TIS ilishiriki katika Jukwaa Linaloongoza Duniani La Ubunifu wa Kielekroniki; Mfumo wa AIR Unafanya Kila Kitu Kuwa Rahisi.
Maonyesho ya HKTDC Hong Kong Electronics Fair (Majira ya Vuli) 2017 kulikuwa na zaidi ya washiriki 3,740 walioonyesha na kutoa fursa kwa wageni kufanya mawasiliano na watengenezaji wa teknolojia, wasambazaji na makampuni yanayoanza ya ubunifu.
Katika jukwaa la kimataifa, TIS Automation group ilitambulisha mfumo wake wa AIR na kukaribisha wageni kutazama sifa zilizo rafiki kwa mazingira za itifaki hii ambazo sio tu zinaongeza kasi na urahisi, bali pia ina viwango vya DIY na ni rahisi sana kufanyia kazi.
Mfumo wa TIS AIR unatoa suluhisho kadhaa ambazo zinatimiza mahitaji ya aina tofauti kama vile kuwasha/kuzima taa/Kupunguza mwanga, motor, viziba mwanga dirishani, joto, kuokoa nishati na ulinzi. Inawezesha nyumba yako kujisimamia kwa vifaa vya chapa moja na kuunganishwa na mtandao wa BUS; inawezekana kwamba, kama kuna sehemu ya mfumo janja wa nyumba inatumia waya, suluhisho likaunganishwa nayo pia.
Kwa maelezo ya wataalamu wa kidigitali wa TIS waliohudhuria maonyesho haya, idadi ndogo ya swichi, muonekano mzuri wa ndani, uthibiti kwa kutumia rimoti na uwezo mkubwa wa kujiendesha ni baadhi ya faida chache za itifaki ya TIS AIR. Lakini kipekee kabisa faida kubwa kuliko zote za mtandao huu ni kupungua kwa matumizi ya nishati.
Wageni wa onyesho hili walikaribishwa kuchukulia uzito sera za ufanisi katika matumizi ya nishati na kujaribu kuona urahisi unaoletwa na mfumo wa TIS AIR katika sekta yoyote ambayo wanafanyia kazi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TIS, Turath Mazloum anaamini kwamba kama tukianza kuweka maarifa yetu ya kidigitali katika kutengeneza vifaa suluhishi ambavyo ni rafiki kwa mazingira, tunaweza kutegemea kwamba sayari yetu itaendelea kuwa salama na ya kijani kwa mara nyingine na hii ndiyo sababu teknolojia za kisasa ni za muhimu sana.
We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha