Sikuhizi, uhitaji wa huduma za afya zenye ubora unakua. Wagonjwa wana matarajio makubwa juu ya ubora wa huduma ya afya watakayoipokea, na uongozi wa hospitali umezidi kuwa mgumu kutokana na ongezeko la kanuni ngumu za kufuata. TIS inakuletea teknolojia janja ili kuongeza ufanisi, kutoa huduma zinazomjali zaidi mgonjwa kwa kutumia fursa kuu katika usimamiaji.
Tunakusaidia kutengeneza hospitali ya kijanja ambayo kila chumba kinakuwa kimefungwa na suluhisho la kijanja ambalo linasaidia kuboresha mahusiano kati ya mgonjwa na nesi. Mfumo wetu wa Nurse Call System una kitufe cha kuita kinachoweza kufungwa pembeni tu ya kitanda cha mgonjwa. Pia, kama kikifungwa na kipaza sauti cha Kihisio chetu cha Afya (Health sensor), inawezesha mgonjwa kupiga simu kwa nesi wahusika kwa urahisi kama wakihitaji msaada.
Kuhifadhi joto na unyevu kuwa katika kiwango sawa ndani ya chumba cha mgonjwa ni muhimu sana, kwa kutumia kihisio chetu cha Health Sensor, sio kazi ngumu kabisa. Suluhisho hili linatazama na kugundua gesi hatarishi ndani ya nyumba huku kikisaidia kuweka hewa safi. Hebu fikiria faida za suluhisho hili kwa timu nzima ya uongozi wa hospitali: wanaweza kusimamia mazingira ya afya wakiwa mbali kwa kulingana na hali ya hewa ya nje pamoja na hali ya kiafya ya mgonjwa fulani, wanapewa taarifa moja kwa moja kama hali ya hewa ya ndani ni hatarishi, wanaweza kuepuka ukuaji wa kuvu (mold) kwa urahisi zaidi, na mengine mengi.
Kihisio chetu cha Pressure Sensor ni teknolojia nyingine muhimu ya kijanja kwa vituo vya afya. Suluhisho hili, linakuja na msaada wa upande wa tatu (3rd-party support), ni nzuri kwa kuwaangalia wagonjwa wenye hali mbaya kiafya au ulemavu inapotokea wakidondoka kitandani. Kama mgonjwa akidondoka kutoka kitandani kwake, kihisio chetu cha pressure sensor moja kwa moja kinamtaarifu muuguzi, hivyo kupunguza hatari ya maumivu.
TIS wana kifaa kingine tena cha kipekee kwa ajili ya watoa huduma za afya. Bedwetting Sensor ni kihisio kinachohisi unyevunyevu na kutoa taarifa. Hili linaweza kuwa ni suruhisho bora zaidi katika hospitali za watoto, nyumba za wazee, na kwingine ambapo inaweza kuwasaidia watoa huduma kutoa huduma nzuri zaidi. Kihisio hiki kinachofanya ni kutoa taarifa tu pale unyevunyevu utakapogundulika.
Mwisho, tunaona fahari kutangaza kwamba ubunifu wetu unaboresha mfumo wa hospitali wa BMS, kwa kuwa bidhaa zetu zaidi zimetengenezwa kwa ajili ya kuwasha taa, viyoyozi, mageti, makufuli, kengele, na vingine zaidi kwa namna rahisi kadri iwezekanavyo. Vifaa vyote vya kutengenezea vinapatikana kwa urahisi katika programu moja, hivyo hospitali inaweza kusimamia afya na usalama wa kila chumba kwa kubonyeza kidogo tu.
Nyongeza, ufanisi ni kiini cha kile tunachokitoa. Bidhaa za TIS ni rafiki kwa mazingira katika muundo na pia katika ufanyaji kazi. Vihisio vyetu vinagundua mwendo na kuwasha taa au mifumo ya kiyoyozi kulingana na kama kuna mtu ndani. Kwa kutumia suluhisho za TIS, kituo chako cha afya kitakuwa na ufanisi zaidi wa nishati na kupoteza kiasi kidogo sana cha nguvu katika matumizi.
TIS Control imeweka jitihada katika kukupa suluhisho bora zinazoendana na mipangilio na mazingira tofauti. Tupo hapa kukusaidia kuboresha kituo chako cha afya kuwa cha kisasa kwa bei iliyo rafiki kabisa.
We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha