Uwanja wa Nyuma Ya Nyumba: Oasis Tulivu au Kitovu cha Sherehe

IoT ni kifupi cha Internet of Things, dhana inayokuja na fursa kubwa za kufanya mambo kuwa mazuri zaidi. Fikiria dunia ambayo kila kitu cha kidigitali kimeungana, kuanzia vyombo vyako nyumbani mpaka vifaa vyako kazini.

Kwa kuwezeshwa na IoT, TIS technology inakuwezesha kufanya nyumba yako kuwa ya kidigitali kwa namna iliyo fanisi kushinda zote. Unaposikia neno “smart home”, unapata picha ya mashine ya kutengenezea kahawa inayowaka yenyewe na kuanza kutengeneza kahawa baada ya saa ya asubuhi kupiga kengele ya kuamka, lakini ni kwamba teknolojia imekua zaidi ya hapo.

Siku hizi, soko la bidhaa janja za kiteknolojia linakupa vifaa suluhishi na bidhaa ambazo zinaweza hata kukusaidia kusimamia maeneo yako ya nje. Katika uwanja wako nyumbani wa kijanja, geti la mbele ya nyumba linafunguka lenyewe moja kwa moja punde wanafamilia wanapofika, na unaweza kutazama uwanja wako hata wakati wa usiku kwa kamera zinazoweza kuona usiku. Na vitu vyote hivi vinaweza kufanyika huku ukiwa umelala kitandani ukiwa na simu yako janja.

Mifumo ya ulinzi wa nyumbani imekua kwa kasi sana miaka hii ya karibuni kadri idadi ya kamera mbalimbali za nje inavyoongezeka. Module ya ulinzi ya TIS imetengenezwa kukupatia usalama kwako na kwa wale uwapendao.

solution smart home

Mlango wa gereji wa kijanja kutoka TIS unakurahisia wewe kufikia fyekeo, vifaa vya gadeni, na vingine vilivyohifadhiwa. Unaweza kufungua mlango wa gereji kwa kutumia app ya bure ya TIS katika simu ya mkononi. Vifaa suluhishi hivi pia vinakupa taarifa iwapo mlango wa gereji utakua uliuacha wazi.

Lakini zaidi ya hayo, unaweza kupewa taarifa za mapema juu ya yatakayojiri katika hali ya hewa kwa kutumia Kituo Janja cha Hali ya Hewa kutoka TIS (TIS smart Weather Station). Kifaa hiki kinafungwa nje, kinakupa taarifa za hali ya joto, kasi ya upepo, mvua, na UV. Kifaa hiki ni uwekezaji bora kabisa kama unahitaji kujua taarifa za hali ya hewa ili uweze kufanya maamuzi ya lini upande au kuweka vifaa vya kumwagilia.

solution smart home

Kuhusu vifaa vya kumwagilia, unaweza kuokoa kiasi kikubwa cha umeme kama tu utafanya mchakato wa kumwagilia kiwanja chako kuwa cha kidigitali. TIS technology inachofanya ni kurekebisha ufanyaji kazi wa kifaa chako cha kumwagilia kwa kulingana na hali ya hewa ili kiwake pale tu kinapohitajika. Kifaa hiki bora cha kiteknolojia kinakupunguzia kazi hii ngumu ya kumwagilia na pia kukupunguzia bili.

Kipindi cha kiangazi, unapopunga upepo nje jioni na familia na marafiki, unaweza kutaka kufurahia kutazama filamu nje kwa kutumia baadhi ya vifaa vyetu suluhishi. Tazama filamu ya mapenzi ukiwa na mchumba wako chini ya nyota, au tumia skrini kuonyesha picha zako za utotoni katika sherehe ya kushtukiza ya siku ya kuzaliwa ya mtoto wako.

Cheza mziki uupendao katika uwanja wako nyumbani; sio lazima iwe ndani tu. Kutegemea na aina nyingi mbalimbali za muziki zilizopo, kuna teknolojia nyingi tu za spika za nje pia. Spika zetu janja zisizokuwa na waya, za ubora wa hali ya juu, rahisi kubebeka, na zinaweza kucheza muziki kutokea sehemu yoyote ya uwanja wako, bila kujali ni spika ya jiwe iliyojificha katika bustani au spika isiyopitisha maji iliyo katika bwawa la kuogelea.

solution smart home

Kama una bwawa la kuogelea, hakikisha linang’arishwa na taa janja za LED. Taa zetu janja mbalimbali zitakuwezesha kuhifadhi muonekano wa bluu na kuvutia katika uwanja wako.

Mwisho wa siku, haijalishi namna unataka uwanja wako uonekane, kuna kifaa kipo kitakachokusaidia kufanya eneo hilo kuwa bora zaidi, na TIS technology ipo hapa kukusaidia kuchagua kile kilicho bora zaidi.

solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home
solution smart home

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK