Maboresho katika teknolojia ya IoT yametengeneza fursa nyingi za kuwezesha kukidhi mahitaji ya wateja na kuongeza faida zaidi katika sekta ya biashara ya reja reja. IoT imewezesha pia kusaidia kuepukana na ugumu katika kusimamia vituo vya maduka, kwa kuwa BMS ni moja ya matokeo ya itifaki ya kijanja.
Wamiliki wa Mall/maduka wanaweza kufunga vihisio vya kijanja ili kuweza kutazama na kusimamia usalama. Kamera zenye picha za ubora wa juu zinatoa picha halisi ya umati wa watu katika eneo, ambazo zinaweza kutumika kutoa tathmini kamili ya maeneo yanayojaa watu. Data hizi zinaweza kutumika katika kufunga vyema mfumo wa kiyoyozi, na ule wa taa. Kwa mfano, taa zinaweza kufanywa ziwake kwa mwaga mkali katika maeneo ya kuingilia, kutokea, na katika njia za kupita ambazo zinapitiwa na watu wengi. Vihisio hivi mara nyingi vinakuwa na uwezo wa kuhisi mwendo na kuviwezesha kufanya kazi tu kama kuna uwepo wa watu na hivyo kuokoa umeme.
Kuna suluhisho za aina nyingine zinazoweza kugundua moshi na/au kuvuja kwa maji, jambo ambalo linaweza kuwa na umuhimu mkubwa katika kituo chabiashara na kuepusha hasara katika sekta ya biashara hizi za reja reja. Lakini sehemu ya muhimu zaidi katika ufanyaji kazi wa itifaki ya kijanja inawezekana ikawa ni mfumo wa kengele ulioboreshwa ambao unasimamia kengele zote za moto, na kama ikitokea kuna moto, milango ya kutokea itafunguka yenyewe moja kwa moja na taa zitawaka kwa ajili ya kuwezesha uokoaji wa dharura. Zaidi ya hayo, gesi zitafungwa na mifumo ya viyoyozi itazimwa ili moshi usisambae zaidi.
Moja ya jambo la muhimu zaidi katika mtandao wa kijanja ni kutumia maji kwa ufanisi ndani ya jumba kubwa. Pampu na vyanzo vya maji vinabaki kama vilivyo, ili kuweza kusaidia kusimamia mifumo ya kupooza/kuchemsha na pia kuepuka kupoteza maji kwa kiwango kikubwa.
Zaidi ya hayo, kutumia thermostat za kijanja kunakusaidia kusimamia hali ya hewa ya ndani kwa namna iliyo fanisi zaidi. Joto la kila duka linaweza kubadilishwa kwa kulingana na ukubwa wake. Pia, joto la maeneo ya baridi m.f maeneo ambayo yana idadi ndogo ya watu – linaweza kupunguzwa huku ukiwa katika kituo kingine kabisa.
Mall na vituo vya biashara vinaweza kujiendesha na kuwa salama kwa kutumia sumaku za mlangoni za kijanja, saa, na vifaa vingine vya logic vingi.
Spika za kijanja na skrini zinaweza kutumika kuvutia wateja na kutangaza chapa au bidhaa fulani. Sababu mwisho wa siku, ubunifu ndio utaleta tofauti kubwa.
Haijalishi kama mtu atakuwa na hofu juu ya madhara ambayo biashara yake inaweza kuleta katika mazingira au tu anataka kukata gharama kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo, ni muhimu sana kuwa na kumbukumbu ya matumizi ya umeme katika mradi.
Mwisho wa siku, vitu hivi vinafungua njia inayowezesha kukidhi mahitaji yote ya mteja na faida kubwa zaidi. Teknolojia inaweza kumsaidia mmiliki wa biashara kumridhisha mteja na kupunguza gharama zake pia.
We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha