Nyumba yenye Afya na Uendeshaji wa TIS

Baadhi ya watu wanaamini ya kwamba kukaa ndani nyumbani kuna matokeo bora zaidi kiafya kuliko kutoka nje katika miji mikubwa iliyojaa uchafuzi, lakini jambo hili sio kweli muda wote. Hewa ya ndani ya nyumba mara nyingine inaweza kuwa na athari hiyo pia kutokana na kushuka kwa ubora unaosababishwa na kemikali zenye madhara. Hii ni kwasababu maeneo yaliyofungwa yanasababisha kemikali zenye madhara kama vile carbon monoxide na Volatile Organic Compounds(VOCs), kukua zaidi ukilinganisha na maeneo yaliyo wazi.

VOC ni gesi inayozalishwa na vitu vingi vinavyopatikana ndani ya nyumba, na inapatikana kwa wingi zaidi ndani ya nyumba zaidi ya nje kwenye maeneo yaliyo wazi. Gesi hii inamchanganyiko wa kemikali ambazo zinaweza kusababisha muwasho katika macho, pua na koo, kukosa hewa, kichwa kuuma, viungo kukakamaa, kichefuchefu, kujisikia kuumwa, na matatizo ya ngozi. Kama hali ikiwa mbaya zaidi, maumivu katika mapafu, matatizo katika ini na figo au kuwa na matatizo katika mfumo mkuu wa fahamu.

Inahisiwa ya kwamba baadhi ya gesi za VOCs husababisha kansa. Madhara ya kiafya ya VOCs yanategemea na wingi wake na kwamba mtu amevuta kemikali hizi kwa muda mrefu kiasi gani.

Uchafu ndani ya nyumba na vitu vinavyochafua hali ya hewa mara nyingi vinazalishwa na vyanzo vinavyopatikana katika mazingira yetu, kaa vile moshi wa tumbaku, vifaa vya kujengea majengo, fanisi, vifaa vya kufanyia usafi, na viondoa harufu, au baadhi ya vifaa vya umeme kama vile kompyuta, printers, na vitu vingine vingi vya ndani ya nyumba kama vile microwaves na ovens. Binadamu wanaweza kuzalisha VOCs pia.

Joto la ndani ya nyumba na unyevu pia vina nafasi kubwa katika matatizo ya ngozi kwa mtoto mchanga, mafua, ukuaji wa fangasi, na vifo vya ngafla kwa watoto wachanga (SIDS), au kwa jina linguine cot death.

Joto kali sana ndani ya chumba pia linaongeza hatari ya SIDS kwa watoto wenye mwezi 1-12. Wataalamu wengi wanapendekeza kwamba chumba cha mtoto kibakie katika nyuzi joto 68–72°F (20–22°C).

Mtoto akiwa amelala katika chumba salama chenye vifaa vya kujiendesha vya TIS

Unyevu ukizidi pia unakuwa na athari kiafya. Unaweza kusababisha pua kutokwa na makamasi na kutengeneza mazingira mazuri kwa ukuaji wa fangasi au utitiri, ambao wanaweza kusababisha aleji. Madaktari wanapendekeza unyevunyevu katika chumba cha mtoto ubaki katika kiwango cha kati ya 50 na 70%.

Zaidi, baadhi ya tafiti zinaeleza kwamba kirusi cha homa ya mafua kinakuwa katika imara katika maeneo yenye ubaridi na kavu na kwamba ukuta wa kirusi unakuwa mgumu pale kunapokuwa na baridi sana, na kuwafanya kuwa na hatari zaidi, na rahisi kuambukizwa wakati wa baridi kali. Hata hivyo, hali ya hewa ya baridi kali sio jambo pekee linalosababisha magonjwa; mabadiliko ya ghafla ya joto pia yanaweza kusababisha uwezo wa mwili wa binadamu kupambana na magonjwa kupungua.

Tatizo lingine ni fangasi(mold). Aina hii ya fangasi inaweza kuathiri afya ya mwili na vitu vinavyotuzunguka, jambo linaloweza kusababisha aleji, asthma na matatizo mengine katika mfumo wa upumuaji. Baadhi ya watu wana aleji na aina hii ya fangasi, lakini pia ijulikane wanaweza kusababisha kuwashwa kwa macho, ngozi na mapafu bila kujali una aleji au hauna.

Fangasi hawa wanaweza pia kuharibu fanisi na baadhi ya vifaa vya ndani ya nyumba. Changamoto kubwa ni kwamba wanaweza “kujificha” ndani ya ukuta na chini ya zulia. Fangasi hawa wanahitaji vitu vinne ili kukua: spora(mold spores), chakula cha fangasi, joto linalofaa, na unyevu. Spora wa fangasi wako kila sehemu ndani ya nyumba na nje katika mazingira yanayotuzunguka, na fangasi hawa wanaweza kula karibu kila kitu, hivyo sio suala lahisi kuondoa spora au chakula cha fangasi hawa.

Linda nyumba yako isipatwe na kawa(mold) - Anti Mold sensor – nyumba inayojiendesha

Fangasi wanakua vyema katika kiwango cha joto ambalo tunapendelea kuwa nacho takribani nyuzi joto 60-80°F (16-27°C). Pale hewa yenye joto, na unyevu inapogusana na uso wa sehemu iliyo ya baridi inatengeneza umande (hewa ya baridi haiwezi kushikilia unyevu mwingi), umande huu unatengeneza mazingira yanayofaa kabisa kwa ukuaji wa fangasi hawa. Kwasababu sio jambo linalowezekana kwa urahisi kuzuia fangasi kwa kutumia joto pekee, uangalizi wa unyevu hewani ni jambo la muhimu pia.

Kuzuia ukuaji wa fangasi, Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa wanashauri kuwa katika mazingira ya ndani ya nyumba kuwe na kiwango cha unyevu kisichozidi 50%. Kiwango hiki kinaweza kufikiwa kwa kutumia vifaa kama dehumidifier au kiyoyozi.

Kuna teknolojia nyingi za kuangalia joto na unyevu, na vinatoa onyo kwa sauti kama kiwango cha unyevu au joto kikifikia kiwango Fulani. Vihisio vingi vinavyopatikana katika masoko ya sasa ni vifaa vinavyotumia teknolojia hii.

Kuna vihisio vya viwango vya juu zaidi ambavyo vinaweza pia kuangalia kiwango cha carbon monoxide au VOCs katika hewa.

Vihisio hivi vinaweza kutumika kama vifaa vya kujitegemea au vikatumika kama sehemu ya mfumo mkubwa wa uangalizi. Vina uwezo wa kutuma ujumbe mfupi kumjulisha mtumiaji kama kuna ukuaji wa fangasi au joto kali au kutuma taarifa za viwango vinavyosomwa kila siku.

Wakati bidhaa za IoT zimejikita zaidi katika rimoti, ulinzi, taa na vifaa vya kupunguza mwanga wa taa, mifumo mingine ya kisasa ya uangaliaji wa nyumba vinaenda mbali zaidi na kuhusisha uangalizi na uendeshaji wa kiyoyozi ili kuokoa umeme. Lakini, upande wa kiafya mara nyingi unakuwa unapuuziwa kuangaliwa katika mifumo mingi ya uangalizi wa majumbani kwetu.

Lakini je, kuna teknolojia ambayo inaweza kufanya mambo yote ambayo yameongelewa juu? Je, kuna kifaa kimoja tu ambacho kinaweza kuwajibika na kulinda nyumba yako dhidi ya uchavuzi wa hewa na kutunza joto na kiwango cha unyevu kinachotakiwa na kuweka hewa katika kiwango kilicho safi?

Kampuni ya TIS Smart Home inayo furaha kukufahamisha kuwa hili linawezekana. Kihisio chake cha juu kwenye dari kinachofanya kazi cha —Health Sensor— kina kihisio cha carbon monoxide na VOCs, kihisio cha joto pamoja na unyevu, kihisio cha mwendo, uwezo wa kugundua mwanga, kinasa sauti, 2 digital inputs, na 32 lines of logic and timers. Kifaa hiki ndani yake kina suluhisho kwa kila jambo la muhimu kwa afya na kitakufanya ukae ukiwa na amani.

Kihisio cha TIS cha Afya

Hizi ni baadhi ya sifa za kifaa hiki:

  • 1- Kinahifadhi kiwango cha joto na unyevu katika chumba katika kiwango bora kwa afya ili kuepusha ukuaji wa fangasi wakati ukiwa haupo, na kitakutumia ujumbe mfupi wa kukupa tahadhali katika programu ya TIS maalumu kwa ajili ya simu.
  • 2- Kitaruhusu hewa safi na feni kama kiwango cha gesi za VOC au carbon monoxide katika chumba kitakuwa kikubwa sana, na pia kitatuma ujumbe wa tahadhali kama kikigundua viwango vya hali ya juu vya uchafuzi wa hali ya hewa.
  • 3- Kitaepusha chumba cha mtoto wako kisiwe na joto kali kupita kiasi. Kinahakikisha joto lika katika kiwango kinachofaa, hivyo kuepusha hatari ya ugonjwa wa kifo cha ghafla kwa watoto (SIDS).
  • 4- Kinahakikisha unyevu katika chumba cha mtoto wako unabaki katika kiwango kinachofaa cha 40 – 50% ili kuepusha matatizo ya ngozi kwa mtoto mchanga.
  • 5- Kinasaidia kuepusha mafua kwa kukupa tahadhali kama kuna mabadiliko ya ghafla katika hali ya joto ya chumba. Pia inakutaarifu kama joto likishuka kwa kiwango cha chini sana.
  • 6- Kwa kutumia teknolojia yake ya kipaza sauti, unaweza kumsikiliza mtoto wako au mzazi mwenye umri mkubwa sana. Kama mtoto akilia au mzazi wako akikuita, kihisio ndani yake kitakujulisha kwa kukutumia ujumbe mfupi kwako sebuleni au katika chumba cha mapumziko au kitandani kwako na katika panel ya Luna ya ukutani na kwenye programu iliyopo katika simu yako ya mkononi.
  • 7- Ina 2 digital inputs ambazo zinaweza kuunganishwa na kitufe cha dharura kwa daktari kilichopo pembeni ya kitanda hata taarifa kutoka kwenye vihisio vya pale mtoto atakapojikojolea.
  • 8- Kifaa hiki kinaweza kuingiliana na PIR Motion sensor, ambayo inakuwezesha kuweka kama unataka taa ziwake kama mtoto atakapotembea au kulia wakati kuna giza. Nyongeza, unaweza kukiweka katika hali ya kuokoa ummeme kama chumba kitakuwa hakina mtu kwa zaidi ya masaa 10.
App za kisasa za TIS zinakupa taarifa kama chumba cha mtoto kina joto au baridi sana

Tunajihisi fahari kubwa kuwa moja wa mapainia katika bidhaa za kisasa za uangalizi wa afya ya ndani. Tunaimani ya kwamba wateja wetu wanastahili vitu vilivyo bora, na tunafuraha kuwapatia maisha yenye furaha tele kupitia bidhaa za kisasa zitakazowaweka salama na wenye afya bora.

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK