simu hii ya mlangoni inakurahisishia kuona nani yuko mlangoni.
Zaidi, simu hii ya mlangoni ina kamera ya 3M-pixel, uwezo wa kumulika yenyewe, na G-sensor kwa ajili ya kutoa king’ora inapojaribu kufunguliwa (tamper alarm), na hivyo kufanya bidhaa hii kuwa suluhisho la kipekee la kidigitali kwa miradi yako ya kujiendesha nyumbani. King’ora cha kufunguliwa (tamper alarm) cha TIS-AP-CDM-18 kimewezeshwa iwapo ikitokea mwizi akijaribu kuingia ndani ya nyumba yako wakati mfumo umewashwa. Kama mtu akijaribu kuuzima mfumo kwa kuuchomoa au kutoa betri ya ziada, king’ora (tamper alarm) kitawashwa.
Kifaa hiki kina relay za output 3 na sifa za sauti ya ubora wa juu kadhaa, kama vile kipaza sauti cha ndani, spika ya 2W, uwezo wa kugundua sauti, kutuma sauti yenye ubora mkubwa.
Lakini sio hayo tu; sifa zote za video za TIS-AP-CDM-18 ni za kipekee, pia. Kamera yenye uwezo wa 720p na uwezo wa kuona usiku na kihisio cha ndani cha mwanga kwa ajili ya kumulika picha wakati wa usiku ni baadhi tu ya sifa mbalimbali ambazo watu wanaopenda teknolojia janja wanaweza kuzifurahia.
Suluhisho hili linafaa kutumika kama simu katika mlango wa ofisini na kifaa cha mawasiliano katika mlango wa apartment/flat zenye mlango wa kudhibiti watu.
Ona Mbali na Upeo wa Macho Yako
Je, umepishana na mgeni au imebidi ubadilishe ratiba yako pale unapokuwa ukimsubiri mgeni inaweza kuwa inakera sana vyote hivi vinapotokea. Ni sawa pia pale unapokuwa nyuma ya nyumba ukipika alafu mtu akagonga hodi; inawezekana usisikie kengele ya mlangoni ikilia, au unakuwa umetingwa na kazi ya kupika ukashindwa kwenda. Kampuni ya TIS Smart Home imekuja hapa kukuletea WIFI Door Bell—bidhaa mpya kukuwezesha wewe kutumia simu yako ili kuepuka matatizo yote haya yaliyotajwa.
Kifaa hiki cha video kupitia WiFi kinafungwa nje ya mlango wako wa kuingilia ndani na hakihitaji panel yoyote ndani ya nyumba. Badala ya panel ya ndani, video na mawasiliano katika kifaa vinapatikana kwako katika simu yako ya mkononi. Hiyo ni sahihi. Kwa kutumia simu yako, unaweza kuona ni nani yuko mlangoni, kuongea na wageni, na hata kufungua mlango kama ikihitajika.
Kufunga na kuweka mipangilio yake ni rahisi sana. Vyote hivi vinaweza kufanyika bila kuhitaji findi wala mtu anayejua kutengeneza programu; unaweza kukamilisha kila kitu wewe mwenyewe.
Kama ilivyo kwa vifaa vingine vya AIR, kifaa hiki kimewekewa WiFi ambayo inaunga moja kwa moja katika intaneti na katika kompyuta za TIS (TIS server). Hii inakuruhusu wewe kupokea wageni hata pale unapokuwa mbali. Ongeza tu programu ya TIS katika simu yako na utapewa taarifa muda wowote mtu akija mlangoni kwako—hata kama simu yako imezimwa.
Inawezekana pia kutumika na kengele za RF za aina nyingine, hivyo hata kama hakuna intaneti au betri yako imeisha, kengele ya WIFI Door Bell inakujulisha kuwa kuna mgeni.
Je, una sherehe ya kushtukiza katika siku ya kuzaliwa kutoka kwa rafiki yako? Hautaikosa. Kifaa hiki cha kuwasiliana kinaweza kuunganishwa na idadi yoyote ya simu za mkononi. Kufanya hivi, kama mtu akikuletea barua nyumbani na haupo, inawezekana pia zikapokelewa.
WIFI Door Bell ni mlinzi wako wa kisasa. Ni boresho katika mfumo wako wa ulinzi wa mali zako, na kihisio chake cha mwendo kina ubora na kitakujulisha kama kukiwa na aina yoyote ya mwendo. Unaweza kuzuia kuvamiwa ndani pia kwa kupokea hodi inapopigwa au kufanya mawasiliano ya haraka kwa mtu unayemfahamu ambaye yupo karibu.
Zaidi ya yote, kengele hii ya mlangoni inakupa picha nzuri ya mbele ya nyumba yako masaa 24 siku 7 za wiki. Muda wowote ukiwa unajiuliza ni nini kinaendelea nje ya nyumba yako, tumia kamera yake ya kiwango kikubwa na yenye uwezo wa kuona usiku pia.
Bidhaa hii ya kisasa, ambayo kwa sasa inapatikana katika rangi ya fedha, imetengenezwa na muonekano wa kifahari na ina mng’ao laini huku kikiwa kimekaa pembeni ya mali yako.
Uvumbuzi wa kiteknolojia kutoka TIS unalenga katika kufanya maisha yako yawe ya furaha na rahisi. Ukiwa na WIFI Door Bell unaweza kukutana na wageni wako kutoka eneo lolote la dunia na siku zote ukajisikia uko nyumbani. Hakika unastahili.
Kutana na Superman wa Vifaa janja vya kisasa
Kama vifaa vyako janja vimeunganishwa na nyaya kiasi au vinafanya kazi bila kutumia waya kwa kiasi fulani, usijali kuhusu hilo. Kampuni ya TIS Smart Home ipo hapa kuhakikisha haubanwi na mifumo ya aina yoyote. Furahia uwepo wa teknolojia ya kisasa itakayokurahisishia maisha yako. AIR-BUS Converter, sasa inapatikana kwa ajili ya kutumika kwa vifaa vinavyotumia waya na visivyotumia waya, hakika itaongeza thamani katika biashara yako.
Kiunganishi hiki kitakuwa ni kama daraja kuunganisha vifaa vyako vinavyotumia waya na vile visivyotumia waya. Hii inamaanisha ya kwamba kama una panel ukutani iliyofungwa na nyaya na pia una air ceiling sensor, vinaweza kuunganishwa na kuendeshwa kwa pamoja. Unapokuwa uko njiani kuelekea nyumbani, washa AC, ongeza mwanga wa sebuleni kwako, washa microwave oven ili kupasha chakula chako. Vyote hivi vinawezekana kwa kugusa kidogo tu na vidole vyako.
Air Bus ni mini converter ambayo inaboresha nyumba yako mara moja. Unachohitaji kufanya tu ni kufunga kifaa hiki pembeni ya au nyuma ya kifaa cha waya (wired module) na kisha weka mipangilio kwa ndani yake kwa kutumia app ya simu yako.
Suluhisho hili linaweza kutumika kuunganisha vifaa vya waya kwenye WiFi au kukuwezesha kutumia rimoti ili kuendesha au kubadilisha baadhi ya bidhaa zetu (Luna, Mars, Terre series) na kuwa WiFi Air panels. Kwa mgano, kuongeza itifaki za WiFi (WiFi protocol) ndani ya panel ya Luna TFT ndani ya ofisi yako inakuwezesha kuendesha kwa kutumia rimoti, hivyo unaweza kutumia panel ya Luna kuwasha kiyoyozi kikuu kwa kutumia simu yako ya mkononi. Air Bus Converter pia inaweza kutumika kama nyongeza katika panel zote za ukutani bila kuhitaji zile za zamani.
Air Bus converter inaweza kuja pamoja au bila power supply. TIS Air-Bus haitoi umeme kwa ajili ya vifaa vyako, lakini kama ukifunga TIS Air-Bus-3W, inaweza kutoa umeme kwa ajili ya kifaa. Hii inamaanisha kwamba kifaa kilichofungwa kinachotumia nyaya, kama vile Luna 9G panel, kinaweza kufanya kazi hata bila kufungwa na nyaya.
Nyongeza, kifaa hiki kina logics zaidi ya moja kwa ajili ya kuelezea utendaji kazi wa kifaa hiki cha kisasa, na kinakifaa kinachotumika kuweka ratiba ambacho kinakuwezesha kufanya ubora wa utendaji kazi wa vifaa vyote uende sawa. Air-Bus Converter kiujumla ni kama vile mwamvuli kwa ajili ya TIS IP Port na TIS Automation Timer; japokuwa ni kifaa kidogo, kinabeba uwezo wa kufanya kazi zao zote.
Kama vile unavyoweza kuona, Air Bus Converter ni supermana wa vifaa vya kujiendesha vyenyewe kikiwa na utendaji kazi wa kiwango cha juu na kinafanya uendeshaji wa vifaa vya aina yote kuwa rahisi kama kula keki. Jaribu leo.
Gateway ya Teknolojia
TIS inakuletea bidhaa ambazo sio tu kwamba zitazidi mahitaji yako yote, lakini pia zitasimama juu ya bidhaa zingine zote kwa sababu ya kazi nyingi ambazo vifaa vyetu vinazifanya. Kwa mfano, IP-Com_Port ni module kwa ajili ya kufanyia mawasiliano iliyotengenezwa kwa ajili ya kuunganisha mtandao wa BUS na kutengeneza ulimwengu wa kijanja unaokupa nafasi nyingi za kuchagua.
Inafaa haswa miradi mikubwa, TIS’s IP-Com_Port inaunganisha na kushirikisha vifaa vyako vyote janja na kuvifanya kuwa rahisi kuvisimamia. Mpangilio wa nyaya katika TIS-BUS unabeba hadi vifaa 64 kwa kila waya. Katika miradi ambayo ina vifaa vingi sana, port ya IP inaweza kuongezwa katika kila mtandao ili kufanya kila kitu kiweze kuwa kimeunganishwa kwa pamoja. Ukitumia module za IP na nyaya za Ethernet, kusimamia mfumo wa mwanga, hali ya hewa, na mfumo wa ulinzi katika ghorofa kubwa inakuwa ni jambo rahisi kulifanya.
Pia, module hii inaunganisha mtandao wa BUS kwenye wireless gateway, na kukuwezesha kusimamia nyumba yako hata kipindi unapokuwa mbali na nyumbani. Hakuna haja ya kuongeza dongles au adapters. Unachotakiwa tu kufanya ni kuweka app ya TIS katika simu yako janja, na kisha utazame nyumbani/kazini kwako popote utakapokuwa.
Kama unataka kuunganisha bidhaa tofauti za makampuni tofauti, IP-Com-Port ndiyo kitu unachokihitaji. Kuunganisha na vifaa vya watengenezaji wengine inawezekana pia. Unaweza kuunganisha makufuli yote ya umeme, Mifumo ya viyoyozi ya VRV, na zaidi kwenye module hii na kisha ukatengeneza muundo wako binafsi wa vifaa vilivyounganishwa kirahisi. Kwa njia hii, kama mlango ukifunguliwa sehemu Fulani, taa inakuwa inawaka ndani ya chumba kitupu, au unakuwa na kiyoyozi kikifanya kazi kwa nguvu, unachohitaji tu ni simu yako ili uweze kuendesha kila kifaa.
Mwisho, kifaa hichi kina sehemu mbili za kuunganisha: RS232 na RS485. Kimewekewa ASCII pamoja na Hexadecimal python katika baud rate yeyote. Hii inamaanisha kiasi cha data kisicho na kiwango kinaweza kutumwa na kusomwa kwa kila sekunde, hivyo unaweza kutoa amri kwa vifaa vingi kwa kadri unavyotaka, na zote zitafanyika bila muingiliano wowote.
Ifunge, na uunganishe kila kitu. Furahia ulimwengu bora wa kisasa na TIS IP-Com-Port.
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Inakuja hivi karibuni…
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha