TIS booth and seminar at TurkeyBuild Istanbul, Turkey

TIS iliwasilisha kifaa chake sulihishi kipya katika nyanja ya ubunifu wa kiteknolojia na muundo wa kidigitali; Energy Servant Sensor, ambacho sasa kinapatikana kwa manunuzi, kilitambulishwa katika onyesho la TurkeyBuild nchini Uturuki.

Onyesho hili ambalo ndilo onyesho kubwa katika jengo la mji huo la maonyesho ya majengo na vifaa vya ujenzi na teknolojia lilifanyika Julai 2019 na lilikaribisha wataalamu, wauzaji wa jumla, wakandarasi na wataalamu wa kidigitali wengi. 

Mnamo siku ya 4 ya maonyesho hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TIS aliendesha semina juu ya kuokoa nishati mjini Uturuki na alisisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia janja katika kuokoa sayari. Turath Mazloum alitambulisha kifaa ambacho kinawawezesha watumiaji kuongeza ufanisi katika matumizi yao ya nishati huku wakifurahia teknolojia mpya elevu ya kusimamia taa na joto. ES 10F sensor ni kihisio cha darini cha mwendo cha PIR ambacho kinakuwezesha kusimamia taa na joto bila kuhitaji kuwepo. 

Lengo kuu la muhimu la kutambulisha kihisio cha TIS ES sensor ilikuwa, Bw. Mazloum alisema, ni kumkumbusha kila mmoja wetu kwamba kuchukulia sera ya kuokoa nishati kwa uzito ni muhimu sana katika kuboresha sekta. ES sensor ilitambulika kama kifaa kilichotengenezwa ili kuepusha upotevu wa nishati kwa kutazama kwa ukaribu taa na kiyoyozi nyakati tofauti tofauti za siku. Suluhisho hili ni – kama mwakilishi wa TIS alivyosema – la umuhimu mkubw kwa matumizi ya majumbani na ya kibiashara kwa mtumiaji anayetaka kupunguza matumizi makubwa ya nishati.

Salamu nyingi ziende kwa Muhendislik Tecnoloji wa TIS kwa kuandaa stendi ya TIS. Bidhaa ilipendwa na Waturuki wengi  pamoja na wageni wa kutoka nje wanaotoka katika sekta tofauti za ujenzi. TIS Automation Group inatarajia kuona matumizi mengi zaidi ya teknolojia janja majumbani ndani ya miji ya Uturuki. Tunatazamia kuona miradi mingi zaidi ya kidigitali ndani ya Istanbul. Kwa kuwa, Uturuki na miji yake mizuri kama vile Istanbul, Izmir, Ankara, Antalya, n.k. sasa iko tayari kusimama na kutambulika kama miji inayotembelewa na watu wengi zaidi duniani kwa kukuza matumizi ya uchumi fanisi na rafiki kwa mazingira.

Wageni kutoka Istanbul, Ankara, Izmir, Konya, Bursa, Adana, Gaziantep, Antalya na kutoka miji mingine walikuja kutembelea banda letu.

TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image
TIS Website News Image

We use cookies to personalize content, customize and analyze advertising and ensure the safe use of the site. By clicking or navigating this site, you consent to the collection of information at www.tiscontrol.com and beyond using cookies. More information are available in the document: Sera ya Faragha

OK