Marekani ya Kijani
Japokuwa nyumba nyingi Marekani zinazidi kuwa za kijanja na watu wanawezeshwa kutazama chakula chao ndani ya friji kwa kupitia simu zao za mkononi, lakini bado kuna uwepo wa pengo la teknolojia janja. Hii inaweza kuwa ni kwa sababu mbalimbali: kutokuwa na ufahamu, gharama, na kutokutazama madhara ya ongezeko la joto duniani.
TIS Automation Group ilihamisha ofisi kwenda eneo jipya kubwa zaidi la ofisi mjini Dallas, TX. Malengo ya timu yetu iliyoko Marekani ni kuwakilisha huduma janja kwa wote, kuonyesha kwamba vifaa janja ni suluhisho sio tu kwa matajiri wakubwa ambao kila mara wanatafuta kitu cha tofauti na kipekee cha kununua.
Lengo lingine la muhimu ni kusaidia kuokoanishati kwa njia iliyo rafiki zaidi kwa mazingira huku wakirahisisha mambo kwa kiwango fulani. Vihisio(sensors), moduli, itifaki zinazoingiliana na vifaa vingine (intergraba protocols), na paneli za ukutani kutoka TIS sio tu kwamba zinaleta amani kwa watu walio hatarini na kwa walezi wao lakini pia vifaa hivi vinaongeza ulinzi na kuokoa fedha nyingi.
Tunataka kufanya maisha ya watu yawe rahisi zaidi. Kila muuzaji na mfungaji wa vifaa vya TIS amejikita katika kutoa vifaa suluhishi bora kabisa kusaidia katika kurekebisha joto, taa, na mahitaji ya motor. Lakini muhimu zaidi ni kwamba, tunataka kufanya miji iwe na ufanisi zaidi na kupunguza upotevu wa nishati.
Kwa kutumia TIS smart technology, wateja wetu wanaweza kusimamia joto, taa, unyevu, mapazia, motor, na pia kufanya karibu kila kitu wanachotaka kiweze kujiendesha na kuwa sehemu ya kufanya Marekani kuwa ya kijani na endelevu.
We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha