Tuwe Wajanja

Tunapoelekea katika Mageuzi ya Tatu ya Kijani, matumizi ya taarifa na teknolojia za kisasa katika kilimo ni muhimu sana. Ulimaji wa Kijanja (Smart Farming) unamaanisha kusimamia maji, mwanga, unyevu, na joto kwa lengo la kukuza wingi na ubora wa mavuno.

Vihisio(sensor) na vitendaji(atuators) kutoka TIS vinaweza kufungwa shambani ili kuzalisha zaidi na kutoa mavuno bora katika kilimo.

Kujisimamia katika kilimo na matumizi ya roboti kunalifanya shamba kuwa janja. Kufunga maroboti, mifumo ya kujisimamia yenyewe pamoja na mbinu mbalimbali za artificial intelligence kunaokoa muda wa muhimu unaopotea katika kufanya kazi za kujirudia rudia, kama vile kutazama maji mara kwa mara au kwenda wewe mwenyewe shambani ili kuwasha na kuzima taa moja moja.

farm

Kuna panel za kijanja zinazosaidia kusimamia pampu na taa, na matokeo yake kumuokolea mkulima pesa nyingi. Jambo zuri zaidi ni kwamba kutumia teknolojia hizi ni rahisi sana, na mtu yoyote mwenye simu ya mkononi au tablet anaweza kuvitumia.

Haijalishi una shughuli za shamba kubwa au shamba dogo tu mfano la uyoga la familia, Smart Farm inaweza kuwa msaada mkubwa katika masuala ya mazingira. Mfano, inawezesha matumizi fanisi zaidi ya maji na kurekebisha kiwango sahihi cha joto na unyevu katika mazingira yanayosimamiwa. TIS smart automation inakupa mifumo suluhishi mbalimbali ya kijanja itakayokusaidia kuendesha kilimo kulingana na michanganua ya taarifa (data-driven and data-enabled processes).

switch

Pia, unaweza kupanga maamuzi ya kuchukuliwa na taratibu ili tendo flani lifanyike moja kwa moja kunapokuwa na hali fulani. Hii inaweza kutumika kutuma taarifa katika simu ya mtumiaji kama kuna baridi kali au ardhi imekauka kwa siku kadhaa.

Na nyongeza ni kwamba, teknolojia janja inakupa usimamizi mkubwa zaidi katika usimamiaji wa umwagiliziaji kwa kujisimamia moja kwa moja na kumwagilia yenyewe katika muda fulani wa siku ambapo joto ni sahihi. Usimamiaji wa umwagiliaji wa kijanja (smart sprinkler control) pia unapunguza sana upotezaji wa nishati, kwa sababu inasitisha yenyewe wakati wa kipindi cha mvua.

Kwa kipindi cha muda mrefu, hatua hii ni muhimu katika kupunguza gharama na kufanya biashara ziwe fanisi zaidi katika matumizi ya nishati.

tree

Zaidi ya hayo, kutegemea na aina ya mazao unayolima, kiwango cha joto na unyevu vinaweza kuwa ni muhimu sana. Ni jambo la busara kufikiria katika kuchukua vifaa vya usimamizi wa unyevu, haswa kwa kuwa baadhi ya mazao yana utegemezi mkubwa katika joto na ubora wake unategemea unyevu. TIS smart technology inakusaidia kurekebisha mazingira ya joto katika maeneo tofauti ya shamba. Hivi ni vihisio vya kijanja vya joto vyenye ubora na utendaji wa hali ya juu ili kuhakikisha usalama katika biashara yako.

Sasa ni muda wa kuweka imani katika teknolojia na kuruhusu mashine zikusaidia katika kilimo.

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK