Sote tunaweza kuona kasi iliyopo katika kuunganisha teknolojia katika kila nyanja ya maisha yetu ya kila siku.
Kwa uwepo wa teknolojia na muunganiko wa vifaa vya TIS vinavyotumika kila kona, kuna vifaa suluhisho vingi vya kidigitali kwa ajili ya kusimamia maji, umeme, na matumizi ya nishati kwa ufanisi.
Lakini je, mji wa kijanja ni nini? Ndani ya mji wa kijanja, taarifa zinapokelewa katika kifaa kimoja katika sehemu moja na kuwasilishwa kwenye kifaa kingine kilichopo mbali na pia kwa mtumiaji ili kumuwezesha kuchukua hatua stahiki na pia vifaa vyote vinaweza kubadilishwa mipangilio. Kutumia teknolojia kuboresha maisha ya watu ni kipaumbele ndani ya mji wa kijanja, na TIS inatizamia kupiga hatua mbele zaidi ya yeyote katika safari hii.
Ndani ya mji wa kijanja, watu wanatumia Intaneti kukata tiketi; wanaweza kuwa wamekaa katika mgahawa wakinywa kahawa huku wakiwa wanaangalia chumba cha hoteli kwa kupitia simu ya mkononi, au wanaweza kuwa wanatembelea mtandao na kufanya manunuzi mtandaoni muda ambao wakapokea ujumbe mfupi wenye bili yao ya umeme. Popote ulipo, programu ya simu ya bure kutoka TIS ipo hapa kukurahisishia zaidi maidsha.
Kuwa na ndoto ya mji ambao hakuna bili inayochapishwa kwenye makaratasi na watu wote pamoja na serikali wanaweka nguvu katika kutunza nishati. Katika mji huu, kila nyumba inakuwa ni ya kidigitali, na Vitengo vya Nishati katika sekta mbalimbali vina uwezo wa kupata taarifa za mtumiaji wake ili kuwa na ufanisi katika sera za matumizi na pia kuchukua hatua mambo yanapokuwa sio kama yalivyotarajiwa.
Katika mji wa kijanja, majengo yanalindwa kwa usalama kutoka katika kituo kimoja cha kati kinachotazama na kuchanganua matumizi ya nishati ya kila sehemu. Nyongeza, kwa kutumia ‘logics’ na ‘timers’ za kijanja, mameneja wa majengo watakuwa na uhakika kwamb majengo yanasimamiwa kwa usalama. Kifaa cha kijanja cha ulinzi na vihisio kutoka TIS vinatoa taarifa kwa wanausalama na meneja juu ya jambo lolote hatarishi au moshi uliogundulika au maji yanayovuja katika nyumba.
Miji ya kijanja inapunguza upotevu wa nishati kwa kiwango kikubwa. TIS technology inakupa module janja ya Weather Station pamoja na vifaa vilivyofungwa lux-meter ili kila mtumiaji aweze kuweka mipangilio yake katika mifumo ya maji na umeme ili kuwa na ufanisi mkubwa na kifaa kiweze kuwashwa tu pale kinapohitajika.
Katika mji wa kijanja, kila mtu ana haki ya kufurahia uzuri na urahisi ulioletwa na teknolojia. Bidhaa zetu kutoka TIS ni rahisi sana kuvitumia (vifaa vimetengenezwa kwa viwango vya DIY) na kwa bajeti ndogo.
Lakini je, nadhalia hii ya mji wa kijanja ina uhusiano gani na ongezeko la idadi ya watu katika maeneo mbalimbali ya mijini? TIS technologu inakupa fursa ya kuokoa gharama na kukuza ufanisi uliopo katika mali uliyonayo; hivyo basi, inasaidia katika kusimamia maeneo ya watu wengi na kuokoa pesa nyingi sana kwa serikali. Hiyo ndiyo tafsiri halisi ya kusimamia.
Uchafuzi wa hali ya hewa, afya, na masuala mengine ya usalama yanaendeshwa vizuri zaidi kwa msaada wa vihisio vyetu janja (smart sensors) pamoja na vifaa vingine vya kidigitali. Kama kila nyumba ndani ya mji ikiweza kujisimamia moja kwa moja, nishati kidogo itapotea na utoaji wa gesi za greenhouse kutapungua.
Inapendekezwa kwamba serikali zifikirie teknolojia za IoT kama wanapanga kupiga hatua mbele na kujenga jamii ya watu wanaojitegemea na nzuri kwa binadamu.
We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha